Tafuta

Vatican News
Lazima kulinda na kuwatetea watoto na watu wengine waathirika na mikakati madhubuti itekelezwe ya ulinzi wa watoto waathirika Lazima kulinda na kuwatetea watoto na watu wengine waathirika na mikakati madhubuti itekelezwe ya ulinzi wa watoto waathirika 

Caffo:Mipango mipya ya Vatican kwa ajili ya ulinzi wa watoto!

Mwanzilishi wa simu ya dharura itwayo telefono Azzurro na mjumbe wa Tume ya Kipapa ya ulinzi wa watoto amesimulia juu ya hitimisho la mkutano mkuu wa mwaka.Kiini cha kazi yao ilikuwa ni kusikiliza wathirika na uwajibikaji wa maaskofu na watawa.Kuna hitaji la malezi endelevu ya wakleri na walei ulimwenguni.Ni lazima kubuni mikakati yenye kutekelezeka kwa ajili ya ulinzi wa watoto.

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican

Mwanzilishi wa simu ya dharura iliyopewa jinia (telefono azzura) na mjumbe wa Tume ya kipapa ya ulinzi wa watoto Profesa Ernesto Caffo katika Mkutano Mkuu wa  mwaka, uliofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 15 Septemba 2019 amewataka wafanyakazi kuwasikiliza waathirika pamoja na uwajibikaji wa maaskofu na watawa. Taarifa iliyotolewa na Federico Piana mwandishi wa Radio Vatican na Profesa wa Mawasiliano katika Chuo Kukuu cha Kipapa cha Santa Croce inasema, kumekuwepo na uhitaji wa kipekee katika kuwajibika kwa maaskofu na watawa katika kutoa taarifa kwa Baba Mtakatifu. Profesa Ernesto Caffo ambaye pia ni mjumbe wa Tume ya kipapa kwa ajili ya ulinzi wa watoto amesema, wameweka mikakati ya utatuaji wa matatizo nchini Poland na Amerika ya kusini inayotarajiwa kufika katika kila nchi.

Katika kusisitiza, Profesa Caffo, amesema kuna hitaji la malezi endelevu ya wakleri na walei ulimwenguni na lazima kubuni mikakati yenye kutekelezeka. Kwa kipindi hiki Tume  hiyo imependekeza mipango  hiyo ambayo pia inalenga Afrika na Asia yenye malengo ya kuwa na malezi endelevu na stahiki na Maaskofu wanayo fursa kubwa ya kushiriki katika malezi ya wakleri na ulinzi wa  watoto.  Aidha msisitizo zaidi umewekwa katika kuwasikiliza waathirika na kutafuta namna ya kuwasaidia. Mchakato huo unahitaji umakini wa hali ya juu hasa katika kubaini madai ya kweli ya waathirika na wahitaji. Tume  hiyo inaendelea pia na mkakati wake wa kushirikiana na vyombo vya serikali ya kila nchi kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu. Mipangilio ya usikilizaji wa kesi hizo utawekwa kwa kila jimbo na katika ofisi za uwakilishi wa Vatican ili kurahisisha uwajibikaji katika sekta hiyo nyeti.

Katika mkutano huo wa mwaka wajumbe waliweza kufanyia kazi miongozo na ufafanuzi katika mazingira yanayopaswa kupewa kipaumbele maana waathirika siyo watoto tu bali pia na marika mengine. Hatua za utambuzi, utekelezaji na uwajibikaji kwa walengwa wa nyanyaso hizo zinahitaji uwazi wa hali ya juu. Hii itahitaji kuwepo na miundo mbinu ya kuwasaidia wale wasioweza kujitetea. Ikumbukwe kuwa hii ni kazi kubwa  ya kukabiliana na mila na tamaduni nyingi duniani kote ili kufikia mabadiliko ya kweli. Mkutano huo wa Tume ya kipapa utaendelea tena kuanzia tarehe 24 hadi 25 septemba 2019 kwa ajili ya uboreshaji katika hutoaji wa huduma hiyo.

TELEFONO AZZURRA
19 September 2019, 13:37