Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko akiwa na Baraza la makardinali washauri katika kikao kinachoendelea Vatican hadi tarehe 19 Septemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko akiwa na Baraza la makardinali washauri katika kikao kinachoendelea Vatican hadi tarehe 19 Septemba 2019  (© Vatican Media)

Mkutano wa Baraza la Makardinali washauri wa Papa kuanza mjini Vatican!

Tarehe 17 Septemba 2019 mjini Vatican umefunguliwa Mkutano wa 31 wa Baraza la Makardinali washauri wa Baba Mtakatifu,kwa ushiriki wa Papa mwenyewe Mkutano huo utamalizika tarehe 19 Septemba 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 17 Septemba 2019 mjini Vatican umefunguliwa Mkutano wa 31 wa Baraza la Makardinali washauri wa Baba Mtakatifu,kwa ushiriki wa Papa mwenyewe Mkutano huo utamalizika tarehe 19 Septemba 2019. Katika kiini cha mkutano ulioanza tarehe 25-27 Juni 2019, mada kuu ilikuwa ni juu ya Katiba Mpya ya Kitume, ambayo inahusu juu ya madiliko ya Sekretarieti Kuu ya Vatican kwa mswada unaojulikana   “Praedicate evangelium,  yaani Hubirini Injili” kama alivyo kuwa amethibitisha katika Mkutano na waandishi wa habari Vatican, Katibu Mkuu wa Baraza la Makardinali washauri, Askofu Marcello Semeraro.

Hata hivyo tarifa zaidi zinaeleza kuwa umuhimu wa Muswada wa kipapa uanataka kujikita kuchukua nafasi ya Katiba ya zamani ya Kitume inayojulikana kama “Pastor Bonus” yaani “Mchungaji Mwema”, ya Mtakatifu Yohane Paulo II iliyotangazwa kunako  tarehe 28 Juni 1988. Utume wa Muswada mpya kwa mujibu wa matashi ya Baba Mtakatifu Francisko umejieleza tayari katika Wosia wa Kitume wa “Evangelii Gaudium” yaani Furaha ya Injili”, kama alivyokuwa amesema Askofu Semeraro kwamba msisitizo ni “enendeni mkahubiri duniani kote”,  ambacho ni kifungu kutoka Injili ya Matakatifu Marko, na ambayo leo hii inapaswa kwa dhati kusomwa zaidi kwa mantiki ya kuendelea katika mabadiliko ambayo ni kutangaza Habari Njema kwa kila kona ya dunia .

Aidha Makardinali walikuwa wamesisitiza hata shughuli ya kina ya mapendekezo na kusikiliza Katiba moja ambayo itafuata shughuli yake ya mwisho na kuiwakilisha kwa Baba Mtakatifu  ili kutoa uthibitisho wa makubalinao yake ya mwisho. Askofu Semeraro alikuwa amesema kuwa, mabaraza yote ya  kipapa Vatican waliweweza kutoa majibu yao, mapendekezo na Mswada huo pia ulitumwa kwa marais wote wa mabaraza ya maaskofu kitaifa mahalia, Sinodi za Makanisa ya Mashariki, Mabalozi wa Vatican duniani kote, mabaraza ya wakuu wa mashirika makuu na baadhi ya vyuo vikuuu vya kipapa ambavyo vitaendelea kutoa majibu yao.

Kwa sasa Baraza la washauri wa Baba Mtakatifu ni makardinali sita ambao: Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, Kardinali Oscar Andrès Rodrìgues Maradiaga, Kardinali Reinhard Marx, Kardinali Seàn Patrick O’Malley, Kardinali Giuseppe Bertello, Kardinali Oswald Gracias pamoja na Kardinali Giuseppe Bertello. Aidha katika Baraza wapo pia wengine ambao ni Askofu Marcello Semeraro, katibu mkuu wa Baraza la makardinali washauri kwa kusaidiwa askofu Marco Mellino.

18 September 2019, 12:31