Tafuta

Papa Francisko amemteua Monsinyo Carlo Maria Polvani kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Utamaduni. Papa Francisko amemteua Monsinyo Carlo Maria Polvani kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Utamaduni. 

Mons. Carlo Maria Polvani ateuluwa kuwa Katibu mwambata: Baraza la Kipapa la Utamaduni

Monsinyo Carlo Maria Polvani alizaliwa tarehe 28 Julai 1965 huko Jimbo kuu la Milano, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi alipewa Daraja takatifu ya Upadre tarehe 14 Februari 1998. Katika maisha yake ni kiongozi aliyebahatika kupata elimu ya juu na mang’amuzi makubwa ya kitamaduni kutoka Canada, USA na Italia. Mwaka 1999 alianza utume wake Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Carlo Maria Polvani kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Utamaduni. Monsinyo Carlo Maria Polvani alizaliwa tarehe 28 Julai 1965 huko Jimbo kuu la Milano, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi alipewa Daraja takatifu ya Upadre tarehe 14 Februari 1998. Katika maisha yake ni kiongozi aliyebahatika kupata elimu ya juu na mang’amuzi makubwa ya kitamaduni kutoka Canada ambako mwaka 1985 alijipatia shahada ya uzamili katika masuala ya kemia ya kibayolojia kutoka Chuo Kikuu cha McGill, kilichoko Montreal nchini Canada. Baadaye akajiendeleza zaidi na kunako mwaka 1990 akajipatia shahada ya uzamivu.

Mwaka 1993 akaanza kugeuza mwelekeo na kuzama zaidi katika masuala ya kitaalimungu na hatimaye, kujipatia shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Taalimungu cha Cambridge, nchini Marekani. Baadaye alirejea nchini Italia na kuendelea na masomo ya Sheria na Kanuni za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian na kujipatia Shahada ya uzamili kunako mwaka 1996 na hatimaye, kujipatia Shahada ya uzamivu katika Sheria, Taratibu na Kanuni za Kanisa kunako mwaka 1999. Akaanza utume wake wa shughuli za kidiplomasia ndani ya Vatican kunako mwezi Julai 1999. Tangu wakati huo, akatumwa kutekeleza utume wake kwenye Ubalozi wa Vatican nchini Mexico.

Tangu mwaka 2001 akarejeshwa tena kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican kama Afisa mtendaji wa mawasiliano, hifadhi za nyaraka na mratibu wa ofisi za ufundi za Vatican. Alikuwa pia ni mjumbe mshauri wa uongozi wa Vatican kuhusiana na masuala ya mitandao ya kijamii na pia alikuwa ni mjumbe wa Kamati ya “Internet Corporation for Assigned Names and Numbers” (ICANN). Kunako mwaka 2015 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa ni mjumbe wa Vyombo vya Mawasiliano vinavyomilikuwa na kuendeshwa na Vatican pamoja na kuwa ni mjumbe wa Kamati Tendaji ya Teknolojia na Mawasiliano ya Vatican. Ni mwandishi mahiri wa mada za kisayansi kimataifa!

Katibu Mwambata
29 July 2019, 09:32