Tafuta

Vatican News
2 Juni ni siku ya 53 ya Upashanaji habari duniani 2019, na kaulimbiu "Kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo:Jumuiya ya mtandaoni kwenda kwenye Jumuiya halisi ya watu 2 Juni ni siku ya 53 ya Upashanaji habari duniani 2019, na kaulimbiu "Kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo:Jumuiya ya mtandaoni kwenda kwenye Jumuiya halisi ya watu 

Dk.Ruffini:Sisi sote ni wahusika wa mawasiliano na tunawajibika katika mtandao!

Ikiwa mabilioni ya watumiaji wa mtandao watajitahidi kutoa matunda ya mitandao ya wakati endelevu katika kugawanya kanuni msingi na kutuunganisha sote,ndipo mtandao utatufanya tugundue kwa upya kuwa kila mmoja ni mshiriki na mwajibikaji.Ni kwa mujibu wa Dk.Paulo Ruffini wakati akitafakari Ujumbe wa 53 wa Upashanaji Habari Duniani 2019. Mtandao ni kwa ajili ya kuunganisha na siyo kutenganisha!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wakati wa Mtandao unatuambia kuwa ulimwengu wa mawasiliano siyo tena dunia yenye kuwa na umbali zaidi uliotengezwa na wataalam, waandishi wa habari, wawawakilishi hata kama ilikuwa hivyo nyakati ziliozopita. Ni dunia yetu. Ni ulimwengu wa watu.Na  ikiwa mabilioni ya watumiaji wa mtandao watajitahidi wenyewe kuzaa matunda ya mitandao ambayo kwa wakati endelevu itahusika kugawanya kanuni msingi na kutuunganisha sote, ndipo mtandao utatufanya kujigundua kwa upya kuwa kila mmoja ni kama mshiriki na mwanachama. Vinginevyo, ikiwa tutafikiria ni kujikita katikati ya wali sawa na hata zaidi ya wangine tutaishia kupotea wenyewe. Huu ni uthibitisho wa Dk. Paulo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, wakati akitafakari ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa siku ya 53 ya Upashanaji habari duniani 2019, ambapo ujumbe huo umetangazwa katika Kitabu kiitwacho “Kutoka Jumuiya ya mtandaoni kwenda kwenye Jumuiya halisi ya watu” (Toleo la  Scholè).

Mtandao kwa ajili ya kuunganisha na siyo kutenganisha

Dk. Paulo Ruffini katika tafakari yake ameandika kuwa, mara nyingi kuna haja ya mtu mwingine wa kuelekeza mambo ili kuyatazama, hata kama yapo mbele ya macho yetu. Hata tunapokuwa ndani mwake. Hii ni kutokana na kwamba mara nyingi mtazamo wetu ni mfupi  hauwezi kusimama peke yake na kutazama juu. Kwa kinagaubaga ndiyo lengo ambalo Baba Mtakatifu Francisko anaonesha katika ujumbe wake wa Siku ya 53 ya upashanaji wa habari duniani 2019 ambayo imeadhimisha tarehe 2 Juni 2019, ikiongozwa na mada “Kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo (Ef4,25): Kutoka Jumuiya ya mtandaoni kwenda kwenye Jumuiya halisi ya watu.

Kwa uvumilivu ambao changamoto za kisasa katika ukosefu wa uvulivu, Baba Mtakatifu anatupeleka katika mwanzo wa historia yake binafsi, ya kwetu: na mwanzo wa historia ya pamoja ile ya mawasiliano ya kijamii katika wakati wa Mtandao; ili kuweza kuepuka hatari ambazo kwa pande zote mbili zinapotea na kuelekea katika kuvunjika vipande vipande. Kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo, lakini siyo namna ya kusema, bali ni  ukweli ambao sisi mara nyingi tunaukana. Na hii mara nyingi ni kishawishi cha mtu, kuvunja kile ambacho kinatuunganisha na kuwa sehemu yake, kwa kujidanganya wenyewe kwamba tunaweza kutenganisha hatima yetu kutoka kwa wengine; na pia akili ya mtu binafsi kutoka nafsi ya mtu. Kiukweli mgawanyiko ni kitambulisho cha wakati wetu na ambacho kimeunganishwa na upweke wa kina kutokana na mawasiliano na waathirika wa kutokuwasiliana.

Kuna uwezekano wa kuchat na sura mbili au tatu kwa wakati mmoja

Akiendelea na ufafanuzi wa Ujumbe huo Bwana Ruffini amesema kama alivyo andika Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wa Kitume wa Gaudet et Exsulatae, leo hii kuna uwezekana wa kuchat katika sura mbili au tatu kwa wakati mmoja na kuunganisha mambo mengi tofauti kwa wakati mmoja. Lakini bila kuwa na hekima ya mang’amuzi hayo tunaweza kugeuzwa kwa urahisi kuwa bidhaa za michezo katika tabia hiyo ya wakati. Hayo yote Baba Mtakatifu  Francisko anathibitisha ni changamoto duniani ya mawasiliano katika mchakato wa njia ndefu ya uwezo. Badala yake, kuna njia fupi ambayo inajiwakilisha kama vile mtu mwenye uwezo wa kutatua matatio yote, au kinyume kama kuwatupia mizigo ya kila uwajibikaji. Inahitajika kwa harak kutafuta suluhisho katika kuwakilisha hali halisi hii. Ni katika mchakato wa dasa wa mawasiliano ambayo yanakwenda haraka na hakuna wakati wa kutafakari. Hii ndiyo mpaka, wa wakristo katika mawasiliano. Hii ndiyo uwajibikaji. Ndiyo utume. Kila siku, watoto wetu, wajukuu wetu wanaweza kuuliza je tulikuwa wapi?  Iwapo hatuoni mahali tulipo, ipo hatari ya kuwa vipofu wanaoongoza vipofu wengine ambao badala ya kujenga wakati endelevu, tunauharibu. Mbele ya yule anayepanda mgawanyo, mbele ya yule anajifikiria anapambania ustaarabu uliogeuka kuwa kinyume chake, jibu moja lenye uwezekano ni lile kuanza  mwamzo kabisa!

Kupanga  kwa pamoja ni siasa. Kupanga peke yake ni tamaa

Akitazama juu ya kauli mbiu “Sisi ni kiungo na wengine”, anaandika kuwa,  mtandao ulizaliwa kwa ajili ya kuunganisha na siyo kutengenisha. Kwa ajili ya kushirikishana wema, uzuri, utambuzi na siyo uovu, ubaya na habari za kugushi. Akikimbuka Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko katika kaburi la Padre Lorenzo Milan, Bwana Ruffini anasema, Baba Mtakatifu alikumbusha leo hii  watu ambao wamegawanyika na kuchanganyikiwa ya kwamba, "nimejifunza kuwa matatizo ya wengine ni sawa na matatizo yangu. Kupanga wote kwa pamoja ni siasa. Kupanga peke yake ni tamaa”. Hata hivyo ameongeza kusema, kinachooneka , utafikiri ni suala la maneno , lakini kiukweli ndani ya mtandao ni jamuiya ya dhati, ni suala halisi  la wakati wetu, na ambalo linakuwa kwa haraka sana na kuchanganyikiwa, maisha kuwa na umoja na kugawanya, kuwa na ujasiri pia  hofu. Ni suala ambalo linahusu kila mmoja wetu kama mtu na sisi sote kama binadamu. Hili ni suala linalohusiana kati ya mwanadamu (wote, katika mwili na mfupa, nafsi na mwili) na teknolojia; njia ambayo teknolojia inabadilika (kwa sababu gani inabadilika) uhusiano kati ya watu; kwa uhakika ni asili ya yetu).

Kwa hakika inahitaji sisi kuwa na busara wa kubadilisha Mtandao ukawa katika matumizi halisi. Mpango usiwe wa kuingia mtandaoni na kuwa  mahali penye  hatari ya kupotea, badala yake pawe ni mahali pa kuelekeza kwa dhati umoja wa upamoja  na kuunda utambulisho. Ujumbe wa Baba Mtakatifu unatualika kutafakari kwa kina dharura ya kubadilisha mtandao ukawa na maana iliyo nzuri, kuwa sehemu ya mazungumzo, ya utambuzi, ya mahusiano na ushirikishwaji. Ni mwaliko wa wote na uwajibikaji  na changamoto kwa wote katika kujibu wote tunavyoalikwa katika kaulimbiu  “Kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo (Ef 4,25):Kutoka Jumuiya ya mtandaoni kwenda kwenye Jumuiya halisi ya watu.

Padre Maffeis:(Cei)WeCa,imetimiza 25° kwa ajili ya ya kuendeza ujumbe wa  Papa

Baba Mtakatifu Francisko anaweka kidole chake juu ya jeraha wakati akitoa angalisho la kutokuwa wabobeaji wa kidigitali na kujikinga kama ilivyo mara nyingi mbele ya vioo vyetu. Baba Mtakatifu Francisko amatushawishi kuishi kwa namna ya kukamilisha utamaduni wa kidigitali na kukutana kwetu kama  mwili na mfupa. Ikiwa mambo haya yanatokea, Baba Mtakatifu ni wa kwanza kutambua kwamba tumebobea kwa nguvu katika mazingira ya kiteknolojia na ambayo sisi ni sehemu pia huleta uwezo wake kamili. Haya yamethibitishwa na Padre Ivan Maffeis, Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasilinao ya kijamii ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI) wakati wa fursa ya Miaka 25 tangu kutangazwa kwa WeCa, inayoijita kutangaza Ujumbe Papa katika tukio la maadhimisho kwa ajili ya Siku ya 53 ya Upashanaji habari duniani 2019, ambayo imeadhimisha tarehe 2 Juni 2019.

03 June 2019, 09:45