Tafuta

Ijumaa ya kwanza ya kusali wakati wa Mfungo wa Ramadhan Ijumaa ya kwanza ya kusali wakati wa Mfungo wa Ramadhan 

Wakristo na waislam wanahamasishwa kuwa na udugu wa kibinadamu!

Kama ilivyo utamaduni wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini katika kuanza mwezi wa Ramadhan kwa waislam wote duniani,Baraza limeandika ujumbe wake kwa kuhamasisha mazungumzo,heshima ya uhuru wa mawazo na imani.Haitoshi tu kuwa na tabia ya uvumilivu,bali tunahitaji umoja wa kweli wa kuishi kidugu na amani.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Ikiwa ni mwezi wa Ramadhan, ambao unajikita katika kufunga, sala na kutoa sadaka, pia ni mwezi wa kuongeza juhudi za uhusiano kiroho na ambao unashirikisha katika urafiki kati ya wakaristo na waslam, kwa maana hiyo ni furaha kubwa kutumia fursa hii, ili kuwatakia maadhimisho mema yenye utulivu na ufanisi wa Ramadhan. Ndiyo mwanzo wa ujumbe wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini ambapo kama ilivyo utamaduni wa kuwasindikiza na matashi mema katika mfungo wao wa Ramadhan  kwa waslam  wote duniani kote umetolewa tarehe 9 Mei 2019. Ujumbe huu unaongozwa na kauli mbiu: “wakristo na waslam:kuhamasisha udugu wa kibinadamu duniani kote”. Katika ujumbe uliotiwa sahini na Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Askofu Miguel Ángel Ayuso Guixot, M.C.C.J unasema, dini zetu zinatualika kubaki tumesimama kidete na kuwa na thamani za amani; kusaidia thamani za uelewa wa pamoja, wa udugu wa kibinadamu na kuishi kwa pamoja; kuwa na msimamo wa hekima, wa haki na upendo(Kutoka katika Hati ya  udugu wa kibiadamu kwa ajili ya amani duniani na kuishi kwa pamoja uliotiwa sahini huko,Abu Dhabi, tarehe 4 Februari  2019).

Kuwa na  moyo kupeleka mbele utamaduni wa mazungumzo

Katika ujumbe huo unasema unasema “Sisi kwa maana hiyo tunatiwa moyo wa kuendelea kupeleka mbele utamaduni wa mazungumzo kama chombo cha kushirikiana, na kama mtindo wa kukua kwa uelewa wa pamoja. Katika mantiki hiyo, ujumbe unakumbusha kwamba Baba Mtakatifu Francisko wakati wa ziara yake mjini Cairo, alionyesha miongozo mitatu msingi ya kufuata katika mazungumzo na ili kuweza kuwa na  na maelewano na dini mbalimbali. Na miongozo hiyo ni kama: “wajibu wa utambulisho, ujasiri wa kuwa na uwiano, na nia wazi (rej, Hotuba ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa amani katika kituo cha Al-Azhar, tarehe  28 aprile 2017)

Waislam na wakristo tunaalikwa kujifungua mmoja na mwingine

Waisalam na wakristo tunaalikwa kujifungua mmoja na mwingine, ujumbe unaendelea kwamba, kutambuana kama ndugu kaka na dada. Kwa kwa kufanya hiyo kwa dhati tunaweza kuangusha kuta zilizo inuliwa za hofu na ujinga, huku tukitafuta kwa pamoja kujenga madaraja ya urafiki ambayo ni msingi wa ustawi wa ubinadamu wote. Na kutokana na misingi hiyo ujumbe unathibitisha kwamba, tujitahidi kukuza hayo  katika familia zetu na katika taasisi zetu za kisiasa, za kiraia na za kidini, ili kuwa na njia mpya ya maisha inayokataa vurugu, na mtu aweze kupata heshima ya  ubinadamu wake. Na ili kuweza kuheshimu utofauti, mazungumo yanatakiwa kutafuta kuhamasisha haki ya maisha ya kila mtu, ushirikishwaji kimwili na uhuru msingi kama vile uhuru wa dhamiri, wa mawazo, wa kujieleza na wa dini. Hii ni pamoja na uhuru wa kuishi kulingana na hatua za mtu binafsi katika sekta binafsi na za umma. Kwa njia hii, Wakristo na Waislam kama ndugu kaka na dada, wanaweza kufanya kazi pamoja kwa ajili ya ustawi wa pamoja.

Haitoshi kuwa na uvumilivu bali kuwa na tabia ya kuishi kwa udugu na amani

Kwa kuhitimisha ujumbe huo kutoka Baraza la Kipapa la Mazungunzo ya kidini ni kutaka kusema kwamba ujumbe huo wa kindugu uweza kupata mwangwi hasa katika mioyo ya wale ambao wanashikilia nafasi za mamlaka katika sekta ya maisha ya kijamii na raia wa familia nzima ya wanadamu na wanaweza kutuongoza sisi sote katika kufanya mazoezi ambayo siyo tu, katika tabia ya kuwa na uvumilivu, lakini zaidi  ni ile hali ya kuishi kwa dhati na amani ya kweli. “Katika salam hizi za kindugu ninapenda kupyaisha urafiki wetu na kwa niaba ya Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini ninawatakia matashi mema ya mwezi wa Ramadhani wenye kuleta mafanikio na furaha ya ‘Id al-Fitr”.

10 May 2019, 13:42