Tafuta

Vatican News
Wanahija katika sala huko  Medjugorje Wanahija katika sala huko Medjugorje 

Papa ameruhusu hija ya kwenda Medjugorje

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa kudumu wa kutembelea Parokia ya Medjugorje Monsinyo Henryk Hoser amesema,Baba Mtakatifu ameruhusu hija ya kwenda Medjugorje.Na kwa mujibu wa Msemaji wa vyombo vya habari Dk Gisotti amethibitisha huo ni umakini huo ni kwa ajili ya kukuza na kuhamasisha matunda ya wema,japokuwa bado hakuna uthibitisho halisi wa matukio yanayo semekana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Akijibu maswali ya baadhi ya waandishi wa habari, msemaji wa mpito wa vyombo vya habari Bwana Alessandro Gisotti kuhusu hija za Medjugorje amethibitisha kuwa; kama alivyokuwa ametangaza Mjumbe maalum wa kudumu wa kutembelea kwa namna ya pekee Parokia ya Medjugorje, Monsinyo Henryk Hoser na kutoka  Ubalozi wa Vatican huko Sarajevo, Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uwezekano wa kuandaa hija za kwenda Medjugorje.

Umakini wa kuruhu hija na kutokana na wimbi la watu wa Mungu kwenda Medjugorje,

Hii ni kutokana na kujali wimbi la watu wa Mungu wanokwenda hija huko Medjugorje, na ili kuepuka hija zitafsiriwa kama uthibitisho wa matukio yanayo julikana, lakini ambayo bado yanahitaji uchunguzi wa Kanisa. Na kwa kufikiria matunda ya neema ambayo yanonekana na ambayo ni masuala yanayojikita katika umakini wa shughuli za kichungaji ambazo Baba Mtakatifu Francisko amependelea kuwa na mtazamo wa kusaidia shughuli hizo. Kutokana na hilo, Msemaji Mkuu Dk Gisotti anasema, ni lazima kuepuka kwenda bila kuwa na utaratibu au kuleta utata kwa mantiki ya mafundisho. Hii inawahusu hata wachungaji wa kila daraja la ukuhani ambao wanatarajia kwenda huko Medjugorje kuadhimisha au kushiriki kwa njia ya pekee maadhimisho ya Ekaristi.  Kutokana na hiyo Mjumbe Maalum wa Kitume, atakuwa kwa namna moja na urahisi zaidi katika kuanzisha, kuwa na makubaliano na maagizo ya maeneo hayo; aidha kuwa na  mahusiano na makuhani wanaoshughulikia au kuandaa  hija za kwenda Medjugorje na kwamba, watu wawe na  salama na kujiandaa vizuri kuwapatia taarifa na maelekezo maalumu kwa ajili ya kuwaongoza ili kuleta ufanisi wa  hija hiyo.

Ruhusa ya Hija ya Medjugorje ni kukuza na kuhamasisha matunda ya wema

Hata hivyo ili uweze kutambua zaidi ya sababu na maana ya kina ya maamuzi ya kuridhia hija ya kwenda Medjugorje kwa upande wa Baba Mtakatifu Francisko, ni vema na lazima kusoma kwa kina hatua mbalimbali za Wosia wa Kitume wa Evangelii gaudium. Katika Wosia huo wa Baba Mtakatifu anakumbusha kuwa, katika sayari ya watu, unaweza kupokea kwa mitindo mbalimbali ambayo imani inapokelewa na inaundwa katika utamaduni na kuendelea konekana...

Aidha amekumbusha zaidi akitaja hata maneno katika Hati ya mwisho ya Baraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini huko Aparecida ya kwamba, “kutembea kwa pamoja kulekea katika madhabahu na kushiriki maonesho mengine ya ibada ya watu, wakati wanampeleka mwanawake wake ndani ya roho zao au kuwaalika hata watu wengine, ni tendo lenyewe la uinjilishaji”. hivyo “Hatuna kulazimisha wala kujifanya kudhibiti nguvu hii ya kimisionari!”, Alihitimisha Baba Mtakatifu.....

/content/dam/vaticannews/pam/audio/agenzie/netia/2019/05/13/10/hija-medjugorje-135020080.mp3
12 May 2019, 14:05