Tafuta

Papa amemteua Askofu Miguel Ángel Ayuso Guixot kuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini Papa amemteua Askofu Miguel Ángel Ayuso Guixot kuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini 

Papa amefanya uteuzi wa mabalozi na Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini

Tarehe 25 Mei,Baba Mtakatifu amefanya uteuzi wa mabalozi wa Vatican katika maeneo kadhaa kama vile Fiji na Palau,kupewa Askofu Mkuu Novatus RUGAMBWA pia ni Balozi wa Vatican huko New Zealand na mwakilishi wa Kitume wa Visiwa vya Pasifiki.Aidha wengine ni Balozi wa Vatican katika ufalme wa Monako na Costa Rica na hatimaye Askofu Ayuso Guixot kuongoza Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini.

Na Sr. Angela Rwezaula Vatican

Tarehe 25 Mei, Baba Mtakatifu amewateua mabalozi wa Vatican katika maeneo kadhaa kama vile Fiji na Palau, kuwa Askofu Mkuu Novatus RUGAMBWA ambaye pia ni Balozi wa Vatican  huko  New Zealand na mwakilishi wa Kitume wa Visiwa vya Pasifiki aidha wengine ni Balozi wa Vatican katika ufalme wa Monako na Costa Rica, U.NE.P na hatimaye Askofu Ayuso Guixot kuongoza Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini.

Fiji na Palau, wamepata Balozi, Askofu Mkuu Novatus RUGAMBWA,ambaye pia ni Balozi wa Vatican  huko  New Zealand

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa Vatican huko  Fiji  na  Palau, Askofu Mkuu Novatus RUGAMBWA, ambaye pia ni Balozi wa Vatican huko New Zealand na mwakilishi wa Kitume wa Visiwa vya Pasifiki.

Mwakilishi wa Vatican wa kudumu katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa U.N.E.P.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua mwakilishi wa kudumu  katika Ofisi za Umoja wa Mataifa kwa ajili Mazingira na Makazi ya kibinadamu (U.N.E.P., UN-Habitat) Askofu Mkuu Hubertus Matheus Maria van MEGEN (Novaliciana), ambaye pia ni Balozi wa Vatican nchini Kenya na  Sudan Kusini.

Balozi wa Vatican katika ufalme wa Monaco

Baba Mtakatifu Francisko amemtea Balozi wa Vatican katika ufalme wa Monaco, Askofu Mkuu Antonio ARCARI, (jimbo Ceciri) ambaye hadi uteuzi wake alikuwa Balozi wa Costa Rica.

Monsinyo Ayuso Guizot kuongoza Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini

Papa Francesco amemteua Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini, Askofu Miguel Ángel Ayuso Guixot, mwenye umri wa miaka 66 ambaye hadi uteuzi wake alikuwa katibu mkuu wa Baraza hili. Anachukua nafasi iliyo achwa wazi baada ya  kifo cha Kardinali Jean-Louis Tauran,kilichotokea mwezi Julai 2018.

Mmisionari wa kikomboni

Askofu Ayuso Guixot alizaliwa huko Siviglia, nchini Hispania kunako tarehe  17 Juni 1952. Ni mmisionari wa Shirika lwa Wakomboni wa Moyo wa Yesu, ambaye alipata daraja la upadre kunako tarehe 20 Septemba  1980 na amewahi kujikita katika shughuli za kimisionari nchini Misri na Sudan hadi mwaka 2002.

Mtaalam wa masuala ya kiislam

Akiendelea na mafunzo yake ya juu amesomea kiarabu na Uislam katika Chuo cha Pisai Roma mwaka 1982 na kupata shahada ya dogma ya taalimungu katika Chuo Kikuu cha Granada kunako 2000. Tangu mwaka 1989 amekuwa profesa wa kiislam  kabla ya kwenda Khartoum na baadaye Cairo katika Taasisi ya kipapa ya Mafunzo ya Kiarabu na Kiislam hadi mwaka 2012 akiwa ni mkuu wa chuo hicho. Askofu Ayuso Guixot ameweza kuhutubia katika mikutano mbalimbali ya majadiliano ya kidini barani Afrika  kama vile ( Misri Sudan, Kenya, Ethiopia na Msumbiji).

Kuchaguliwa na Papa mstaafu  Benedikto XVI na baadaye Papa Francisko

Tarehe 30 Juni 2012, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alimteua Monsinyo Ayuso Guixot kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Majadiliano ya Kidini. Na kuteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu wa Luperciana na kupewa daraja la uaskofu huo kunako mwezi Machi 2016. Anaelewa vizuri lugha ya kiarabu, kingereza, kifaransa, kiitaliano ikiwa ni pamoja na lugha yake mama!

25 May 2019, 12:05