Tafuta

Vatican News
Mitandao ya kijamii, ya mawasiliano, ya watu,mitandao ya kidigital, vyote hivyo  ni muhimu katika kueneza habari ya Injili kwa wote wasio kuwa na habari hiyo Mitandao ya kijamii, ya mawasiliano, ya watu,mitandao ya kidigital, vyote hivyo ni muhimu katika kueneza habari ya Injili kwa wote wasio kuwa na habari hiyo 

Mitandao ya kijamii ni zana za kujenga na kutoa sauti kwa hasiye kuwa nayo!

Tarehe 21 Mei 2019 umefanyika Mkutano ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la mawasiliano Vatican kuhusu mada: “Kutoka katika mawasiliano ya mitandao ya kijamii kufikia jumuiya ya kibinadamu.Uzoefu wetu”.Kuwa katika mitandao katika nyakati za mitandao ya kijamii siyo hali ya kujenga ukiritimba kidigitali ni kufanya utamadunisho wa ujumbe wa kiinjili katika vyombo vya habari duniani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Video zilizowekwa katika ukurasa wa Vatican newa katika Faceboo zimetazamwa mara milioni 15. Zile ambazo zimetazamwa sana ni  zinazohusu  ziara za Baba Mtakatifu Francisko. Na kati ya hizo kuna Misa Takatifu katika uwanja wa Zayed Sports City di Abu Dhabi, mkesha wa Siku ya Vijana huko Panama, ziara ya Baba Mtakatifu huko Morocco na ile ya hivi karibu nchini Bulgaria na watoto ambao walikuwa wanacheza na mawaridi mara baada ya kupokea Komunio ya kwanza katika mikono ya Baba Mtakatifu. Kwa hakika mitandao ya kijamii ndiyo imekuwa kitovu cha mkutano katika Makao makuu ya Baraza la Kipapa la mawasiliano Vatican, tarehe 21 Mei 2019 kwa kuongozwa na tema : “Kutoka katika mawasiliano ya mitandao ya kijami kufikia jumuiya ya kibinadamu. Uzoefu wetu”.

Kupeleka ujumbe wa kiinjili katika Mtandao

Kuwa katika mtandao katika  nyakati za mitandao amesema Bwana Paulo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliani Vatican kuwa  siyo hali ya kujenga ukiritimba wa kidigitali, bali ni kutamadunisha ujumbe wa kiinjili duniani katika vyombo vya habari. Manano ya  Baba Mtakatifu tayari yako katika mitandao ya kijamii , lakini vijana wengi hawajuhi. Na ndiyo hii mitindo mipya ya kushuhudia ili waweze kujua kwanza na kuitawala baadaye wote waweza kuwa na mabadiliko ambayo yanasubiriwa. Mitandao ya kijamiii Vatican ambavyo kwa sasa inapatikana kwa luggha 23 kwenye Facebook; 6 account ya Twitter; lugha 14 katika YouTube na lunha nyingine katika Instragram . Kila siku wanasasisha habari ambazo hazitazami Vatican tu, lakini hata katika Kanisa la ulimwengu.

Tweet za Papa: tembe ya upendo katika dunia

Naye Nataša Govekar mkurugenzi wa Kitivo cha Taalimungu ya kichungaji katika Baraza la Kipapa la Mawasiliano amesisitiza kuwa “uwepo wetu katika mitandao ya kijamii, lengo lake ni kuwafikia watu mahali popote walipo. Na ili kuweza kuwapelekea Neno la Mungu kila mahali. Waamini wengi wanaishi katika maeneo ya mbali sana  na Roma na labda hawatawahi hata siku moja kuja katika uwanja wa Mtakatifu Petro kumsikiliza Baba Mtakatifu Francisko. Lakini Tweet zake katika @Pontifex zinafuatiliwa na milioni 48 ya watu katika lugha 9, kutokana na hiyo, mitandao ya kijamii inageuka kwa namna moja au nyingine  zoezi la kuweza kutafuta kile kilicho cha muhimu. Ni kama kuwasiliana kidogo vidogo kama kipande cha kidonge kidogo cha hekima au tembe ya upendo.

Kuzungumza katika mtanao kwa njia ya lugha nyingi

Naye Juan Narbona Profesa wa Chuo kikuu cha Msalaba Mtakatifu Roma  ( Santa Croce) amesema kuwa, wale ambao wanafuata kurasa za mtandao wa Vatican, siyo watu walisimama bali wanazidi kuongezea kwani,wanauliza maswali, wanadadisi, hasa kwa njia ya kutoa maelezo yao katika kurasa za Facebook. Kuna lugha nyingi katika mitandao ya kijamii  Na watu wasuburi kujifungua zaidi na wakati huo kuhusu Twitter, mara nyingi mawasiliano ni yale ya muhimu. Kinyume na Instantgram ni ulimwengu uliofunguka  ambao umeelekezwa kwa vijana zaidi;  hivyo lazima iwe hai na inayochangamka. Tunapowasiliana na mitandao ya kijamii tunapaswa kuheshimu sheria maalumu ambayo inapendekeza kuelimisha na kuwa na utaratibu mzuri wa matumizi ya lugha  kitu ambacho wakati huu kimekuwa ni kigumu kuthibiti katika mitandao amesema.

23 May 2019, 15:32