Tafuta

Vatican News
Ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II nchini  Bulgaria, mwezi Mei 2002 Ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II nchini Bulgaria, mwezi Mei 2002 

Papa Francisko nchini Bulgaria baada ya miaka 17 tangu ziara ya Mt.Yohane Paulo II

Kufika kwa Baba Mtakatifu Francisko nchini Bulgaria huko Sofia,ikiwa ni ziara ya 29 ya Kitume inayoongozwa na tema ya Pacem in terris,itakuwa ni fursa ya wazalendo kukumbuka ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II miaka 17 iliyopita.Katika ziara hiyo mwaka 2002 alikazia juu ya jitihada za pamoja kwa wakatoliki na waorthodox za kulinda amani na haki.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mtakatifu Yohane Paulo II akiwa ziarani nchini Bulgaria alimwelekeza Patriaki Maxim na wajumbe wote wa Sinodi Takatifu kuwa Ulaya nzima ikiwa ya Mashariki na Magharibi zinasubiri jitihada za pamoja za Wakatoliki na Waorthodox katika ulinzi wa amani na haki, haki ya binadamu na utamaduni katika maisha. Alisema maneno hayo kunako tarehe 24 Mei 2002 huko Sofia na baada ya miaka 17, mfuasi wa Mtume Petro anakwenda kwa mara nyingine tena katika ardhi hii ya Bulgaria kwa ajili ya  kupyaisha amani katika dunia. Tema ya ziara ya 29 ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko kwa hakika inajifafanua vizuri: “Pacem in terris” ikiwa wazi na  kumlika juu ya  Waraka wa Mtakatifu Yohane XXIII ambaye alikuwa wa kwanza kutembelea akiwa mwakilishi wa kitume nchini Bulgaria.

Familia ya kibinadamu hadi leo inakuwa vigumu kukuza maelewano

Familia ya kibinadamu hadi leo inakuwa ngumu kukuza maelewano ni wasiwasi ambao ulikuwa tayari umeoneshwa na Mtakatifu Yohane Paulo II alipokutana na wawakilishi wa dunia ya utamaduni, wa sayansi na sanaa. Akiwa katika Jumba la utamaduni, kwa kutazama nyuma alikuwa amesema kuwa ni lazima kutambua kuwa karibu na utamaduni wa Ulaya na vyama vingi vya kifalsafa, wasanii na watu wa dini ambao wanatofautiana, karibu na Ulaya ya kazi ambayo inaelekea maendeleo ya kiteknolojia na ufundi wa karne ambayo imehitimishwa, lakini kwa bahati mbaya kuna Ulaya ya serikali za udikteta na vita, Ulaya ya damu, machozi na ukatili wa kutisha zaidi. Labda hata kwa uzoefu huu wa uchungu wa siku za nyuma, katika Ulaya ya leo, utafikiri jaribio la kuwa na wasiwasi, kutojali na  sintofahamu za kukanyaga misingi muhimu  ya maadili, na ambayo ndiyo yenye kuonekana  yeye nguvu za kimaadili katika kuishi  kibinafsi na kijamii.

Mtakatifu Yohane Paulo katika mji wa Sofia alijikita juu ya mazungumzo na waorthodox

Mtakatifu Yohane Paulo II alipendelea pia kutoa wito wa nguvu ya roho ya kiekumene ambapo alisema “ Kutoka Bulgaria ardhi ya watakatifu wa Cyril na Methodius na katika nchi yenyewe ni daraja kati ya Ulaya Mashariki na Ulaya ya Kusini, kwa maana hiyo alikuwa amewahikishia kuwa, kila dini inaalikwa kuhamasisha haki na amani kati ya watu, msamaha na maisha na upendo. Alisisitiza hayo wakati akitoa heshima kwa wafia dini wa madhehubu tofauti ya kikristo. Mtakatifu Yohane Paulo II pia  akiwa mjini Sofia aliwaalika makanisa ya kikristo kutafuta kwa pamoja njia ya umoja. Na ndiyo hilo  lengo lililokuwa la ziara yake na ili kukuza uelewa wa pamoja kati ya makanisa ambapo alisisitiza mbele ya Patriaki Maxim na wajumbe wote kwa uhakika kwamba, kwa  msaada wa Mungu na kwa  siku ambayo yeye atapenda, itawezekana kufikia kuishi kwa dhati katika umoja wa mawazo na maelewano!

Maneno ya kuwatia moyo ili waweze kuwa na upyaisho kijamii

Aidha aliweza kutoa maneno ya kutia moyo katika mchakato wa kidemokrasia uliokuwa umeanza ili kuondoka kutoka katika nchi ya kikomunisti, akiwatakia matashi mema ya kuwa na nguvu za upyaisho kijamii uliokuwa umeanza  na kwa ujasiri nchini Bulgaria, ili waweze kupokea makaribisho na msaada muhimu kutoka katika Umoja wa Ulaya. Vile vile  Mtakatifu Yohane Paulo II aliwaalika watu wa Bulgaria kuitikia wote mbele ya hali ya mazingira ya wakati ule kwa mantiki ya wasiwasi, hasa kwa kutafuta utambulisho wake wa kina. Kutokana na mtazamo huo, inaonesha wazi kwamba hili  ni  jibu la kijasiri kama kwaya ya pamoja na ambayo itapata fursa  tarehe 6 Mi 2019, wakati wa hitimisho la ziara ya Baba Mtakatifu Francisko atakapo fanya mkutano wa amani mbele ya wajumbe mbalimbali kutoka madhehebu tofauti ya dini nchini Bulgaria.

04 May 2019, 11:03