Tafuta

Kardinali Parolin Katibu wa Vatican ameandika utangulizi katika toleo la  kitabu kilicho andikwa na Agostino Giovagnoli na Elena Giunipero Kardinali Parolin Katibu wa Vatican ameandika utangulizi katika toleo la kitabu kilicho andikwa na Agostino Giovagnoli na Elena Giunipero 

Injili nchini China:Ukatoliki kati ya wakati uliopita na ujao!

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ameandika utangulizi wake katika toleo jipya la kitabu kilichoandikwa na Agostino Giovagnoli na Elena Giunipero kuhusu Makubaliano ya Mkataba wa Vatican na China.Ukatoliki wa China kati ya wakati uliopita na ujao

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika kitabu kilicho andikwa na Agostino Giovagnoli na Elena Giunipero kuhusu Makubaliano ya Mkataba wa Vatican na China.Ukatoliki wa China kati ya wakati uliopita na ujao. Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ameandika utangulizi katika kitabu hicho.Ni toleo lilotolewa na Chuo Kikuu Urbaniano. Hiki ni kitabu cha kwanza kinacho jikita katika kufafanua juu ya Mkataba wa Muda ulitiwa sahini tarehe 22 Septemba 2018, kati ya Vatican na Jamhuri ya watu wa China. Katika kitabu kimeundwa na mkusanyiko wa wanahistoria wengi, mahakimu, maandishi ya kichungaji yaliyo andikwa na wasomo wa Italia na wachina, katika mantiki ya kuona matokeo muhimu  yaliyoendelea zaidi ya miaka  miaka 40 ya mawasilianao kati ya Vatican na Jamhuri ya nchi ya China ili kutoa suluhimisho la matatizo magumu ya Kanisa Katoliki nchini China .

Katika utangulizi wa kitabu hicho Kardinali Pietro Parolin anathibitisha kuwa,kama inavyo fahamika, Mkataba wa Muda kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China iliotangazwa tarehe 22 Septemba 2018, kwa hakika ni baada ya mchakato mrefu wa mawasiliano. Mkataba huo ni tunda la hatua ndogo ndogo na ukaribu ambao umewezekana kwa njia ya mazungumzao yaliyo dumu kwa miaka mingi  na hatimaye  kufikia kuonesha hatua hiyo ndani ya historia  ndefu iliyotangulia na ambayo ni matarajio ya Kardinali Parolini kwamba kuundeleza.

Kulinganisha na utamadunisho wa China umewezesha kupata nafasi ya kwanza katika mpango wa historia ndefu ya Kanisa na China

Moja ya vitabu vilivyo andikiwa na Matteo Ricci kwa lugha ya kichina, kulikuwapo na  kile kkitwacho “De amicitia” yaani “urafiki” na baadhi ya wafuasi wake wa China ambao wamepanua kwa hakika na kwa kina ule urafiki kama vile wa Xu Guangqi, Li Zhizhao na Yang Tingyun na baadaye kuwa nguzo ya Kanisa la China. Wamekuwa kwa hakika nguvu ya kukuza utamadunisho wa imani ambapo kama wamisionari peke yao, wasingeweza kuukuza kwa mapana, kwa kina na kuaminika. Huo ni mfano mmoja tu wa mizizi ya kuanzishwa kwa ukristo, anaongeza Kardinali Parolin na ambao unaunda hata zile changamoto nyingi za Kanisa nchini China kujiuliza, sambamba na kile ambacho Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican ulikuwa inaita kama kukubaliana, na ambapo baadaye ukawa ndiyo mwongozo wa utamadunisho.

Kuelekea mahusiano mapya na Kanisa la Ulimwengu

Aidha Kardinali Parolin katika utangulizi wa kitabu hicho anaandika kuwa: japokuwa inaelewaka kwamba wameongozwa na mapenzi ya kutaka kuwa  na  huduma ya Kanisa kwa watu mahalia, lakini pamoja na hayo,  kati ya Karne ya XIX na XX, Utume katoliki ulikuwa unawekewa  vikwazo, hata matatizo yaliyoibuka kutokana na ukoloni wa Ulaya. Kardinali Parolini anathibitisha kwamba, ni Papa Benedikto XV, aliweza kutoa maamuzi na kushinda hali hiyo. Hata hivyo Kanisa Katoliki na uwepo wake dunia baadaye uliwekewa vikwazo vigumu vyenye kuwa na  vita baridi. Katika mantiki ya mivutano ya kimataifa na China Mpya, ilianza kuwa na kipindi kigumu cha Kanisa katika nchi, vilevile walipata vikwazo vya kina vilivyo sababisha hata  kuwapo kwa jumuiya za kikristo mahalia wanaojificha. Kutokana na hali ngumu hiyo nchini China, Kardinali Parolin anasema, Maaskofu wengi, makuhani, watawa na walei katoliki walitakiwa kushuhudia imani yao kwa njia ya majaribu makubwa ya mateso n amara nyingi kesi hizo ziliishia katika kutoa  zawadi binafsi ya maisha yao kwa ajili ya Kristo na kwa Kanisa.

Mkataba wa muda katika maamuzi na mazungumzo

Kardinali Pietro Parolini aliendelea na maelezo zaidi anasema: Kwa hakika mara baada ya utashi wa kuwa na mazungumzo na safari ndefu, iliwezekana kishinda vikwazo, upinzani na kukosefu wa maelewano!  Hatua hiyo imewezesha kufikia hali halisi ambayo leo hii, wakatoliki nchini China wako katika muungano kamili na Mfuasi wa Mtakatifu Petro na wamepokea kutoka kwake uwajibikaji kichungaji na kuhudumia. Katika kukabiliana na masuala ya utangazwaji wa Maaskofu, Kardinali Parolin anasema Mkataba umeweka misingi ya kutoa msukumo mpya zaidi wa kichungaji katika Kanisa la China na kazi yake ya uinjilishaji.

Mkataba huo siyo hatua ya kufikia lakini ni ya kuanzia

Kama alivyokwisha sisitiza katika fursa nyingi, Kardinali amebainisha kwamba, mkataba huo kwa hakika “siyo hatua ya kufika , badala yake ni katika  hatua ya kuanzia” katika  matazamio ya kuweza kufikia mwisho wa kushinda kila aina ya uchungu uliorithiwa wakati uliopita. Ni maratajio ya Vatican kwamba, Kanisa katoliki nchini China, linaweza sasa kuwa na uwezo wa kuishi kwa kiasi kukubwa muungano wa Kanisa la ulimwengu na ni matarajio ya kuwa na nafasi kubwa ya maendeleo ya kawaida kwa ajili ya kushuhudia imani katika nchi ya utamaduni wao. Ushiriki wa maaskofu wawili wa China katika Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana iliyoitishwa na Baba Mtakatifu Francisko mwezi Oktoba 2018,  aanasisitiza Kardinali kuwa, inawakilisha ishara ya njema! Lengo la Vatican ni lengo la kiuchungaji, kwa maana ya kusaidia Kanisa mahalia ili hatimaye wafikie kufurahia hali nzuri ya uhuru kamili wa kujitegemea na kupanga kwa namna ya kwamba, wanaweza kweli kujikita katika shughuli za kiutume na kutangaza Injili kwa kuchangia maendeleo ya binadamu na katika jamii”.

Tema ya umoja wa familia ya binadamu

Kama wakati uliopita hata leo hii matatizo na maswali yanayoulizwa kutoka China yanauliza Kanisa zima katoliki na kupelekea kuhisi kwa kina juu ya  tema ya umoja wa familia ya binadamu ambayo katika utume wa huduma ya Papa waliotanguliwa wamelezea mara nyingi kwa wakristo wa Karne ya XX na ambapo mafundisho hayo yameendelezwa au kuwa sambamba na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Ziara yake ya Falme za nchi za Kiarabu kwa tema ya udugu. Na katika kesi ya China, kwa kuwa ilikuwa ni mazungumzo  kati ya wafalme na marais na ambapo kumtengenezwa hata tendo la kisheria,  kwa mkataba wa pamoja ambao unawajibisha sehemu zote mbili mbele ya  jumuiya ya kimataifa. Karidinali Pietro Parolin anasema: suala hili, halina umuhimu wa kurudia kusema, kwa sababu mazungumzo haya ya taasisi yalifanyika na Vatican kwa ukamilifu kulingana na ukweli wa imani inayokiri Kanisa Katoliki na imani ya kuendelea katika  mafundisho ya wote waliotangulia Baba Mtakatifu Francisko.

16 April 2019, 11:04