Tafuta

Vatican News
Baraza la Kipapa la Mawasiliano imetengeneza Nembo ya siku za kimataifa za uhariri katoliki,kuanzia tarehe 26-29 Juni mjini Roma  Baraza la Kipapa la Mawasiliano imetengeneza Nembo ya siku za kimataifa za uhariri katoliki,kuanzia tarehe 26-29 Juni mjini Roma  

Siku za Kimataifa za uhariri katoliki:Unaweza kujiandikisha!

Siku za Kimataifa za uhariri katoliki zilizo andaliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano,kuanzia tarehe 26-29 Juni mjini Roma. Unaweza kujiandikisha tayari kutumia:gec@spc.va Siku hizi zimeandaliwa kwa ajili ya mijadala,hotuba na ushuhuda kutoka kwa wahariri katoliki wa pande zote za dunia.

Siku za Kimataifa za uhariri Katoliki zimeandaliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kuanzia tarehe 26 -29 Juni 2019. Lengo la siku hizi nne ni kuungana pamoja katika mkutano wa kujadiliana na wahariri katoliki, wadogo na wakubwa ambao wanajikita katika kupeleka utume wao duniani ili kueneza ujumbe wakikristo.

Mtazamo wa siku hizo ni mijadala,hotuba na ushuhuda kutoka kwa wahariri katoliki

Mijadala hiyo itafunguliwa na Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Bwana Paulo Ruffini na kuongozwa na hotuba mbalimbali ili kutafakari juu ya changamoto na matatizo ya  dunia ya uhariri katoliki wanayo kumbana nayo leo hii, katika mantiki ya utandawazi na digitali. Hata hivyo,tafakari hii itaajirishwa na ushuhuda kuhusu uzoefu wa wahariri katoliki kutoka katika mabara tofauti, hotuba mbalimbali na kati ya wengine, ni wataalam katika kuthamanisha bidhaa zao kwa mfano, kutakuwapo na mwasilishaji wa “maktaba” ya online.

Watashiriki pia misa Takatifu itakayo adhimisha na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sikukuu ya Watakatifu Petro na Paulo tarehe 29 Juni

Wahariri wengi  hao pamoja na  na meza za mduara katika kushirikishana uzoefu wa kila mantiki ya utamaduni  katika mchakato wa siku hizo, pia utakuwa na tabia ya kiutamaduni  na ushiriki wa Misa Takatifu, itakayo ongozwa na Baba Mtakatifu Francisko katika fursa ya Sikukuu ya watakatifu Petro na Paulo wasimamizi wa Kanisa la Roma tarehe 29 Juni. Kwa maelezo zaidi na kujiandikisha  tumia anuani hii: gec@spc.va

09 April 2019, 10:00