Tafuta

Vatican News
Tarehe 25 Aprili 2019, Baba Mtakatifu amekutana na Rais wa nchi ya Lithuania Bwana Raimonds Vejonis na wawakilishi wengine Tarehe 25 Aprili 2019, Baba Mtakatifu amekutana na Rais wa nchi ya Lithuania Bwana Raimonds Vejonis na wawakilishi wengine  (Vatican Media)

Papa akutana na Rais Raimonds Vējonis wa Lithuania

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Lithuania Bwana Raimonds Vējonis,tarehe 25 Aprili 2019 na baadaye kukutana na Monsinyo Antoine Camilleri,Katibu Msaidizi wa Vatican wa Mambo ya Nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa

Na Sr. Angela Rwezaula Vatican

Tarehe 25 Aprili 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Nchi ya Lithuania Bwana Raimonds Vējonis na baadaye amekutana na Monsinyo Antoine Camilleri, Katibu Msaidizi wa Vatican wa Mambo ya Nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Hata hivyo kati ya mada nyingi zilizogusiwa na Baba Mtakatifu ni pamoja na hali halisi ya kijamii na kidini katika nchi , vile vile haya Amani na usalama wa Kanda.

Mahusiano mazuri yaliyopo katika nchi mbili

Na katika mazungumzo na Katibu msaidizi wamegusia juu ya mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizo mbili na kukumbuka hata ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko kunako  2018 katika fursa ya maadhimisho ya miaka mia 100 ya uhuru wa nchi ya Lithuania.

Mada ya kijamii, kidini na kimataifa

Katika mchakato wao wa mazungumzo, viongozi hawa wawili, baadaye amegusia mada msingi inayohusu hali halisi ya kijamii na kidini katika nchi. Lakini pia wameendelea kutazama tema nyingine za kimataifa, hasa juu ya amani na usalama wa Kanda na wakihitimisha kwa kutakiana matashi mema ya mipango ya wakati endelevu ya  Ulaya na katika kulinda mazingira.

25 April 2019, 13:40