Tafuta

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Rais Faure Essozimna Gnassingbe wa Togo: Amani, Utulivu na Usalama Barani Afrika mambo msingi katika mazungumzo yao! Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Rais Faure Essozimna Gnassingbe wa Togo: Amani, Utulivu na Usalama Barani Afrika mambo msingi katika mazungumzo yao! 

Papa Francisko & Rais wa Togo: Amani na utulivu Barani Afrika

Baba Mtakatifu na Rais wa Togo katika mazungumzo yao, wamegusia uhusiano mwema uliopo kati ya nchi hizi mbili na kwamba, kuna haja ya kuimarisha uhusiano huu kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wa Togo. Wamegusia pia hali halisi ilivyo nchini Togo, mchango wa Kanisa katika mchakato wa maendeleo fungamani hasa katika sekta ya elimu na afya.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 29 Aprili 2019 amekutana na kuzungumza na Rais Faure Essozimna Gnassingbé wa Togo pamoja na ujumbe wake. Baadaye Rais Gnassingbé amebahatika kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, aliyekuwa ameandamana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Baba Mtakatifu na mgeni wake, katika mazungumzo yao, wamegusia uhusiano mwema uliopo kati ya nchi hizi mbili na kwamba, kuna haja ya kuimarisha uhusiano huu kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wa Togo.

Wamegusia pia hali halisi ilivyo nchini Togo pamoja na kuangalia mchango wa Kanisa katika mchakato wa maendeleo fungamani ya familia ya Mungu nchini Togo mintarafu huduma katika sekta ya elimu na afya. Mwishoni mwa mazungumzo yao, Baba Mtakatifu Francisko na Rais Faure Essozimna Gnassingbé wa Togo, wamegusia pia changamoto zinazoendelea kujitokeza Barani Afrika na kwamba, kuna umuhimu wa kuunganisha nguvu kikanda na kimataifa, ili kukuza na kudumisha: ulinzi na usalama, amani na utulivu Barani Afrika.

Papa: Togo
29 April 2019, 15:46