Tafuta

Vatican News
Ni muhimu kuwaimarisha wanawake vijijini Ni muhimu kuwaimarisha wanawake vijijini   ([Photographer name] for CRS)

Vatican:Wanawake vijijini wamesahuliwa kwa sheria na sera za siasa!

Monsinyo Fernando Chica Arellano,mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Shirika la Fao,Ifad na Pam wakati wa hotuba yake katika Mkutano amesisitizia juu ya hali halisi ya maisha ya wanawake ambao ni wakalima katika mashamba vijijini.Kuna haja ya kutambuliwa haki za wanawake vijijini ambazo mara nyingi zinakiukwa na mahitaji yao hayafikiriwi

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Hotuba ya Monsinyo Fernando Chica Arellano mwakilishi wa kudumu wa Vatican  katika ofisi za Fao, Ifad na Pam katika mkutano uliongozwa na mada Madaraja na siyo kuta.Wanawake kati ya maisha na kazi. Ni mkutano ulioandaliwa na Mameya wa  Fai-Cisl, tarehe 13 machi 2019 katika makao ya  Cnel,  Roma.Katika hotuba yake aliipatia jina wanawake na kilimo walinzi wa amani anasema ameandaa kwa  kutazama ujumbe wa Mtakatifu Yohane Paulo VI juu ya wanawake aliouandika wakati wa fursa ya kufunga Mtaguso II wa Vatican. Ujumbe huo ulikuwa unasema kuwa:Wanawake duniani kote, wakristo au waamini ambao wamekabidhiwa maisha muda muu wa kipindi kigumu cha historia ni wao sasa wa kuweza kuokoa amani duniani! Askofu Arellano anasema ni mshangao upi wa thamani ya kinabii katika maneno hayo, makubwa ambayo bado yanahitajika katika nyakati hizi na kutoa  zoezi kuu zaidi zuri na nguvu kwa wanawake! Ni wanawake kwa hakika wenye uwezo wa pendo mkuu ambao hata Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza na wenye uwezo kubomoa hata kuta kwa ajili ya kujenga amani.

Akiendelea na hotuba yake Monsinyo Arellano anasema, moja ya mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 1 Januari 2019 ikiwa pia ni Siku ya Amani duniani, Baba Mtakatifu alisema: “dunia ambayo inatazama wakati ujao bila mtazamo wa umama ni kipofu. Itaongeza hata faida, lakini haitatambua watu na watoto. Kutakuwapo na mapato, lakini hayatakuwa kwa ajili ya wote. Tutaishi katika nyumba moja lakini siyo kama ndugu. Msingi wa familia ya binadamu ni wamama”. Akitazama sehemu ya ujumbe huo, pia juu ya mada yake anasema tutazame kwa namna ya pekee wamama ambao wanaishi katika maeneo ya vijiji katika mashamba ya kilimo. Hawa wanashika nafasi moja msingi ya uchumi kwa upande wa miji hasa katika nchi zinazoendelea japokuwa wao wanabaki masikini. Ni muhimu hasa kutazama namna ya kuwasaidia ubora wao hasa kwa upende wa nyeza za maendeleo ili kuongeza nguvu ya jumuiya kwani wanaweza hata wao kunufaika na kuwa na uhakika wa vyakula, lisha na kupambana dhidi ya umasikini.

Hawa siyo tu wenye kuleta faida peke yake  lakini pia wako  mstari wa mbele wa maendeleo ya familia zao na katika jamii. Haki ya kimataifa inatambua umuhimu wa wanawake vijijini. Katika ibara ya 14 ya Katiba juu ya kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawakena ambayo ni moja ya mkataba wa kulinda haki za binadamu, inajikita kutazama kwa dhati wanawake vijijini , hivyo kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria. Ibara hiyo ina maana ya kutaka kuwasaidia wanawake wote vijiji wawe na nafa si ya kutazamwa katika uchumi na familia kuondoa kila iana ya ubagusi kwa kuwa na usawa kati ya wanaume na wawake kwa ushiriki wao wa kuleta maednelea ya vijana na faida zao.

Wanawake zaidi wanao fanya kazi katika mashamba ya vijiji ndiyo wanatunza familia, lakini wanahisi kulipwa kidogo na japokuwa wengine wanalipwa kima cha chini na wanabaki wakiwa hawana ulinzi kijamii. Hata hivyo licha ya kuchangia asilimia 34 ya nguvu ya kazi, kwa upande wao hawafikii hata asilimia 20 ya ardhi yao binafsi. Kuna masuala magumu sana juu ya ardhi na ambap wanawake wako hatari ya kubaguliwa katika mpango wa kugawa maeneo ya kuweza kulima. Aidha ipo hatari ya wanawake kijini kuwa waathirika wa biashara haramu binafsi, ukosefu wa elimu, ukosefu wa kwenda vituo vya afya na mara nyingi wamebaguliwa kwa sababu ya umasikini, ukosefu wa ajira na ukosefu wa majengo. Suala hili Baba Mtakatifu Francisko anasema hao wanakuwa ni wathirika wa kile kiitwacho kubaguliwa na ndiyo mantiki za sasa zinazoikumba sehemu kubwa ya vijiji anathibitisha mwakilishi wa kudumumu.

Kwa maana nyingine, kuruhusiwa kwa wanawake  katika ardhi inakuwa ni msingi mkuu wa kuweza kutumia hata haki nyingine msingi za kibinadamu kama ilivyo ya maisha, afya , vyakula, kazi , elimu , utambulishiowa utamaduni, ushiriki wa maisha ya kijamii na kisiasa. Na ndiyo maana haki ya mwanamke katika ardhi na rasilimali asili zinaweza kweli kuendelezwa kama kweli haki msingi wa maisha ya binadamu. Na ili kuongeza nguvu vijijini kwa ajili ya wanawake anasidi kusisitiza juu ya usawa kati ya mwanamme na mwanamke na haki hizi ziwe msingi, zisimike mizizi yake katika hadhi na isikiukwe kamwe. Ni lazima kukabiliana na kupambana na dhana dume ambayo mara nyingi Baba Mtakatifu Francisko amezungumzia na ambayo inapelekea nguvu dhidi ya wanawake na  na kutimika kama chombo cha kutumia, kama bidhaa na kama faida. Ni lazima kuwa makini ili haki msingi za mwanaume na mwanamke kwa namna moja au nyingine zinatambuliwe japokuwa na utofauti kati yao. Utofauti huo unaoneshe ule umoja  na ulazima wa kukamilishana kati yao.

14 March 2019, 14:08