Tafuta

Vatican News
Tarehe 13 Machi 2013 Baba Mtakatifu Francisko alichaguliwa kuwa katika kiti cha Mtume Petro.Tarehe 13 Machi 2019 ni mwaka wa sita akiwa anaongoza mtumbwi wa Kanisa! Tarehe 13 Machi 2013 Baba Mtakatifu Francisko alichaguliwa kuwa katika kiti cha Mtume Petro.Tarehe 13 Machi 2019 ni mwaka wa sita akiwa anaongoza mtumbwi wa Kanisa! 

Miaka 6 ya Uongozi wa Papa Francisko

Ikiwa ni mwaka wa 6 tangu kuchaguliwa kwa Baba Mtakatifu Francisko kuwa khalifa wa Mtume Petro, tasaufi ya utume wake inaanzia katika kiini cha mafundisho ya Kristo,imani katika nguvu ya sala, utakatifu wa kila siku katika ishara halisi na kumtazama Mama Maria kama msimamizi na mwombezi wa Kanisa!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Asubuhi katika nyumba ya mafungo huko Ariccia, nje ya mji wa Roma kwa Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu, kabla ya misa  Kardinali Giovanni Battista Re, Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu ametoa maneno mafupi kwa niaba ya wote kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye tarehe 13 Machi 2019 ni mwaka wa sita tangu kuchaguliwa kuwa Papa. Kardinali Re anakumbusha kwa jinsi gani ni mwaka wa sita tangu yeye awe Papa wa Kanisa Katoliki na kwa niaba ya sauti ya wote wanaofunga mafungo ya kiroho anaonesha furaha ya kuadhimisha naye misa Takatifu ikiwa inaongozwa naye. Amemkubusha jinsi gani wanamwombea kwa Mungu ili apate mwanga, amlinde na kumpatia nguvu katika zoezi la kuimarisha ndugu katika imani kwa msingi wa umoja na kuwalekeza wote njia ya kwenda mbinguni. Mungu Baba Mtakatifu awabariki na kumwakikishia sala za upendo huo katika maadhimisho ya ibada.

Kwa miaka sita ya Baba Mtakatifu Francisko tangu achaguliwe kuwa kiongozi mkuu wa Kanisa mantiki zake ni msingi kwa ukuu wa ngazi zote kijamii na kikanisa na hasa katika kijamii ambapo mafundisho yake yameweza kupanuliwa zaidi kwa njia za vyombo vya habari, kuanzia katika masuala msingi wa Kristo na imani kubwa ya kina cha sala na udhati wa kila siku katika ukuu wa Mama Bikira Maria ambaye ameonesha ibada kuu kwake na mifano hai zaidi iliyojionesha kwa miaka hii sita ya huduma yake kwa Kanisa.

Ilikuwa ni tarehe 13 Machi 2013 alipochanguliwa Baba Mtakatifu Francisko, kutoka katika bara la Amerika ya Kusini, nchini Argetina. Ni mjesuiti wa kwanza kuchagua jina  la masikini wa Asisi. Mbali na matukio na mantendo yake yanayojulikana kwa siku 2,191 za Baba Mtakatifu Francisko akiwa ni mfuasi wa 265 wa Mtume Petro, bado kuna mambo  kama 10 hivi ambayo yanaweza konesha tasaufi yake kuu na ambayo mara nyingi inakuwa vigumu katika vyombo vya habari kuonesha uwazi wake na ukuu wake. Mambo hayo ni kama yafuatayo 1. Kuishi na imani ni kukutana na Yesu. Hicho ndicho  kiini cha  cha kwanza cha utume wa Baba Mtakatifu kwa kujikita katika fumbo la  kukutana na Bwana Mungu kweli na mtu kweli ambayo ndiyo tangazo la kwanza au Kerygma. Yesu anatupenda, ametoa maisha yakwe kwa ajili yetu (Evangelii gaudium, 164). Imani siyo mawazo ya itikadi, kwa maana mawazo ya itikadi yanagawanya kuamsha kuta, lakini mkutano na Mwokozi anatusukuma kwenda kukutana na wengine na kutubadili maisha anathibitisha Baba Mtatifu Francisko katika Evangelii gaudium.

Kwa kuanzia na tasaufi hiyo ya kwanza ya Kristo  ndipo zinafauata nyingine: 2.kusali kwa maana Mungu ni Baba na sisi ni ndugu;3.Tuache tubadilishwa na Roho Mtakatifu; 4. Kanisa daima ni nyumba iliyofunguliwa ya Baba; 5. Inahitaji mwendelezo wa upyaisho wa kiroho; 6. Imani ya kweli inatuweka katika kipeo; 7. Upendo uwe juu zaidi ya mambo mengine yote; 8. Utakatifu ni huruma ya kila siku; 9. Mkristo yupo duniani, lakini si katika dunia na hatimaye, 10. Msaaada wa Mama Maria na mapambano dhidi ya Ibilisi ambaye Baba Mtakatifu Francisko ameonesha wazi juu ya uwepo wa Ibilisi , ambapo anathibitisha na kuonya kuwa makini ya kutompatia nafasi ya kuzungumza naye, badala yake kumjibu kwa kutumia Neno la Mungu! Haya ni mambo makuu na mengine  zaidi, lakini kwa kupitia tasaufi hizi Baba Mtakatifu Francisko kwa miaka  hii sita ameweka bayana kwenye mafundisho yake kwa waamini na lugha rahisi, kwa mataifa na wenye mapenzi mema!

Baadhi mambo mengine muhimu  katika kipindi cha utume wake kwa miaka hii sita: Katika kipindi cha miaka 6 tangu Baba Mtakatifu Francisko achaguliwe zaidi ya mahubiri 1000 yametolewa na zaidi ya misa 670 zimeadhimisha katika Kanisa la Mtakatifu Marta, ni mfano hai katika mahubiri yake  yasiyo tayarishwa bali ya moja kwa moja kutoka ndani ya moyo.  Zaidi ya hotuba 1200 ameweza kuhutubia kwa watu; katekesi  264 za kila Jumatano na  ambazo imekuwa tunu msingi wa kitasaufi kwa kujikita katika mada zifuatazo:Sala ya Nasadiki, Sakrameti, zawadi za Roho Mtakatifu, Kanisa, Familia, Huruma, Matumaini ya Kikristo, Misa Takatifu, Ubatizo, Kipaimara, Amri za Mungu na hatimaye Sala ya Baba Yetu. Na zaidi kuna tafakari 342 kuhusu Injili  za  Dominka  na Sikukuu, wakati wa fursa ya Sala ya Malaika wa Bwana na Malkia wa Mbingu; kadhalika Baba Mtakatifu ameandika Hati mbili (Lumen fidei, iliyo anzishwa na Papa Benedikto XVI na kumalizia yeye na  Laudato si’); Wosia tatu za Kitume (Evangelii gaudium ambao ni mpango mzima wa Kipapa katika huduma yake kama mkuu wa Kanisa  ni muhimu mapana yake), Amoris laetitia na Gaudete et exsultate); Katiba 36 za Kitume kati ya hizo ni (Episcopalis communio, Veritatis gaudium na Vultum Dei quaerere); Motu Proprio  27;Tamko kuhusu maelekezo ya Jubileo ya Huruma  (Misericordiae Vultus).

Baba Mtakatifu kwa kipindi cha miaka 6 ameweza kuhitisha Sinodi tatu, mbili juu ya familia na moja kuhusu vijana: ameweza kufanya ziara za kitume  za kimataifa 27, katika nchi 41 kwenye mabara yote kasoro moja la Australia, pia ziara 24 nchini  Italia. Kati ya kuwatangaza watakatifu tunawakumbuka mapapa watatu: Papa Yohane wa XXIII, Papa Paulo VI  na Papa Yohane Paolo II, baadaye Mama Teresa di Calcutta, Askofu  Romero, na  wachungaji wawili wa  Fatima yaani  Yacintha na Francisko Marto, wazazi wa Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu  (Martin na Zelia), Mtakatifu Angela wa  Foligno na  Elisabeth  wa Utatu, hatimaye  hata kuingia katika mitandao ya kijamii kama vile Twitter kwa  kwa lugha 9 (@pontifex), ikiwa na wafuasi (Follower) milioni 48 na Instagram (Franciscus) ambayo ina wafuasi karibia milioni 6.

13 March 2019, 13:47