Tafuta

Vatican News
Tarehe 13 Machi 2013 alichaguliwa Papa Francisko Tarehe 13 Machi 2013 alichaguliwa Papa Francisko  

Miaka 6 tangu Papa Francisko kuchaguliwa!

Baba Mtakatifu Francisko ameishi miezi hii kwa kina kati ya ziara na Sinodi. Ni katika mwaka wake wa sita unapokaribia tarehe 13 Machi ni kuona kwa jinsi gani ameweza kukabiliana na janga la manyanyaso na mateso katika baadhi ya mashambulizi ya ndani.Lakini jibu lake limekuwa ni kutoa mwaliko wa kurudi katika moyo wa imani

Na Angela Rwezaula . Vatican

Mwaka wa sita tangu kuchaguliwa kwa Baba Mtakatifu Francisko mwaka ambao unamkuta katika jitihada za kina na muhimu kwa ziara za kimataifa, kuanzia mwanzo wa mwaka hadi  mwisho wa mwaka kwani kuna matukio mawili ya sinodi. Kwanza Mkutano wa Maaskofu kwa ajili ya ulinzi wa watoto ulifanyika mwezi Februari mwaka huu kwa ushiriki wa Marais wa mabaraza ya Maaskofu duniani na Sinodi Maalum ya Amazoni itakayo fanyika mjini Vatican mwezi Oktoba mwaka huu.

Ndiyo mwanzo wa ufafanuzi wa shughuli za kipapa wa Dk. Andrea Tornielli Mkurugenzi wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican wakati tunakaribia katika kilele cha  siku ya kumbukumbu ya kuchaguliwa kwa Baba Mtakatifu Francisko tarehe 13 Machi 2013. Dk Tornielli anaonesha matukio ya  shughuli za Baba Mtakatifu kwa mwaka huu ukiwa ni wa  sita ambapo anathibitisha kwamba mada ya kiekumene itakuwa ina kipaumbele katika ziara za Kitume za Baba Matakatifu Francisko nchini Burgaria, hivyo hata nchini Romania, lakini wakati huo huo hata kuna utashi wa ziara ya Japan japokuwa bado haijatangazwa rasmi. Hii ni kutaka kuimarisha nchi hizi zenye mipasuko na marumbano ya uchochezi wa vita vya kinyukilia na ili watu hao waweza kusitisha malumbani hauo kwa sababu ya kutafuta amani ya sasa na endelevu ya kibinadamu ambapo katika dunia kuna tayari  uzoefu wa vita ya tatu ya dunia ambayo imegawanyika vipenda vipande kama apendavyo kuelezea Baba Mtakatifu Francisko

Hata hivyo mwaka uliopita pia imeonesha ni kwa jinsi gani umejikita katika suala gumu hasa la manyanyaso na migawanyiko ya ndani ambayo imeonekana hata mwezi agosti mwaka 2018, kushutumia na Carlo Maria Vigano, wakati Baba Mtakatifu akiadhimisha Misa Takatifu kwa maelfu na maelfu ya familia walio kusanyika mjini Dublin Ireland, wakionesha kwa dhati uzuri na thamani ya ndoa ya kikristo ambao alitangaza adharani kuwa Baba Mtakatifu ajiudhuru kufutia na kesi ya McCarrick. Mbele ya hali hizi Askofu Mkuu wa Roma, yaani Baba Mtakatifu Francisko aliomba waamini wote duniani kusali Rosari kila siku kwa mwezi mzima wa Bikira Maria Oktoba 2018 kwa kujumuisha kumunio na toba kama watu wa Mungu wakimwomba Bikira Maria Mama wa Mungu na Mtakatifu Malaika Mkuu alinde Kanisa dhidi ya Ibilisi ambaye daima anataka kutengenisha na Mungu na kati yetu. Vile vile  wito wake kwa watu wa Mungu ulikuwa ni kusali ili kuweza kutunza umoja wa Kanisa na ambapo Baba Mtakatifu alitambua kweli hali halisi mbaya inayoikumba  Kanisa, na utambuzi kwamba kwa uwezo wa binadamu hauwezekani bali ni kwa njia ya sala.

Kwa mara nyingine tena Baba Mtakatifu alitoa wito kwa mambo msingi kwamba kanisa halijatengezwa na mashujaa wala mapapa washujaa, aidha haliwezi kwenda mbele kwa njia ya nguvu za rasilimali zake za kibinadamu au mikakati yake. Anatambua kuwa ibilisi yupo katika dunia na ambaye amekuwapo tangu kuumbwa kwa dunia na ili kuweza kuokoa kuna haja ya kupata msaada kutoka kwa aliye juu.Kurudia huko hakuna maana ya kupunguza uwajibikaji binafsi na hata ule wa taasisi lakini n kuurudishia mantiki ya hali halisi. Katika maombi ya Baba Mtakatifu Francisko ya kuomba kusali Rosari mwezi Oktoba mwaka jana, alikuwa anawaomba waamini wa dunia nzima kusali kwa Mtakatifu Mama wa Mungu aweke Kanisa chini ulinzi wa Joho lake, ili kuweza kudhibiti mashambulizi ya ibilisi na mshitaki mkuu na wakati huo huo kuwa na utambuzi juu ya manyanyaso na makosa yaliyo sabishwa nyakati zilizopita. Wakati uliopo na uliopita, unaweza kuwa na makosa lakini siyo kumbebesha aliye kuja baadaye kabla yetu makosa na kujiwakilisha kama waliotakasika.  Hata leo hii Kanisa lazima kuomba mwwanga  zaidi ili kuweza kuondokana na mabaya .Ndiyo hali halisi ambayo Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuwaomba waamini na waafua wote na kutoa mwito wake wa kila siku.

 

12 March 2019, 12:10