Cerca

Vatican News
Baba Mtakatifu amesali mbele ya Mama Maria afya ya waroma na kumkabidhi ziara yake ya kitume nchini Morocco Baba Mtakatifu amesali mbele ya Mama Maria afya ya waroma na kumkabidhi ziara yake ya kitume nchini Morocco 

Papa amesali mbele ya Picha ya Maria Mkuu kabla ya ziara yake nchini Morocco

Papa Francisko asubuhi ya tarehe 29 Machi 2019 amekwenda katika kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu afya ya waroma kusali kwa ajili ya kukabidhi ziara yake ya siku mbili, Jumamosi na Jumapili nchini Morocco

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kama kawaida yake Baba Mtakatifu Francisko kabla ya kuanza ziara 28 ya Kitume chini Morocco kuanzia tarehe 30-31 Machi 2019, ikiwa ni kawaida yake, Ijumaa asubuhi 29 Machi 2019 amekwenda katika Kanisa Kuu la Mama Maria Afya ya waroma, kusali na kumkabidhi ziara yake hiyo. Msemaji mkuu wa mpito wa vyombo vya habari Bwana Alessandro Gisotti ametoa taarifa hiyo kupitia Tweet yake ya kuwa, Baba Mtakatifu amekwenda na kukaa mbele ya picha ya Mama Maria kwa ukimya wa sala ili kumkabidhi hija yake ya kitume nchini Morocco.

29 March 2019, 14:30