Tafuta

Mafungo ya kiroho kwa Baba Mtakatifu na waandizi wake yakiongozwa na Abate Maria Gianni  Mafungo ya kiroho kwa Baba Mtakatifu na waandizi wake yakiongozwa na Abate Maria Gianni  

Mafungo ya kiroho:Mji na ustaarabu viwe makazi ya Mungu

Katika tafakari ya mwisho wa Mafungo ya kiroho kwa Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake huko Ariccia nje ya mji wa Roma,tarehe 15 machi 2019 Abate Gianni Maria amekijita na mada kuhusu mji uliowekwa juu ya mlima,kwa kutazama tena sura zilizo mwongoza katika tafakari hizi yaani Luzi na Giorgio La Pira

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Nimejipa ruhusa ya kuwaalika wote kutembelea mlima wa mashariki ya Firenza, uliobarikiwa kwa karne na karne kufuatia na ibada ya mfiadani  wa Armenia Miniato: Hiyo ni kwa sababu juu yake kuna uwezo wa kutazama kwa hakika neema, kwa shukrani, kwa fumbo juu ya mji wa Firenze. Alikuwa amenza na mwaliko huo wakati wa utangulizi wake wakati wa kuanza mafungo, Jumapili Jioni tarehe 10 Machi 2019, ambapo kwa wiki nzima, Abate Bernardo Francisko Maria Gianni Mmonaki wa kibenedikitini kutoka Firenza ameweza kuwangoza kwa tafakari juu ya  mji wa Firenze, kwa maana ya mfano wa mji wa dunia, famili ya kibinadamu ambayo ndiyo kwa hakika inaowakilisha kati ya tamaa kuu za Mungu na changamoto za wakati wetu.

Mwisho wa ubinadamu ni muungano na Mungu

Katika kutafakari asubuhi  tarehe 15 Machi 2019 na ambayo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho, Abate Maria Gianni anatazama sura ya mji  ulio juu ya mlima kwa kupitia maneno ya Ufunuo sura ya  21 ambayo ni maonesho ya mwisho a historia ya binadamu, na Yerusalem mpya makao ya Mungu na watu, mahali ambapo hapatakuwapo na machozi au  kuomboleza na kulia , wala kazi kwa maana mambo ya kale yamekwisha na tazama sasa yapo mapya. Wazo hili ni kutaka pia kutoa ahadi hii ya uhakika wa Muungno na Mungu kwa matumaini ambayo Mungu anamtunzia binadamu wote. Katika hili lakini Abate anathibitsha kwamba  lakini yeye ndiye aliye  mstari wa mbele kusindikiza hata kuwapa jitihada kama Kanisa na jumuiya ili kugeuka kuwa mji wa familia na Injili kama chachu ndani yake!

Ni muhimu sana kufikiria kama Baba Mtakatifu Francisko anavyoeleza kuwa Maonesho yanatulekeza kwamba  ukamilifu wa binadamu  wa historia unakamilishwa katika mji  na muunganiko katika bustani na kwamba ni ukamilisho ambao umejaa ni mji ,maisha ambayo  ambayo ni wito wa kweli na fumbo la kweli la mji,lakini unapaswa  kwa mara nyingine tena  kuonekana hata katika maneno mazuri ya Giorgio la Pira ambapo nia yake iliuwa ni kuona maneno yote yanakuwa kama muungano na uhusiania ambao unageuka  kuwa mji wa familia. Hayo ndiyo matarajio na zoezi lonalobaki kwa watu watakatifu wa Mungu, wachungaji na wote ambao wanahisi uzuri mwaminifu, wa kusifu, au kuwa na mtazamo wa Ufunuo wa leo unajionesha katika nyakati zijazo. Na ndiyo kipimo chake ni neno hai la Mungu ndiyo Maandishi matakatifu.

Sisi ambao hatusitahili tumepewa mema na fumbo ambalo tumepokea

Sisi ambao hatusitahili tumepewa mema na fumbo ambalo tumepokea kwa utambuzi inawezekana kweli tuambukize kwa matumaini wale ambao kwa namna moja au nyingine hawana bahati hiyo. Katika neno la matumaini, kwa dhati amependa kusisitizia juu ya maneno ambayo Baba Mtakatifu Francisko anawapatia kila wakati. Ni kweli kwamba katika miji yetu inateseka na kutoa hisia ya kwamba hakuna mizizi hasa kwa matatizo mengi ambayo yanaikumba dunia kwenye miji mikuu ya sasa, na jamii nyingi zinazopinga  maendeleo na nguvu, ukiongezea hata hofu kama iliyotokea hata New Zealand. Lakini licha ya hayo, Baba Mtakatifu Francisko anasema upendo una nguvu zaidi. Watu wengi katika hali hii wanao uwezo wa kuishi na kubadili , mahusiano ya kuweza kuishi kijumuiya ambayo japokuwa na kukumbwa na janga la ubinafsi na uwezo wa kushinda vizingiti vya ubinafsi huo.

Kanisa haliweza kutofikiria kuwa chachu

Kanisa haliweza kutofikiria kuwa chachu, ushuhuda wa kweli na aaminifu katika mchakato mzima wa upendo ambao unajitokeza katika miji na ambao tunatazama kwa macho yetu kwa kutafakari kama isemavyo Evangelii gaudium, kama ilivyo kuwa kwa  Riccardo wa Mtakatifu  Vittore, Giorgio La Pira,  Mario Luzi,  ambao wamefundisha mengi katika siku hizi za mafungo. Upendo, huruma na umoja ni zawadi ambazo Bwana amekadhi kwa Kanisa ili kuwa njia za kuweza kuwafikia wanawake na wanaume wenye mapenzi mema leo hii. Ni wito kwa wote ni kufanya kwa namna ya kwamba miji na ustaarabu wao wa kumpokea Mungu kwa kipimo ambacho kwanza Kanisa linapokea anathibitisha Abate Gianni na kuongeza, ndiyo Kanisa lifanya pia jumuiya ya kikristo, lazima ihisi kwa dhati,  kwa kina mshikamano na binadamu wote na historia yake, migogoro yake, mahangaiko yake na mateso yake.

Injili ndiyo iwe mji

Injili ndiyo iwe moja ya chachi ya kikua wimbi kama inavyosomeka katika Evangelii Gaudium 237- na iwe mji. Hii ni changamoto ndumu na ambayo ametaka kuwaachia moyoni mwao kwa kumwalika Baba Mtakatifu Francisko na Sekretarieti nzima watembelee Monasteri ya Mtakatifu Miniato lakini zaidi ni kuwatakia safari njema ya kurudi mjini Roma kwa kuongozwa na shauku ya:"Lucrare animas”, anasema Mtakatifu Benedikto katika Kanuni kwa mwalimu na manovisi ambao kama yeye na kama Mtakatifu Yohane Chrisostom alikuwa anasema kwamba  ni lazima kuwa na watu wengi ili wasiweze kupotea hata neema kutokana na sintofahamu zetu.   Lazima kuwa muhudumu na kubaki katika uhudama ya kugeuka katika moyo wa mji na ishara angavu ya umoja ambao Bwana kwa hakika hatakosa kutoa.

15 March 2019, 13:32