Tafuta

Vatican News
Mafungo ya Kiroho huko Ariccia kwa ajili ya Baba Mtakatifu na waandamizi wake wa karibu Mafungo ya Kiroho huko Ariccia kwa ajili ya Baba Mtakatifu na waandamizi wake wa karibu  (Vatican Media)

Mafungo ya kiroho:Mungu anataka tuwe wenye uwezo wa kuota ndoto kama yeye!

Katika mwendelezo wa tafakari ya mafungo ya kiroho huko Ariccia nje ya mji wa Roma kwa Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu,,Abate Maria Gianni tafakari yake ya jioni Jumatatu 11 Machi iliongozwa na mada ya “tuko hapa kuimarisha pumzi kwa cheche zetu”.Mungu anatutaka tuwe wenye uwezo wa kuota ndoto kama yeye

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kufafanua shahiri linalotazama ndoto, Abate Bernardo Francesco Maria Gianni amependekeza kwa namna ya pekee wote wanaofanya mafungo ya kiroho watazame na kusikia mwaliko wa upepo mwanana katika cheche za matumaini na imani. Abate Maria Gianni anawakumbusha katika tafakari hii kuwa moto wa upendo wa Yesu umekabidhiwa kwao hata katika ushuhuda, kuulinda na  ni shauku ya kila mmoja. Katika kipindi cha Kwaresima, kinawezesha kupyaishwa moto ambao umezimika  kutokana na mazoe ya ukawaida na ubaridi ambao kwa hakika unakemewa  katika kurasa za kitabu cha Ufunuo anathibitisha

Aidha anasema ni kweli kwamba Barua ya Mtakatifu Paulo kwa (Waroma 11, 20) inakumbusha kuwa, zawadi na wito wa Mungu ni mambo yasiyo tenguka kamwe.  Swali anauliza je ni kwa jinsi gani tunaweza kufikiria kutafuta kwa shauku kubwa makaa yanayowaka na ambayo ni  ya lazima ili kuweza kuendelea kuwaka na kukuza cheche za wito wetu tulio upokea?

Majivuno ya kudai  kuwa hatuna haja ya kitu chochote: Aidha Abate Bernardo Francesco Maria Gianni anaweka anagalisho juu ya majivuno ya kujidai kuwa hatuna haja ya kitu chochotehivyo anasema je tunazingatia kweli kuwa  tunaweza kutunza moyo na kulinda zawadi kubwa ambayo Bwana ametupatia katika maisha ya sala, kusikiliza Neno lake, kumwilishwa kwa Ekaristi takatifu na kuishi kwa kina udugu ambao unatokana na kusikiliza Neno na kuendelea kuthibitisha juu ya  mantiki ya Ekaristi ambayo ndiyo  ya ndoto maisha ya Mungu na njia ya maisha yetu binafsi?.   Je ni kweli tunatengeneza njia kwa nguvu ya fumbo la nguvu ya Roho Mtakatifu? Anajibu akisema kuwa pumzi ni nguvu ya Roho Mtakatifu ambayo inastahili kupitia kwetu na ambayo inastahili kubadilisha nguvu zetu dhaifu, udogo wetu na kutufanya tuwe na uwezo wa kuamka tena na kupyaisha cheche hai za shauku katika Kristo!

Maelewano ya nyakati: Akiendelea na tafakari, bado anatazama maneno ya kinabii ya matumaini ya Giorgio la Pira, na kukumbusha kuwa, mtu anaweza kuzaliwa upya kutoka katika uzee, hiyo inajitokeza hasa tunapohisi kuwa na mahitaji na shauku ya ungofu na iwapo kweli tunakubali kuwa watafutaji wa matukio ya njia ya Pasaka na zaidi kwa kukubali kuzaliwa upya kutoka kwa aliye juu. Kutokana na hiyo ndipo anasema tnatakiwa kugundua kwa upya kwamba undani wetu umelemewa na mazito ya udhaifu na lazima kutafuta kufanana na Roho ambaye ni tajiri katika dhana mbalimbali za kiufundi na katika saa zetu ambazo utafiri ndizo zinapendekeza namna yetu ya kuishi na kutenda. Anatoa mfano kuwa Mtakatifu Paulo katika Barua ya kwanza ya kwa wakorinto anasema maneno maalum na makubwa ya ukweli wa kitasaufi na kibinadamu. Yeye anasema, kuwa  kwa maana hiyo sisi tusikate tamaa lakini hata kama ndani ya nje ya ubinadamu kuna uharibifu , lakini inawezekana kabisa kupyaishwa kila siku!

Kuvumilia katika majivu ya dunia hii: Kuna mantiki ambazo zinajihusha kwamba hakuna haja ya kuvumilia laikini ili usiweze  kukata tamaa mbele ya majivu ndani na nje yetu kuna uwezekano kkuvumilia kwani katika uumbaji wa pili inaweza kutimizwa kwa kila mtu kwa njia ya neno na kwa njia  ya kila  matukio. Huo ni mtazamo ambao unaweza kumrudishia binadamu hadhi yake kutoka katika dhambi. Hiyo inawezekana kabisa kutamani kutamani kweli Pasaka kila mahali na kilamantiki ambayo sisi tumeamua kuchagua, katika kutafakari nafasi ya kuishi kwa pamoja kama raia, kwa maana ni kuahidi kwasbau ya utambuzi kuwa sisi ni mavumbi na tunda linatokana na uharibifu, lakini lenye kuwa na matumaini na ndoto hasa ya kuacha hata kwa vizazi vijavyo. Kwa njia hiyo Abate anasema kuna haja ya kutofuata matokeo ya haraka ambayo yanazaliwa katika siasa za haraka, badala yake ni matendo ya dhati yenye uwezo wa kuunda jamii na uwezo wa kuifanya jamii ichanue maua ya kibinadamu zaidi.

Uwezekano wa kuanza upya: Maisha kwa hakika ni kawaida, ni kama saa inavyolazimisha kwenda mbele bila kusimama, lakini daima kuna kipindi cha kufanya maamuzi,  ndiyo nguvu ya mwanzo, nguvu ya mapya ambayo yanazaliwa kutokana na Roho, kutoka ndani ya moyo. Katika uchaguzi mkubwa ni ile ya uhuru wa mtu ambaye anapaswa anafanane na Kristo badala ya kukata tamaa na kukosa furaha. Anapaswa akuze ndani mwake matumaini ya maisha badala ya kuzima kila aina ya shauku na kusema kuwa hakuna haja ya sadaka katika maisha yote. Wito ni kwamba hakuna kusikiliza moono ya uzee wa moyo ambao unazuia kukua hata kwa vijana. Ni lazima kwenda kwa watu wazima na wenye macho mang’avu ya kuangaza matumaini anasema. Mungu anatutaka tuwe wenye uwezo wa kuota ndoto kama yeye na kwake yeye tutembee na umakini wa kuota ndoto tena, kuchota matumaini kupitia kumbukumbu ya asili ambayo ni chche nzuri na labda mwanzo hazikuwa nzuri na ambazo zilikuwa chini ya majivy labla ya kukutana kwa mara ya kwanza na Yesu.

12 March 2019, 10:20