Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Rais Marie-Louise Coleiro Preca wa Malta. Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Rais Marie-Louise Coleiro Preca wa Malta.  (Vatican Media)

Papa akutana na Rais Malta: Wakimbizi, Ushirikiano & dini

Papa Francisko na Rais Marie-Louise Coleiro Preca wa Malta katika mazungumzo yao, wamegusia pia mambo msingi yanayowaunganisha na hasa zaidi mwelekeo wa Bara la Ulaya kuhusu ushirikishwaji wa umma pamoja na hali ya Mediterrania. Mawazo makuu hapa ni wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji, ushirikiano wa kimataifa sanjari na majadiliano ya kidini!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 21 Machi 2019 amekutana na kuzungumza na Rais Marie-Louise Coleiro Preca wa Malta ambaye baadaye, amepata fursa ya kukutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Monsinyo Antoine Camilleri, Katibu mkuu Msaidizi wa mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican.

Baba Mtakatifu na mgeni wake, katika mazungumzo yao, wameridhika na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Vatican na Malta sanjari na ushirikiano kati ya Kanisa na Serikali ya Malta kama sehemu ya mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani katika masuala ya kijamii, kitamaduni na maisha yao kiroho kwa ajili ya familia ya Mungu nchini Malta. Wamepongeza mchango wa Kanisa hasa katika utume kwa vijana na hasa katika mafundisho ya katekesi ambayo yamewasaidia wengi katika maisha ya ujana wao! Viongozi hawa wawili katika mazungumzo yao, wamegusia pia mambo msingi yanayowaunganisha na hasa zaidi mwelekeo wa Bara la Ulaya kuhusu ushirikishwaji wa umma pamoja na hali ya Mediterrania. Mawazo makuu hapa ni wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji, ushirikiano wa kimataifa sanjari na majadiliano ya kidini!

Rais wa Malta

 

21 March 2019, 14:52