Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteua Monsinyo Tymon Tytus Chmielecki kuwa Balozi wa Vatican nchini Guinea na Mali na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Papa Francisko amemteua Monsinyo Tymon Tytus Chmielecki kuwa Balozi wa Vatican nchini Guinea na Mali na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. 

Mons. Tymon Tytus Chmielecki: Balozi wa Vatican: Guinea & Mali

Askofu mkuu mteule Tymon Tytus CHMIELECKI kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Mshauri wa Ubalozi wa Vatican. Alizaliwa kunako tarehe 29 Novemba 1965, Torun, Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 26 Mei 1991. Alianza utume wake katika diplomasia za Vatican kunako tarehe 1 Julai 1995.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Tymon Tytus CHMIELECKI, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Guinea na Mali na wakati huo huo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu. Askofu mkuu mteule Tymon Tytus CHMIELECKI kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Mshauri wa Ubalozi wa Vatican. Alizaliwa kunako tarehe 29 Novemba 1965, Torun, Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 26 Mei 1991.

Askofu mkuu mteule Tymon Tytus CHMIELECKI, ana shahada ya Sheria za Nchi na Sayansi ya Binadamu. Alianza utume wake katika diplomasia ya Vatican kunako tarehe 1 Julai 1995. Tangu wakati huo, amebahatika kutekeleza dhamana na utume wake katika Balozi za Vatican nchini Georgia, Senegal, Austria, Ucrain, Kazakhstan, Brazil na hatimaye, alipangiwa utume kwenye Idara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Sekretarieti kuu ya Vatican.

Balozi
27 March 2019, 09:41