Tafuta

Vatican News
Askofu mkuu Pedro Lopez Quintana ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Austria. Askofu mkuu Pedro Lopez Quintana ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Austria. 

Askofu mkuu Pedro Quintana, ateuliwa kuwa Balozi Austria!

Askofu mkuu Quintana alizaliwa tarehe 27 Julai 1953 huko Barbastro, nchini Hispania. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 15 Juni 1980. Kunako mwaka tarehe 12 Desemba 2002, akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II, kuwa Askofu na kuwekwa wakfu tarehe 6 Januari 2003 na Papa Yohane Paulo II mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Pedro López Quintana kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Austria. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Quintana alizaliwa tarehe 27 Julai 1953 huko Barbastro, nchini Hispania. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 15 Juni 1980. Kunako mwaka tarehe 12 Desemba 2002, akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II, kuwa Askofu na kuwekwa wakfu tarehe 6 Januari 2003 na Papa Yohane Paulo II kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Mwaka 2003, Askofu mkuu Quintana akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini India na Nepal. Kunako mwaka 2009 akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Canada na tarehe 28 Septemba 2013 akang’atuka kutoka madarakani. Tarehe 8 Machi 2014 akateuliwa tena na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Lithuania, Estonia na Latvia. Hatimaye, tarehe 4 Machi 2019, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Austria.

Askofu Mkuu Quintana

 

04 March 2019, 13:38