Tafuta

Vatican News
Askofu MKuu Ivan Jurkovič ametoa hotuba yake katika kikao cha 40 cha Mkutano wa Tume ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya haki za Binadamu mjini Geneva Askofu MKuu Ivan Jurkovič ametoa hotuba yake katika kikao cha 40 cha Mkutano wa Tume ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya haki za Binadamu mjini Geneva   (REUTERS)

Ask.Mkuu Ivan Jurkovič kuhusu Ripoti ya mwandishi maalum juu ya uhuru wa dini au imani!

Askofu Mkuu Jurkovičanasema kuwa Vatican inaendelea kupambana dhidi ya matumizi binafsi ya haki na kwa namna ya pekee wanapongeza jitihada zinazotolewa na baadhi ya Serikali ili kusaidia Wakristo wanaoteswa duniani kote,pamoja kuanzishwa kwa mifumo ya kisheria yenye ufanisi inayo heshimu haki hii na kuthaminiwa

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu Ivan Jurkovič, mwakilishi wa wa kudumu wa Vatican katIka ofisi za umoja wa mataifa mjini Geneva ametoa hotuba yake tarehe 5 Machi 2019 katika Kikao cha 40 cha haki za binadamu, kuhusiana na mada ya Ripoti ya Mwandishi Maalum juu ya Uhuru wa Dini au Imani. Katika hotuba yake anashukuru Ripoti ya Mwandishi Maalum juu ya Uhuru wa Dini au Imani ambapo anathibitisha kuwa na uhusiano wake wa karibu na haki ya uhuru wa kujieleza. Kama ilivyoelezwa katika Azimio la dunia  kuhusu Haki za Binadamu,ni  muhimu  kulinda kanuni za Mkataba katika kusudio la kusimamia na kutetea haki zote za binadamu na uhuru wa msingi wa mtu na dhamiri yake ya kujieleza kama haki asili ya kurithi na kuonesha heshima ulimwenguni awe mke au mme mwenye hadhi katika kutafuta ukweli na kutenda kulingana na hilo.

Askofu Mkuu Jurkovic aidha anasema katika tafiti na kujifunza kutokana na uzoefu, baada ya vitendo viovu  ambavyo vimekuwa kikiathiri dhamiri ya wanadamu katika karne iliyopita, jumuiya ya kimataifa ilikubali kuweka uhuru wa dini na imani, pamoja na haki ya uhuru wa kujieleza, kama moja ya nguzo msingi wa haki za kibinadamu. Na kwa maana hiyo katika miongo ya hivi karibuni, mfumo wa kisheria wa kimataifa kuhusu  haki hizi umeweza kuwa na mshikamano na uthibiti kwa kuhusishwa katika katiba ya kikanda na kitaifa.

Lakini pamoja na kuwa na maendeleo hayo mazuri, ripoti za hivi karibuni kuhusu unyanyasaji wa haki hii unashangaza, anabainisha Askofu Mkuu Jurkovic. Na kwa maana hiyo upowasiwasi mkubwa hawali ya yote kwa  kwa shida ya waathirika ambao, katika maeneo mengi ya dunia, na kwa ujasiri wanaendelea kukabiliwa na ubaguzi, kuvumiliana, unyanyasaji, kifungo, hata vifo kutokana na msiamamo wao wa Imani na dhamiri zao. Upo wasiwasi mkubwa hata kwa siku zijazo za jamii hizo, kwa mfano Askofu Mkuu Jurkovic anaongeza kusema kuwa   wakati watu na jamii hawataruhusiwa kuishi na kuadhimisha  kulingana na imani zao za kina,na zaidi kuna wvifungo vinavyowekea jamii pamoja kufutwa, na ukiukwaji wa haki mara nyingi hugeuka kuwa mgogoro wa vurugu.

Na kwa namna fulani, anasema hata mgogoro wa sasa wa kimataifa unategemea, pamoja na ushawishi unaokua ndani ya mashirika ya kimataifa ya nguvu na maslahi ambayo yanapendekeza maono na mawazo yao wenyewe na kusababisha aina mpya ya ukoloni wa kiitikadi na mara nyingi bila kujali utambulisho, hadhi  na uelewa wa watu. Kama Vatican inaendelea kupambana dhidi ya matumizi binafsi ya haki na kwa namna ya pekee wanapongeza jitihada zinazotolewa na baadhi ya Serikali ili kusaidia Wakristo wanaoteswa duniani kote, pamoja kuanzishwa kwa mifumo ya kisheria yenye ufanisi inayo heshimu haki hii na inathaminiwa. Akiendelea na hotuba yake amewambia wajumbe wa Mkutano kuwa miongoni mwa vipimo vingine vinavyotakiwa kuzingatiwa kwa hakika juu ya haki hii pia inahusu uhuru, katika ngazi binafsi, za kijamii au, dhidi ya aina yoyote inayotakakulazimisha kufanya vitendo kinyume na imani ya mtu.

Leo hii zaidi na zaidi, watu wa tamaduni tofauti, dini na imani wanaishi upande upande. Kwa hiyo kuna umuhimu na busara ya kuweza kuingiza sheria, kwa busara na hekima, kuwa na uchaguzi  ambao uruhusu kila mtu, akiwa na tatizo la dhamiri, kutenda kwa uhuru, kwa mujibu wa imani  ya kina anayokiri.  Hata hivyo, pamoja na mifano ya hivi karibuni ya kuongezek wito wa kuzuia hisia ambazo zinakataa haki na kuwa na ukatili ambao unaoneshwa kwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa baadhi ya wakazi katika mashirika ya kimataifa, kusahau hali yao na kutenda bila mamlaka, bado hawajali haki ya uhuru wa dhamiri na imani. Ufanisi wa ulinzi juu ya  uhuru wa dini na imani, pamoja na haki ya uhuru wa kujieleza, itasaidia usalama wa wakati endelevu ili kuweza kufikia ufanisi wa utekelezaji wa Agenda ya maendeleo endelevu kufikia 2030.

Askofu Mkuu Jurkovic amehitimisha akitazama ujumbe wa pamoja wa Baba Mtakatifu Francisko na Imam Mkuu wa Al-Azhar,Ahmad Al Tayyib, wa hivi karibuni ambao walitia sahini kwa pamoja kuhusu mazungumzo, ufahamu na kuhamasisha utamaduni wa kuvumiliana, kukubaliana na wengine na kuishi pamoja kwa amani na kwamba utachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kimazingira ambamo ndiyo sehemu kubwa ya watu wanaishi.

06 March 2019, 13:38