Tafuta

Vatican News
Kufunda wahudumu wa amani kwa hakika ni changamoto kubwa,kwa namna ya pekee katika mazingira ya chuo kikuu na ili kukuza mafunzo msingi ya kisayansi kwa ajili ya amani Kufunda wahudumu wa amani kwa hakika ni changamoto kubwa,kwa namna ya pekee katika mazingira ya chuo kikuu na ili kukuza mafunzo msingi ya kisayansi kwa ajili ya amani  (Vatican Media)

Ask.Gallagher:Kufunda wahudumu wa Amani ni changamoto!

Askofu Mkuu Paul Gallagher,Katibu Mkuu wa mahusianao na ushirikiano na nchi za nje Vatican akitoa hotuba katika semini ya mafunzo kwa wahudumu wa amani katika chuo kikuu cha kipapa Laterano amesema,kufunda wahudumu wa amani kwa hakika ni changamoto kubwa ili kukuza mafunzo msingi na maalum ya kisayansi

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 28 Februari 2019, Askofu Mkuu Paul Gallagher, Katibu Mkuu wa mahusianao  na ushirikiano na nchi za nje Vatican ametoa hotuba yake katika Semina ya mafunzo kwa wahudumu wa amani. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano. Na katika hotuba yake yake anashukuru kukaribishwa kwake ili kushirikisna nao kipindi cha maisha yao ya taaluma kinachojikita kwenye mazingira ya Chuo Kikuu cha Laterano na kozi mpya ya sayansi ya Amani na Taasisi ya Taalimungu ya Yohane Paulo II kwa ajili ya Sayansi ya Ndoa na Familia kwenye mtazamo wa Hati ya Gaudium et spes. Askofu Mkuu anathibitisha kuwa ni mchanganyikao ambao siyo wa bahati mbaya, kwani amani inajengwa kuanzia chini kwa njia ya michakato ya elimu na mafunzo.

Kufunda wahudumu wa amani kwa hakika ni changamoto kubwa, kwa namna ya pekee katika mazingira ya chuo kikuu kama hicho, ili kukuza mafunzo msingi na maalum ya kisayansi ambayo ni lazima yachote kutoka katika matendo ya Mafundisho ya Kanisa na Hati za Kanisa. Hili ni zoezi ambalo siyo rahisi lakini ni muhimu kwa sababu Chuo Kikuu kinabaki ni mahali penye  ishala ya ule ubinadamu fungamani ambao uhahitajika kuendelezwa daima na kupyaishwa, kwa kutajirishwa kwa sababu uweze kutambua kuzaa utamaduni jasiri uliopyaishwa na ambao katika nyakati hizi ndiyo unatafutwa, kama anavyoelekeza Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake kuhusu mafundisho ya Sayansi ya Amani kwa Kansela wa Taasisi ya Kipapa ya Laterano ya tarehe 12 Novemba 2018.

Na tazama wazo la Chuo Kikuu ni mahali ambapo uhamasishwaji wa kujua na kujitegemea,kuwa makini kwenye nidhamu tofauti ambazo daima zimekuwapo na kutarajiwa , kwa matumaini ya maisha ya mtu na watu, kama ilivyo kwa waamini na watu wa Mungu. Thamani yake inaonesha, na si tu kama jambo la kutazamia kwa kila mtu na kama wema ulio mkuu wa maono ya imani, lakini pia hata kwa nidhamu ya mafunzo na utamaduni, uwezo wa kuchota kutoka katika sayansi na ujuzi mwengine ambao ndiyo kiini msingi ambacho wahudumu wa amani wanapaswa wachote na kumwilishwa.

Utafiti wa amani unataka urudi katika msingi wa mahusiano ya kibinadamu na hivyo kuweza kwa upya jurudi katika msingi ambao ni utaratibu wa Taifa na kama vile wa kimataifa kwa jinis inavyorudia mara nyingi kukumbusha hati ya Mtaguso wa II wa Vatican, Gaudium et spes. Hii ndiyo maana ya kweli ya amani ambayo inajengwa kwa njia ya uchaguzi wenye msingi juu ya nguvu za kimaadili na mwenendo wa dhati wa kimaadili na tabia ya uwezo wa kujitambua mtu kama asili na mwisho wa kila tendo.

Hata hivyo Askofu Mkuu anathibitisha kwamba mambo hayo tunatambua kuyaelewa zaidi baada ya kuwa na uchungu wa migogoro  na umwagaji damu na migawanyiko ndani ya taifa lenyewe. Badala yake amani inapaswa iwe ndiyo msingi imara na muundo wa maisha ya watu na kati ya mataifa, kuwa ndiyo uchaguzi mkuu na vyombo vya kisiasa, kisheria na taasisi zote kwa mantiki ya kukuza amani.

Leo hii ni tishio la amani linawakilishwa si tu na utamaduni za migogoro ya kisilaha ndani ya nchi na kimataifa, lakini pia hata na hali nyingine. Kwa namna hiyo inapbidi kuwa na utashi wa serikali kuingilia kati kwa dhati ili kutoa jibu mwafaka katika katiba na maamuzi ambayo yabaki kuwa ni utekelezaji wa dhati. Na iwapo haifanyiki basi inasababisha H kuunda hali isiyo kuwa na imani na mivutano katika maisha ya kutaifs, wakati ingekuwa ulazima wa kupyaisha matendo ya pamoja ili kufungua njia za kukabiliana na hatua kubwa za kutafuta amani.

Kwa maana hiyo ndiyo kuna zoezi kubwa la kuwaandaa wahudumu wa amani iwapo upo utashi wa kutaka kuhakikisha amani latola jamii na kuhepuka migogoro. Ni kwa njia hiyo inawezekana kupata haki ya kila nchi ambayo inapendelea kila mtu , watu na jumuiya nzima kuishi kwa amani. Mafunzo ni njia ya dhati japokuwa haizuii matatizo kwa ajili ya kuelekeza utamaduni wa amani, ikiwa na utambuzi wake wa kujenga na ambao lazima uwe ni matarajio na shauku kwa wote. Askofu Mkuu Gallagher amalizia kusema, Baba Mtakatifu alipokutana na wanadiplomasia tarehe 7 Januari 2019 alisema ni kukuza uhusiano wa urafiki ambao unatuunganisaha na kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya ujenzi wa amani ambayo dunia inahitaji.

01 March 2019, 14:36