Tafuta

Vatican News
Kuwa na utambuzi na kuelewa nini maana ya uyahudi ni suala moja muhimu katika juhudi za kupambana na ubaguzi,kuondoa ujinga na hukumu Kuwa na utambuzi na kuelewa nini maana ya uyahudi ni suala moja muhimu katika juhudi za kupambana na ubaguzi,kuondoa ujinga na hukumu 

Vatican:ukosefu wa elimu na hukumu ni vichochezi vya ubaguzi!

Haja ya kutetea hadhi ya binadamu kwa kuhakikisha uhuru wa dini ndiyo mada kuu ya hutoba ya Padre Norbert Hofmann mwalikishi wa Vatican katika Mkutano wa Shirika kwa ajili ya usalama na ushirikiano barani Ulaya (OSCE).Mkutano huo ulijikita juu ya mapambano ya ubaguzi katika Kanda hizo mjini Bratislava,Slovakia

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 5 Februaria katika Mkutano juu ya mapambano ya ubaguzi katika Kanda za Shirika kwa ajili ya usalama na ushirikiano barani Ulaya (OSCE) mjini Bratislava, Mwakilishi wa Vatican, Padre Norbert Hofmann, S.D.B,  hotuba yake imejikita kusisitizia juu ya kulinda hadhi ya binadamu na uhuru wa dini na ili pasitokee aina zozote za kiubaguzi.

Kulinda hadhi ya binadamu, kuhakikisha uhuru wa dini

Kwa kukumbuka wito wa Baba Mtakatifu juu ya kuhifadhi kukumbuku hai ya janga la wakati uliopita na ili kujifunza historia na makosa ya nyuma yasirudiwe tena, Mwakilishi huyo ameonesha kwamba, ili kuweza kuthibiti ubaguzi huo ina maana  kwanza ya kutambua hali halisi na changamoto za dhati ambazo jumuiya ya kiyahudi iliweza kuptia na kuishi, na kwa upande mwingine kuha haja ya uangalizi na kulinda hadhi ya binadamu, uhuru wa dini  kwa kuhifadhi misingi ambayo haileti ubaguzi. Aidha kwa mujibu wa Padre Hofmann, shughuli hizo kwa ajili ya wakristo zinatoa chachu msini ya mahusiano kati ya ukristo na uyahudi,na kwamba kama alivyokuwa amesisitiza Baba Mtakatifu kuwa Mkristo wa kweli hawezi kuwa na Ubaguzi (Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko kwa Jumuiya ya Kiyahudi Roma tarehe 11 Oktoba 20173)

Ubaguzi wa kidini unahatarsisha usalama wa kimataifa

Padre Hofmann akipongeza juhudi za Shirika kwa ajili ya usalama na ushirikiano barani Ulaya (OSCE) kuhusiana na suala la matatizo ya kutovumiliana,chuki na vurugu, ubaguzi wa Kiyahudi kama vile hata ule unao wakumba wakristo, waislam au watu wa dini nyingine kwa hakika ni hatari ya usalama na ambao unaweza kusababisha nafasi pana na ngaza yenye uwezo wa kudidimiza msimamo wa kimataifa.

Hata hivyo pongezi hizo zimetolewa kutokana mwongozo wa kutambua uhalifu wa chuki na ubaguzi na kukabiliana na mahitaji ya usalama wa jumuiya ya wayahudi kama ilivyokuwa imetangazwa katika Gazeti la Ofisi ya OSCE  kwa ajili ya Demokrasia ya Kariba na  Haki za binadamu (ODIHR). Mwakilishi wa Vatican anahitimishwa kwa kuunga mkono juhudi ambazo wakati ujao anaseama kuwa, wanaweza kuziweka katika kazi zaidi hata kwa ajili ya kukabiliana na usalama wa jumuiya za kikristo kwa kuzingatia hali halisi mbaya wanayoisho baadhi ya maeneo ya nchi za OSCE kama vile mashabulizi ya Kanisa,Madhabahu na majengo ya Kanisa.

Ujinga na hukumu vichochezi vya ubaguzi

Kuwa na utambuzi na kujua nini maana ya uyahudi ni suala moja na  muhimu ili kuweza kuongeza juhudi zaidi za kupambana na ubaguzi, kwa kuondoa ujinga na hukumu mbalimbali. Kwa mtazamo wa Padre Hofmann amekuwa na utambuzi wa thamani ya juhudi ya Ofisi ya OSCE kwa ajili ya Demokrasia ya Katiba na Haki za Binadamu (ODIHR) ambayo inarahisisha mabadilishano mema ya matendo kati ya Serikali.

06 February 2019, 16:18