Tafuta

Vatican News
Kukabidhi Tuzo ya Jacques Hamel kwa Christelle Ploquin katika Siku za Kimataifa za Mtakatifu Francisko wa Sale huko Lourdes, tarehe 1 Februari 2019 Kukabidhi Tuzo ya Jacques Hamel kwa Christelle Ploquin katika Siku za Kimataifa za Mtakatifu Francisko wa Sale huko Lourdes,tarehe 1 Februari 2019   (Vatican News)

Tuzo ya padre Jacques Hamel 2019 huko Lourdes!

Kuanzia tarehe 30 Januari hadi 1 Februari 2019,umefanyika Mkutano wa Siku ya 23 ya Siku za Kimataifa za Mtakatifu Francisko wa Sale,zilizoongozwa na mada ya uandishi na imani.Siku ya mwisho ilitolewa Tuzo ya padre Jacques Hamel kwa washindi wa toleo la pili la Shirikisho la Vyombo vya Habari Katoliki duniani

Na Sr. Angela Rwezaula - Lourdes

Kuanzia tarehe 30 Januari hadi 1 Februari 2019 umefanyika Mkutano Siku ya 23 za Siku za Kimataifa za Mtakatifu Francisko wa Sale zilizoongozwa mwaka huu na “uandishi na imani”. Ni mkutano wa siku tatu ambao umeandaliwa kwa ushiriki wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano,Shirikisho la Vyombo  habari Katoliki na Signis, pamoja na tofauti zao za kimataifa umewezesha kwa dhati ushiriki wa kipekee wa kubadilishana maoni na mitazamo mbalimbali ya Kanisa, familia, siasa na jamii kwa ujumla.

Mada ya Uandishi  na imani iliongoza siku za mkutano

Katika siku hizi ya mkutano wa Siku ya 23 za Siku za Kimataifa za Mtakatifu Francisko wa Sales, wataalam karibia kutoka nchi 30 za mataifa mbalimbaali duniani wameshiriki pamoja ili kubadilishana kati ya waandishi wa vyombo katoliki, wataalam wengine wa masuala ya kijamii na kisiasa na wakuu wa mawasiliano ya Kanisa chini ya mwongozo wa msimamizi wa waandishi wa habari wa Mtakatifu Francisko wa Sales. Hata hivyo mwaka 2019, idadi ya waliodhuria imeongezeka maradufu na pia kwa ushiriki wa  waandishi wa Habari 8 kutoka katika vyombo vya mawasiliano Vatican wakiambatana na Rais wa Baraza la Kipapa  Bwana Paulo Ruffini. Ilikuwa ni njia mojawapo ya kuweza kushirikishana uzoefu na tafakari ya kina na waandishi wengine wa mawasiliano kutoka duniani,hasa kwa mtazamo wa mada iliyokuwa inaongoza ya uandishi na imani.

Na Katika hotuba ya Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Bwana Paulo Ruffini alisema kuwa: uandishi mzuri daima lazima utafuta ukweli. Ni kujibidisha katika uandishi wa sanaa ya kutazama kabla ya kusimulia, kutambua kabla ya kutoa ufupisho,kujaribu kuelewa zaidi ya kuwa na ujujuu tu. Na hii ina maana ya kutazama mambo ambayo wengine hawaoni, kusimulia mambo ambayo wengine hawasimulii, kujua ishara za nyakati na kuweza kuziweka katika tovuti au mtandao kwa kile ambacho wengine wanabagua ili kushinda utofauti na kutoa tafakari ya kina ya kujiuliza. Vile vile Bwana Ruffini katika hotuba yake pia ameonesha kuwa, mara nyingi uandishi unagubikwa na uongo wa uaminifu  au hukumu. Kwa kutazama mada iliyoongoza mkutano amethibitisha mwa imani inasaidia iwapo kuna mzizi wa ukweli na imani upelekea katika  njia ya uongo iwapo kuna mzizi wa ulaghai. Kwa maana hiyo anaseama,“Uandishi wetu wakati mwingine hubaki ni wa kijujuu” hivyo anapendekeza kuwa na mtazamo wa uandishi wa kikristo  ambao unapaswa uwe wa kutafuta na kutambua umoja halisi wa kuweza kujikita katika utambuzi wa jambo gani linaunganisha mambo yote kwa pamoja.

Siku za Mkutano na mada ya uandishi na imani

Tarehe 30 Januari 2019 baada ya makaribisho na kujiorodhesha, washiriki wote wameweza kupata fursa ya ufahamu wa historia ya Lourdes na sehemu zake zote na kwa kutazama film kuhusu historia na ujumbe wa Lourdes, kadhalika kwa kuongozwa kutembelea madhabahu na sehemu zake hasa katika maisha ya Mtakatifu Bernadetta Soubirous. Siku zilifunguliwa rasmi jioni na Misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu Nicolas Brouwet wa Jimbo la Tarbes na  Lourdes. Na Mara baada ya misa wote waliingia katika ukumbi wa mkutano ambapo, François Ernenwein, aliyekuwa mratibu wa kuwakilisha siku alimkaribisha Askofu Nicolas Brouwetna Jean-Marie Montel, Rais wa Shirikisho la Vyombo vya habari  Katoliki; Bi Helen Osman, Rais wa  Signis na Bwana  Paolo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican. Na kwa kuongozwa na mada ya uandishi na imani na wakati wa kusikiliza hotuba zao, waandishi wamealikwa kujikita kwa dhati katika misingi ya shughuli zao na kuwajibika.

Kadhalika katika ukumbi wa Mtakatifu Bernadetta kulikuwa na ujumbe kwa njia ya video wa Jean Vanier ni mwanafalsafa kutoka Kanada na mwanzilishi wa Jumuiya ya Arca, jumuiya yenye tasaufi ya imani na mwanga na amewahi kuwa mjumbe wa Baraza Kipapa la Walei. Ujumbe wake kwa njia ya video  ulikuwa unatazama magazeti ya Kikristo na kuzungumzia juu ya dharura ya kuunganisha imani na uwazi. Vilevile yalifuata mazungumzo kati ya Rais wa Signis wa Vyama Katoliki  vya Habari duniani Bi Helen Osman, (USA) na  François Euvé, Mkurugenzi wa gazeti la Études. Hawa walijikita katika maswala kuhusu uaminifu na kujiuliza kama kweli kuamini kunaweza kusaidia kuishi kinyume na dunia inavyotaka hasa ya kuishi kibinafsi. Padre  André Cabes, Msiamamizi wa Madhabahu na Klaus Nientiedt, na Mwariri Mkuu wa Gazeti la Konradsblatt (Freiburg  Breisgau, Ujerumani) waliweza kujibu maswali ambayo yalikuwa yanahusu:Kanisa linaweza kuishi njia zipi katika imani nyingi? Nini maana ya nafasi ya majadiliano na kazi ya kichungaji? Bwana Dominique Potier, naibu wa chama cha kijamii wa Meurthe-et-Moselle, Ufaransa na Daniel Bougnoux, mwanafalsafa waliweza kufafanua zaidi kwa kuchunguza nafasi ya imani katika utamaduni, elimu na uwepo wao muhimu katika demokrasia.

Imani nadani ya familia shule na katika siasa

Alhamisi tarehe 31 Januari 2019 siku ilifunguliwa na Misa Takatifu, iliyoongozwa na Askofu Norbert Turini, Askofu wa Jimbo la Perpignan-Elne Ufaransa. Siku hiyo ilikuwa na mchanganyiko mzuri wa kubadilishana mawazo na majadala wa kuchunguza imani katika sehemu mbalimbali za jamii, ndani ya familia, shule na katika siasa na watoa mada walikuwa ni Anne Muxel, mwanasayansi wa siasa na padre Nigel Barrett, wa Jimbo Kuu la Bombay (India). Hata hivyo asubuhi hiyo, Profesa Alain Bentolila, mtaalam wa lugha na padre Walter Chikwendu Ihejirika, Profesa wa Chuo Kikuu cha Port Harcourt nchini  (Nigeria) na Rais wa Signis kwa upande wa Afrika, alitoa mjadala kuhusu Shule na Imani, kwa kuongozwa na mada: “Masuala  ya shule”. Kadhalika walifuata Bwana Paul Piccarreta, mkurugenzi wa gazeti  la Review Limites na Bernard Perret, mwanauchumi, ambaye alijikita kufafanua na kuelezea  matokeo majaribio ya kutumia misimamo kwa ajili ya kupamba na hali ya sasa. Mchana kulikuwa na fursa  maalum za kutafakari na kushirikishana kwa waandishi wa habari na wawakilishi wa mauzo ya bidhaa hasa kwa upande wa vyakula na vinywaji.

Ushuhuda unaosababisha kuzingatia mambo ya kidini

Kuanzia 12:30 jioni, Jean Birnbaum, mhariri mkuu wa dunia ya vitabu (Le Monde des livres), na mwandishi wa utafiti juu ya uharibifu unaosababishwa kukataa kuzingatia mambo ya kidini katika uwanja wa kisiasa, alisaidia washiriki wa mkutano kutafakari juu ya matokeo ya “ukimya wa kidini” na kutoa ushauri wa njia za kufuata mbele. Jioni, kulikuwa na uwasilishaji wa Tamasha la muziki wa “Bernadette wa Lourdes”, ambao utaoneshwa katika mji wa Maria katika chumba cha Robert Hossein, kuanzia  tarehe 1 Julai 2019.

Askofu  atoa  Tuzo ya  Jacques Hamel

 Siku ya mwisho ilianza na maadhimisho ya misa ya kufunga na kuwasilishwa kwa Tuzo ya Jacques Hamel, mbele ya Bi Roselyne Hamel, dada wa Pade Jacques Hamel, aliyeuwawa na magaidi wawili tarehe 26 Julai 2016, huko Saint  Etienne-du-Rouvray (Ufaransa). Tuzo imeweza kukabidhiwa Ijumaa asubuhi tarehe 1 Februari 2019 huko Lourdes wakati wa kuhitimisha Siku ya 23 za Siku za Kimataifa za Mtakatifu Francisko wa Sale zilizoongozwa na mada mwaka 2019 uandishi na imani. Aliyealikwa na Shirikisho wa Vyombo Katoliki vya Habari kutoa tuzo ya Jacques Hamel kwa washindi wa Toleo hili la pili la mwaka huu ni Askofu Dominique Lebrun na ambaye ametangaza kuwa mchakato wa kijimbo kwa ajili ya kumtangaza Mwenye heri Mtumishi wa Mungu Padre Jacque Hamel utafungwa rasmi tarehe 9 Machi 2019 saa 4.30 katika Jimbo Kuu la Rouen Ufaransa. Katika mchakato wa mwisho wa Jimbo mara baada ya kuhakiki shuhuda za mwisho, taarifa zote zitafungwa rasmi na kuletwa katika Shirika la Kipapa lamchakata wa kuwatangaza watakatifu Vatican.

Tuzo ya Padre Jacque Hamel kwa Christelle Ploquin

Baada ya Misa iliyoongozwa na Askofu, Dominique Lebrun ya kuhitimisha Mkutano wa Siku ya 23 ya  Mtakatifu Francisko wa  Sales, ambaye ni Msimamizi wa waandishi wa Habari, iliyoongozwa na mada ya Uandishi na imani, “Tuzo Padre Jacques Hamel”, ilitolewa kwa ajili ya kumbukumbu ya Padre huyo, aliyekuwa na umri wa miaka 84. Tuzo ya mwaka huu, imetolewa kwa Mkurugenzi Christelle Ploquin na kaka yake, Padre mdominikani Adrien Cadried ambao walitengeneza picha iitwayo Injili ya Tano na kusikilizwa katika Radio na Tume ya Televisheni, nchini Ufaransa likiwa na fundisho la toleo la Siku ya Bwana. Filamu  hiyo inajikita katika maandishi ya Henri Verges Mtawa wa kwanza aliyeuwawa tarehe 8 Mei 1994 nchini Algeria wakati wa kipindi cha giza nene na ambaye ametangazwa mwenye heri na wengine 18 wafia dini tarehe 8 Desemba 2018 huko Oran.

Maadhimisho siku ya 23 ya Mtakatifu Francisko wa Sales na utoaji wa tuzo huko Lourdes

Wakati wa Maadhimisho ya kutoa tuzo hiyo dada yake marehemu Padre Jacques  Roseline Hamel, amemshukuru Mwenyekiti wa Shirikisho la Habari Katoliki Bwana Jean-Marie Montel. Maneno ya Roselyne, dada yake Padre Jacques wakati anasoma hotuba yake yalikuwa yanachoma moyo kwani alisema:“Mungu wa Upendo na huruma, amekuchagua uwe katika huduma ya wengine ili kukuza upendo, kushirikiana na kuvumiliana miongoni mwa watu wa imani zote. Tujifunze kuishi pamoja kwa maana sisi ni mafundi wa amani, kila mmoja kwa njia yake mwenyewe, kwa sababu ulimwengu unahitaji tumain”.

Mkutano wa mwisho ulifunguliwa kwa vidokezo vya masoko kutoka kwa mwana Blogger Erwan Le Morhedec, mwanasheria, anayejulikana zaidi na kwa jina la Koz na mwanaelimu jamii Jean-Marie Charon. Kuanzia saa 5 asubuhi,Bwana Guillaume Tabard, mhariri mkuu na kiongozi na wa kisiasa huko Figaro na Padre Jean-Paul Sagadou, mwakilishi kutoka Jimbo la Maria mpalizwa huko Afrika Magharibi ya Afrika aliweza kuoneshwa kwamba vyomvo vyote vya habari vina Imani, baadhi ikiwa ni ya wazi na wengine ikiwa ni ya kichini. Na hatimaye, Gilles Vanderpooten, mkurugenzi mkuu wa Espoirs na Michel Zanzucchi, mhariri wa habari wa Gazeti la Avvenire nchini (Italia),waliweza kujikita katika kutoa majibu ya ufumbuzi ambayo yanaweza kuongoza uandishi wa habari ukawa mzuri wa kuaminika na bora kwa ajili ya jamii ya sasa duniani kote.

01 February 2019, 16:33