Tafuta

Wanashirika wa Maria wa Mercede wakimkaribisha Baba Mtakatifu kukutana naye wakati wa fursa ya kuadhimisha miaka 800 ya kuanzishwa shirika lao Wanashirika wa Maria wa Mercede wakimkaribisha Baba Mtakatifu kukutana naye wakati wa fursa ya kuadhimisha miaka 800 ya kuanzishwa shirika lao 

Kard.Sandri ametoa wito wa kuwa na ukaribu na wahamiaji!

Tarehe 20 Januari 2019 wakati wa kufunga Jubilei ya miaka 800 ya Shirika la Maria wa Mercede,Kardinali Leonardo Sandri,Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki,ametoa wito wa kuendeleza juhudi ya kuokoa watumwa wa biashara ya binadamu.Watumwa leo hii hawana minyororo miguuni,wanalazimika kuacha ardhi zao zilizotembelewa na vita au umaskini

Na Sr.Angela Rwezaula - Vatican

Wakati wa maadhimisho ya kufunga Jubilei ya miaka 800 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Maria wa Mercede, Kardinali Leonardo Sandri Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki, ametoa wito kwa wanashirika kuendeleza juhudi za mwanzishi wa shirika ili kuokoa watumwa wa biashara ya binadamu, kwa maana anathibitisha kwamba,watumwa wa leo  hii hawana minyororo miguuni, bali wanalazimika kuacha ardhi zao zilizotembelwa na vita au umaskini.

Kardinali Leonardo Sandri Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki amethibitisha hayo siku ya  Jumapili tarehe 20 Januari 2019 wakati wa misa yakatifu aliyoiadhimisha katika Kanisa Kuu la Mama yetu wa Bonaria huko Cagliari Sardegna Italia katika fursa ya kuhitimisha Jubilei ya Mwaka wa 800 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Bikira Maria wa Mercede (Wamacerdari 1218-2018). Cagliari ni mji mkuu wa Sardegna, mahalia ambapo bahari inapokea maisha ya watu na wakati huo huo maelfu na maelfu wanakufa katika bahari ya meditranea katika miaka ya mwisho ambapo anakumbuka hata janga la hivi karibuni la vifo vya wahamiaji baharini.

Yote hayo anasema ni  tunda la biashara mbaya ya binadamu, inayowakumba watu wenye suta na ambao wana mizizi yao na misingi yao. Kwa maana hiyo Kardinali  anatoa wito wa kujikita katika huduma ya uhuru, na hasa kuwasaidia wale ambao  wamafungwa na minyororo ya biashara mbaya ya utumwa  na zaidi  kujiuliza juu ya thamani ya maisha kuwa kila maisha, tangu kutungwa kwake hadi kifo chake na kwamba lazima kuhudumiwa na kuheshimiwa katika kila kona ya dunia.

Kardinali Sandri katika tafakari yake amefafanua  juu ya tasaufi ya familia ya  Shirika la Wamercede, ambapo amekumbuka hata hotuba ya Baba Mtakatifu alipokutana nao  kunako tarehe 6 Desemba 2018. Katika hotuba yake Papa Francisko alisema kuwa  shirikia lao linajikita katika uzoefu wa utambuzi ya kuwa wao wamekuwa wa kwanza kukombolewa na Kristo, kwa utambuzi wa kukombolewa na Bwana ili waweze kuwasaidia watu kutoka utumwa binafsi, wakati huo huo nao waweze kuwasaidia watu wengine ambao wanaishia katika mambo ya kidunia na utumwa na hawajuhi namna ya kuondokana na mtindo huo wa utumwa.

Kuendelea kutumikia sura ya mweye kuhitaji  kwa dhati siyo kitu ambacho kinawaondolea hadhi yao, badala yake kinachanua na kuwafanananisha na Yesu Kristo aliyekabidhiwa juu ya msalaba na Baba, kwa ajili ya kuwakomboa ndugu wote kuanzia na jambazi aliyekuwa anapumua pembeni mwake kardinali anabainisha. Aidha amewakumbusha alivyokutana na familia ya Wamecerde kwa miaka ya mwisho katika fursa mbili, hasa ya mwisho wakati wa kufanya uchaguzi mkuu wa Shirika 2016. Na tangu wakati huo ameweza kushangazwa na baadhi ya karama zao za asili na  tafakari katika kujikita kwenye matendo yao leo hii katika safari ya pamoja ya Makanisa ya Mashariki.  Akitazama historia ya shirika anasema, Roho Mtakatifu alimjalia Mtakatifu Petro Nolasco ili kuweza kuona, kwa sababu yeye alikuwa ni mfanyabiashara ya vitambaa vya nguo. Yeye aliweza kutambua wakati akiwa katika safari za dunia hii na kuona wengi walivyokuwa watumwa na wanauzwa kwa maana hiyo ilitoka katika katika biashara ya vitambaa ikabadilika kuwa ya watu nandipo yeye alianza kujikita katika juhudi ya kuwakomboa na kuwarudishia uhuru wao!

Ni mambo mangapi yalitokea machoni pa Mtakatifu Pietro Nolasco nchini Uhispania katika Karne ya XIII amesisitiza Kardinali Sandri na kuongeza kusema kuwa,  hiyo ni sawasawa na hali wanayoishi wakristo wengi pamoja na wale wachache nchini Siria, Iraq, zaidi ya katika nchi ambazo zinawapokea watu kutoka katika mataifa. Katika hali hii Mtakatifu  Nolasco bado anaendelea  kupambana na kutafakari juu ya mifumo isiyo kuwa na haki katika zama hizo, kama alivyoamua kukutana na mteswa na kujiweka mstari wa mbele kuthubutu. Ndiyo  njia ya Injili inayohusu msamaria mwema aliyeinana ili kufunga majeraha ya mtu aliyeachwa amejeruhiwa na majambazi na kulipa gharama kutoka mfukoni mwake katika nyumba ya wageni ili aweza kuponya na kurudishiwa hadhi yake amesisitiza Kardinali Sandri!

 

 

 

22 January 2019, 15:16