Tafuta

Vatican News
Vatican inaendelea kuimarisha mfumo wa usimamizi wa rasilimali fedha kwa ajili ya mchakato wa uinjilishaji. Vatican inaendelea kuimarisha mfumo wa usimamizi wa rasilimali fedha kwa ajili ya mchakato wa uinjilishaji. 

Vatican yajiunga na mfumo wa malipo kwa njia ya Euro!

Bodi ya Baraza la Malipo Ulaya, EPC, imeidhinisha upanuzi wa mtandao wa huduma yake kijiografia kwa nchi zinazolipia gharama kwa kutumia fedha moja ya Euro kwa Vatican, kuanzia tarehe 1 Machi 2019 itakapojiunga rasmi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

 

Usimamizi wa fedha za Kanisa katika: ukweli, uwazi, uadilifu na weledi ni kati ya mambo yanayoendelea kupewa msukumo wa pekee na Baba Mtakatifu Francisko ili kweli rasilimali fedha iweze kutumika kiaminifu katika mchakato wa uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili! Bodi ya Baraza la Malipo Ulaya, EPC, imeidhinisha upanuzi wa mtandao wa huduma yake kijiografia kwa nchi zinazolipia gharama kwa kutumia fedha moja ya Euro kwa Vatican, kuanzia tarehe 1 Machi 2019 itakapojiunga rasmi.

SEPA Barani Ulaya inaratibu malipo yote yanayofanyika Barani Ulaya kwa njia ya Euro. Inawawezesha walaji, wafanyabiashara na viongozi wa Serikali mbali mbali kutuma, kupokea au kukopa fedha kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa, kiasi cha kulahihisha malipo ya ndani yanayofanyika kwa njia ya fedha ya Euro! Mpango huu wa SEPA unazijumuisha nchi 36 kati yake kuna Nchi 28 ambazo ni Umoja wa Ulaya. Na nyingine ni Iceland, Norway, Liechteinstein, Uswiss, Monaco, San Marino, Andorra na Vatican.

Akizungumzia kuhusu makubaliano hayo, Dr. Renè Bruehart, Rais wa Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF anasema, hatua hii itasaidia sana kurahisisha ulipaji wa fedha na huduma na kwamba, hiki ni kielelezo makini kuwa, Vatican inaendelea kuimarisha misingi ya ukweli na uwazi katika masuala ya rasilimali fedha!

Vatican: Euro 2019
03 December 2018, 08:30