Tafuta

Vatican News
Nyota ya Daudi huko Betelehem, mahali alipozaliwa Yesu Nyota ya Daudi huko Betelehem, mahali alipozaliwa Yesu  

Ukarabati Bethlehem:Kard.Sandri anasema,sanaa ni njia ya upatanisho na amani!

Kardinali Sandri anasema, katika ukosefu wa haki na mateso, hata ukoesfu wa uwezo wa kupata sauti moja yenye kuwa na mamlaka ya kuwakilisha hali halisi za watu, hasa wale walio wadhaifu wakati huo huo kuendelea kubaki na migawanyiko ndani na nje ya Nchi Takatifu, basi ni sanaa inaweza kugeuka kuwa njia ya kuleta muungano, mapatano na amani

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni nyakati ambazo kwa bahati mbaya zinaendelea na mivutano,  ukosefu wa haki  na mateso, lakini pia hata ukoesfu wa uwezo wa kupata sauti moja yenye kuwa na  mamlaka ambayo yanaweza kuwakilisha hali halisi  za watu, hasa wale walio wadhaifu, wakati huo huo bado kuna hali ya kuendelea kubaki na migawanyiko na kila mmoja kufuata matashi yake binafisi ndani na nje ya Nchi Takatifu na kutokana na hiyo basi ni sanaa tu inaweza kugeuka kuwa njia ya kuleta muungano, wa mapatano na amani. Hayo yamesema na Kardinali Leondardi Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki wakati wa tukio la uzinduzi wa ukarabati wa Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Bwana huko Bethlehem, tukio lililofanyika mjini Roma tarehe 12 Desemba jioni masaa ya Ulaya.

Utambuzi wa jumuiya tatu zinazohudumia maeneo matakatifu

Akiendelea na hotuba yake, Kardinali Sandri amesema kuwa ni wajibu wao kuwafanya hao wasijikie kutambuliwa kwa upande wa Jumuiya tatu ambapo ni Upatriaki wa Kigiriki- Korthodox, Kiarmenia na wasimamizi wa nchi Takatifu, ambao ni ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko. Jumuiya hizo kwa pamoja wanasaidia kulinda mahali patakatifu kwa mujibu wa utamaduni wa kale, ambao ni lazima kuhudumisha.  Lakini pia Kardinali  ameongeza, kusema kuwa pia ni lazima  kupongeza matokeo ya uamuzi wa kuanzisha kazi hiyo kwa upande wa Serikali ya Palestina ambao wanaendelea kulinda na kusaidia huduma yao hao wahudumu wa eneo Takatifu

Akiwageukia washiriki wa tukio hilo, Kardinali Sandri amesisitiza juu ya ushiriki wao kwa dhati na kwamba:kila mmoja katika maisha, hawali ya yote, hata kwa njia ya mchango wake, wanaweza kuchagua kujitoa kwa ajili ya kuwezesha ukarabaiti na ambao unafanana na ule wa mamia elfu ya mapambo mazuri ya rangi hasa inayohusu eneo hilo Takatifu. Licha ya hayo kila mmoja anaweza kuwa sehemu ya jiwe moja lililo nakshiwa. Na kwa pamoja wanaweza kuunda ule unakishi wa Kanisa hilo muhimu! Kwa maana hiyo  Kardinali Sandri amewaalika wote na kuwatakia mema ili amani na mwanga wa Bethlehem uwe kwao ujumbe wa amani kwa watu wote hasa kwa nchi ya Palestina.

KARD.SANDRI:UZINDUZI WA UKARABATI WA BETHLEHEM

 

13 December 2018, 15:00