Tafuta

Vatican News
Prof Andrea Tornielli  Mkurugenzi mpya Uhariri Vatican na Prof Andrea Monda Mkurugenzi wa Osservatore Romano Prof Andrea Tornielli Mkurugenzi mpya Uhariri Vatican na Prof Andrea Monda Mkurugenzi wa Osservatore Romano 

Prof.Tornielli ni Mkurugenzi mpya wa uhariri Vatican

Tarehe 18 Desemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Dk. Andrea Tornielli kuwa Mkurugenzi mpya wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican na Profesa Andrea Monda kuwa Kkurugenzi mpya wa Gazeti la Osservatore Romano

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 18 Desemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko, amemteua Dk. Andrea Tornielli kuwa Mkurugenzi mpya wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Vatican. Dk.  Andrea Tornielli alizaliwa huko Chioggia (VE), Italia kunako tarehe 19 Machi 1964. Mafunzo yake katika shule mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Padova Italia mahali abapo alitunukiwa shahada ya Hisotria ya Lugha ya Kigiriki. Tangu 1992 hadi 1996 amekuwa mhariri mkuu wa Gazeti la kila mwezi (siku 30) na kuanzia 1996 hadi 2011 amefanya kazi katika gazeti la Kila Siku nchini Italia. Kunako mwezi Aprili 2011 alijiunga  tena katika Gazeti la  Stampa, mahali ambapo ameweza kuratibu ukurasa wa Vatican Insider katika mtandao. Anaishi kati ya Roma na Milano na ameoa, baba wa  familia ya watoto watatu. Wakati huo huo pia Baba Mtakatifu amekubali kung’atuka kwa Mkurugenzi wa Uhariri wa Gazeti la Oservatore Romano Profesa Giovanni Maria Vian na akamteua katika nafasi hiyo. Profesa Andrea Monda.

Profesa Andrea Monda, mwandishi wa vitabu na mwariri. Alizaliwa mjini Roma tarehe 22 Machi 1966 na baba wa familia ya mtoto mmoja.  Anayo shahada ya uzamivu wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Sapienza Roma pia shahada ya Sayansi ya Dini katika Chuo Kikuu cha Gregoriana. Amefanya kazi katika baadhi ya ofisi mbalimbali za Roma kwa upande wa Taasisi ya Banki. Tangu 2000 ni profesa wa dini; na karibu miaka kumi hivi amejikitia kutoa semina kuhusu ukristo na historia katika Chuo Kikuu cha Laterano na Gregoriana Roma. Yuko katika orodha ya waandishi wa habari na anandika makala mbalimbali na kushirikiana na magazeti ya utamaduni, kati ya hayo Gazeti la Baraza la Maaskofu Italia, la Avvenire na Civilta Cattolica.

Tamko la Dk. Paolo Ruffini, kuhusu Bwana Andrea Tornielli  na Andrea Monda

Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vaticana Bwana Paolo Ruffini mara baada ya kutangazwa rasmi uteuzi viongozi wapya katika Baraza lake anasema: Kuchanguliwa kwa Andrea Tornielli Kama kuwa  mkurugenzi wa uhariri na  Andrea Monda  kuwa Mkurugenzi wa Gazeti la Osservatore Romano, ni hatua mbili muhimu katika mchakato wa mageuzi ya vyombo vya habari Vatican ambayo nimekabidhiwa miezi michache iliyopita na Baba Mtakatifu Francisko kama Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Dk. Paolo Ruffini anasema, kama alivyo sema Baba Mtakatifu Francisko kuwa hakuna haja ya kuwa na hofu ya neno mageuzi kwa maana magezi siyo mabadiliko kidogo ya mambo, bali ni njia mwafaka ya kuweza kuyapangalia kwa namna nyingine. Ni kuyapeleka katika mpangilio hadi kufikia katika umoja wa lugha zilizo nyingi na bila kupoteza lolote  maalum na historia zake. Hiyo ni kama vile ile  kazi ambayo wamekabidhiwa kila siku na ambayo inapatikana katika barua ya Mtakatifu Paulo kwa wakorinto; ni mwelekeo wa hali ya juu ambao wanafanya  kazi na ili wote waweze kuwa mafundi. Ni kazi ambayo inakuwa na maana, yenye mzizi na kiini chake katika utume wa kutangaza Neno. Kuna namna ya kufanya kazi ya huduma,  lakini Mungu ni mmoja anayewezesha kazi zote katika wote (1Kor 12,6). Kutokana na hilo Bwana Ruffini anathibitisha kuwa, ndiyo wajibu wa kuanzia hapo.

Andrea Tornielli na Andrea Monda

Akiendelea kutazama uteuzi mpya, Dk.Ruffini anasema: Andrea Tornielli na Andrea Monda wote ni waandishi wa habari na ambao wanatazama kwa kina mambo na wanatabia moja ya  kujikita kwa undani katika lugha nyingi ambazo ndizo zenye tabia ya wakati wetu, katika umoja wa mawazo na watu; wanatambua kutafakari kwa kina na wanatambua kusikiliza. Wote wawili zaidi ya kuwa wanahabari, pia ni watunzi wa vitabu. Wote wawili wanatambua kuzungumza na kizazi kipya kwa maana nyingine, kuzungumza na vijana na wote wawili ni wajenzi wa madaraja.

Maneno ya Dr. Andrea Tornielli  baada ya kuteuliwa

Ninamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa uchaguzi huu, ninamshukuru Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasilino Paolo Ruffini kwa kunifikiria. Vyombo vya habari Vatican vina historia ndefu; na inatosha kutaja umuhimu ambao umepatikana wa Radio Vatican katika hali nyingi za hivi karibuni au zaidi za nyakati zilizopita. Vyombo hivi vya habari vinaendelea kufikisha ujumbe wa Mfuasi  wa Petro na pia kutoa sauti kwa wale ambao hawana, na kwa sababu ya kutoa  kwa lugha nyingi, za kipekee duniani. Aidha anaongeza kuwa kutokana na hiyo:“Ninaamini kwamba kuna haja kubwa ya kuwa na  uandishi wa habari wa kusimulia  kabla ya kutoa maoni juu yake. Uandishi wa habari ambao katika wakati wa sasa unaweza kuchambua hali halisi ya  ukweli kwa kuzingatia kila mantiki zake zote”.

Aidha Dk. Tornelli amesema:“Nitajaribu kujikita katika huduma katika muundo wa habari uliooneeshwa na Vatican  na ujuzi wa uandishi wa habari pamoja na kiufundi ambao unaelekeza na kusaidia kuwasiliana, kwa njia zote na kutumia jukwaa zote, kwa njia rahisi na ya moja kwa moja, mafundisho ya Baba Mtakatifu kama yanavyojionesha katika mahubiri yake katika maadhimisho ya kila siku kwenye Kanisa la Mtakatifu marta , ambayo yanasindikiza watu wa Mungu katika kila kona ya dunia

Maneno ya Profesa Andrea Monda

Naye Pofesa Andrea Monda, Mkurugenzi Mpya wa Gazeti la Osservatore Romano anathibitisha: “Nimekuwa nikifanya uandishi wa habari kwa zaidi ya miaka thelathini na nimekuwa nikishughulikia  masuala ya kiutamaduni, kidini na ya kitaalimungu, na siyo kama kwa namna ya pekee kama kitaaluma kama vile wanavyoitwa ( wataalam wa mambo ya Vatican); lakini kwa hakika nisingeweza kufikiria kuitwa kuongoza katika hazeti la Vatican, Gazeti ambao kwa namna moja ni muhimu sana kama alivyolielezea Mtakatifu Paulo VI ( wakati wa fursa ya miaka 100 kunako  1961) kwamba  si kama  gazeti la mawazo ambalo linatoa habari tu; bali ni gazeti la kuujenga mawazo. Aidha ameongeza kusema amesema: “Inafungua sura ya mambo mapya kwa upande wangu na ninayo furaha kukabiliana pamoja na Mkurugenzi mpya wa Uhariri  AndreaTornielli, na wenzangu wote. Nitafanya sehemu yangu hadi mwisho ili kuendelea na kazi iliyofanywa na Profesa Vian na watangulizi wangu wote, nikiwa na uhakika wa kuweza kusema, hata kwa udogo wangu  kwamba: "Ninafarijiwa na ukweli kwamba Bwana anajua jinsi ya kufanya kazi na kutenda pia na vyombo vidhaifu”.

Shughuli na mwongozo wa Uhariri uliokabidhiwa kama Mkurugenzi Andrea Tornielli

Hata hivyo Kazi za na mwongozo wa Uhariri uliokabidhiwa kama Mkurugenzi Dk. Andrea Tornielli kwa misingi ya Kifungu cha ibara ya 9 ya Sheria ya Baraza la  Mawasiliano ni :1° Kuelekeza na kuratibu shughuli zote za uhariri katika uwezo wa Sekretarieti ya Mawasiliano; kuwa na 2°  maendeleo ya mkakati ya mfumo wa mawasiliano; kuwa na, 3° Ufungamani mwafaka wa vyombo vya habari vya kizamani na ulimwengu wa kidigitali, na hatimaye kuwa na tahadhari ya mara kwa mara kwa kiwango cha ulimwengu wa mawasiliano ya Vatican

18 December 2018, 16:08