Tafuta

Vatican News
Viongozi wa Kimataifa wanaomba waweke jitihada dhidi ya ongezeko la joto duniani, iliyoelekezwa na Papa Francisko katika Wosia wake wa Laudato Si Viongozi wa Kimataifa wanaomba waweke jitihada dhidi ya ongezeko la joto duniani, iliyoelekezwa na Papa Francisko katika Wosia wake wa Laudato Si 

Mabadiliko ya tabianchi:Jumuiya ya kimataifa iendeleze jitihada za Papa!

Kwa mujibu wa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican anasema,Jumuiya ya Kimataifa lazima iendeleze mbele jitihada dhidi ya ongezeko la joto duniani, iliyoelekezwa na Papa Francisko kuhusu Wosia wa Laudato Si

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumuiya ya Kimataifa lazima iendelee mbele katika jitihada dhidi ya ongezeko la joto duniani, iliyoelekezwa na Papa Francisko. Hayo ni maneno ya Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, katika Gazeti la Sir wakati akizungumzia juu ya uthibitisho wa Rais Donald Trump ambaye wakati wa mahojiano huko Washington, amesema kwamba ahamini hatari kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na binadamu na kwa maombi ya mwisho wanasayansi waliotoa ripoti kuhusiana na hatari ya kuongezeka kwa viwango vya joto duniani. Kutokana na hilo, Kardinali Parolin anaamini kuwa, Jumuiya ya kimataifa lazima endeleze mbele jitihada za Baba Mtakatifu Francisko kuhusu Wosia wa Laudato Si, ambao unaelekeza kwa dhati na ambapo aliweza kurudia kuzungumza tena katika mkutano aliofinyika mjiniVatican na wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao mjini Vatican. Katika kukusitiza alionesha wazi kwa maana mabadiliko ya tabia nchi ni hali halisi mbele ya kizazi hasa wale ambao wanateseka kwa hali hii na kizazi endelevu. Kardinali Parolin akihitimisha kwa mtazama wake anasema ni lazima kuendelezea jitihada hizo za Baba Mtakatifu.

Mkutano wa 24 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi

Katika mazungumzo ya Kardinali Pietro Parolin, yameangazia mkutano 24 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, (COP24), ambao utafanyika huko Katowice Poland kuanzia tarehe 2 hadi 14 Desemba 2018. Kufuatia na tukio hilo, naye Franz-Josef Overbeck wa Jimbo Katoliki la Essen, na  Rais wa Tume ya Kamati kuhusu masuala ya kijamii ya Baraza la Maaskofu Ujerumani amesema joto linaloendelea kuongezeka duniani, linawakilisha tishio kubwa kwa sayari yetu.  Amesema hayo wakati wa Mkutano huko Jimbo Kuu Katowice kabla ya kuanza kwa Mkutano kuhusu Tabia nchi (COP24).

Rais wa Tume ya Kamati kuhusu masauala ya kijamii akiendelea na hotuba yake anasema: “Ni lazima kusitisha mabadiliko ya hali ya hewa ambayo ni hatari, kabla ya kuchelewa na hakuna wakati zaidi”, kwa njia hiyo, anawashauri “viongozi wa nchi ili wajikite zaidi katika msimamo wa ustawi wa wote juu ya maslahi ya kitaifa na binafsi”. Aidha Askofu Franz-Josef ameongeza kusema kuwa, “Tunahitaji malengo ya hali ya hewa ambayo yanafaa kuaminika na yenye kusudi lililo wazi na kutekelezwa kwa njia thabiti. Ni muhimu wa haki kwa maskini wanaoishi duniani na vizazi vijavyo. Ulinzi wa tabia nchi ni kipaumbele na msingi wa kuhifadhi kazi ya uumbaji na njia ya maisha endelevu kwa wote”. Kadhalika amesema nchizote duniani zinapaswa kukuza na kuishi kwa haraka iwezekanavyo ule mfumo rafiki wa kuheshimu mazingira. Na hii ni kazi inayohusisha kila mtu. Kila mmoja wetu, tunaweza na tunapaswa kutoa mchango wetu kwa kutumia mtindo wa maisha yanayoheshimu mazingira, kwa njia ya kutunza na ubunifu endelevu, amesisistiza.

Matendo mema katika maparokia kwenye utetezi wa mazingira 

Hata hivyo hata Askofu Mkuu Ludwig Schick wa Jimbo Kuu Bamberga na Rais wa Tume ya Makanisa duniani katika Baraza la Maaskofu Ujerumani, wakati wa kutoa hotuba yake katika Mkutano huo amesema kuwa, kuna matendo mengi yaliyaonzishwa katika maparokia kuhusiana na utetezi wa mazingira, lakini inawezekana kutenda zaidi. Akitaka kusisitiza zaidi kwa kujikita juu ya maneno ya kazi ya mkutano huo ambao umeongozwa na mada; kutunza nyuma yetu ya pamoja: jitihada ya ekolojia kwa wakristo, Askofu Mkuu Schick amekumbusha hata amri kumi za mazingira ambazo maaskofu wa Ujerumani waliziweka ili zifuatw katika majimbo yao.

Amri kumi za utunzaji wa mazingira kwa mujibu wa maaskofu wa Ujerumani

Kati ya hizo amri  katika majimbo ya Ujerumani, zinawaalika kutoa nafasi ya kwanza katika  maadhimisho sala ya kuombea kazi ya uumbaji na kuwajibika juu ya uumbaji; kuhamasisha kozi za kusasisha uangalizi wa kazi ya uumbaji kwa wahudumu wa Kanisa na katika hali halisi ya mafunzo kuanzia shule za awali hadi vitivo vya kitaalimungu. Maaskofu wa Ujerumani zaidi ya hayo wanaaalika kujigundua upya katika kipindi cha Kaweresima kwa mtazano wa utetezi wa kazi ya uumbaji na kujikita katika mtindo wa maisha endelevu.

Kati ya mambo msingi kwenye amri kumi walizojiwekea, kuna hata  ule mfumo wa kuheshimu mazingira ndani ya majengo ya Kanisa na kusaidia huduma ya ekolojia na mwisho ili kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa. Shughuli ya maaskofu wa Ujerumani katika jitihada ya utetezi wa mazingira ni ile ambayo pia inahitaji jitihada za kisiasa kwa maana kuu zaidi,ili kuweza kuwa mashuhuda halisi na wanaoaminika wa kulinda na kutetea mazingira katika maisha ya kila siku pamoja na matukio ya umma na matukio ya kitamaduni.

01 December 2018, 15:33