Cerca

Vatican News
Mfumo mpya wa umeme kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kuzinduliwa rasmi tarehe 25 Januari 2019 Mfumo mpya wa umeme kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kuzinduliwa rasmi tarehe 25 Januari 2019. 

Mfumo mpya wa umeme Kanisa kuu la Mt. Petro kuzinduliwa Januari

Ukarabati wa mfumo mpya wa umeme kwenye Kanisa kuu umetekelezwa kwa muda wa miaka miwili, kazi ambayo imefanywa na Kampuni ya OSRAM kutoka Ujerumani kwa kushirikiana na mafundi kutoka Vatican. Mfumo mpya wa taa umewekwa kwa kuzingatia vigezo vya utunzaji bora wa mazingira, changamoto endelevu na fungamani inayotolewa na Baba Mtakatifu Francisko.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 24 Desemba 2018 ameadhimisha Mkesha wa Noeli kwa kutumia mwanga wa taa mpya zilizofungwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Ukarabati wa mfumo mpya wa umeme kwenye Kanisa kuu umetekelezwa kwa muda wa miaka miwili, kazi ambayo imefanywa na Kampuni ya OSRAM kutoka Ujerumani kwa kushirikiana na mafundi kutoka Vatican. Mfumo mpya wa taa umewekwa kwa kuzingatia vigezo vya utunzaji bora wa mazingira, changamoto endelevu na fungamani inayotolewa na Baba Mtakatifu Francisko, kiasi kwamba, mfumo huu mpya utaokoa kiasi cha asilimia 90 ya nguvu ya umeme iliyokuwa inatumika hapo awali.

Mfumo mpya wa mwanga kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican unatarajiwa kuzinduliwa rasmi hapo tarehe 25 Januari 2019 wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo, Mwalimu na Mtume wa Mataifa. Kwa waamini waliohudhuria Ibada ya Mkesha wa Noeli, wameshuhudia matendo makuu ya Mungu katika maisha ya mwanadamu na jinsi ambavyo teknolojia rafiki inavyoweza kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kubana matumizi!

Mfumo wa Taa Kanisani

 

27 December 2018, 09:42