Cerca

Vatican News
Watu wengi duniani wanakabiliwa na biashara mbaya ya utumwa Watu wengi duniani wanakabiliwa na biashara mbaya ya utumwa  

Vatican: milioni 40 ya watu wako katika mtego wa utumwa!

Askofu Mkuu Bernardito Auzi mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, ametoa wito kuwa ni kipindi sasa cha kuondoa kila aina ya mzizi wa biashara ya binadamu kwani ni zaidi ya watu milioni 40 wako katika mitego hiyo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kanisa liko mstari wa mbele katika masuala ya kulinda waathirika wa biashara haramu ya binadamu na utumwa. Ni lazima serikali zitende kazi kwa ujasiri ili kuondoa mizizi ya tukio hilo baya. Ndiyo msisitizo wa Askofu Mkuu Bernadito Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York wakati wa hotuba yake kwenye mkutano kuhusu suala la kusitisha biashara haramu ya binadamu mjini New York. Askofu Mkuu ahimiza Jumuiya ya kimataifa kutosimamia tu juu matokeo ya biashara hiyo, badala yake wagundue zaidi mizizi inayosababisha, hata katika mifumo ya kiuchumi.

Askofu Mkuu katika hotuba yake anasema, leo hii  kuna zaidi ya milioni 40  ya watu katika mitego ya mitindo  ya utumwa, licha ya  kwamba kuna maendeleo yaliofikiwa kwa miaka kumi hivi, kwa namna ya pekee  ya Protokali zilizowekwa huko Palermo Italia, na Mpango wa dunia kuhusu Matendo ya Umoja wa mataifa wa kuthibiti hal ya biashara haramu ya binadamu.

Si kwa nadharia, bali matendo ya dhati

Askofu Mkuu Auza pia akikumbusha maneno ya Papa Francisko katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa, mwezi Septemba 2015,amethibitisha kuwa juhudi za kweli haziwezi kutosha tena, iwapo hakuna kuongeza jitihada za  mapambano dhidi ya janga baya hili la biashara ya binadamu ambayo inazaa mabaya mengine kama vile mifumo ya utumwa mamboleo, utalii wa ngono na biashara haramu ya viungo vya binadamu na manyanyaso ya kijinsia kwa watoto. Kwa njia hiyo Askofu Mkuu ameonesha mambo msingi ya dhati ambayo yanaweza kusaidia kusitisha hali mbaya hiyo kwamba ni kuzuia biashara, kulinda waathirika, kuwashitaki wahalifu na kuhamasishwa mashirika na wadau, na kati yake ni taasisi mbalimbali na vyama vya kiraia vinavyopambana na janga hilo.

Juhudi ya  watawa kwa njia ya mtandao wa Talitha kum

Hata hivyo Askofu Mkuu Auza amesisitiza juu ya uzoefu wa mtandao wa Talitha Kum ambao unaunganisha taasisi 22 katoliki katika nchi 70 duniani, ambazo ziko mstari wa mbele katika mapambano ya biashara ya utumwa. Na kati ya mashirika hayo amekumbusha juhudi za kikundi cha Mtakatifu Marta ambacho kinahamasishwa na Kanisa na kuweka pamoja vingozi wa dini na wakuu ngazi za viongozi wa polisi kuandaa kwa pamoja,Taasisi na mashirikia pamoja ya kidini ili kukabiliana na suala hili sugu la biashara ya binadamu na msaada wa kwa waathirika. Anasema, “ tunahitaji msaada kwa kuamka wote kila mmoja kwa upande wake ili kwa pamoja kukabiliana janga hili uso kwa uso” !

10 November 2018, 14:44