Tafuta

Vatican News
Ziara ya kichungaji ya Kardinali Filoni nchini Angola Ziara ya kichungaji ya Kardinali Filoni nchini Angola 

Kard. Filoni:karama za mashirika ni kuziishi kwa matendo ya dhati!

“Kuweni na ukomavu wa kiroho na kimaadili ili muweze kuwa wanaume na wanawake wa Mungu, wenye ukuu wa kimaadili, tayari kuuishi ule useja wa kidini kwa hali ya kujitoa binafsi kwa Mungu na kwa Kanisa”.Ni wito wa Kardinali Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la Unjilishaji wa watu, kwa manovisi na waseminari nchini Angola

Sr. Angela Rwezauala - Vatican

Kardinali Ferdinando Filoni, Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, akiwa katika ziara yake ya kichungaji, kuitembelea nchi ya Angola hasa katika Kanisa Katoliki la Angola ambao wanaadhimisha miaka 50 tangu kuanza kwa Baraza  Maaskofu Kaliki, tarehe 15 Novemba 2018, amekutana na manovisi, wa kike na kiume na walimu wao wa Kanda ya Kanisa huko Lubango. Katika hotuba yake ameelezea juu ya umuhimu wa kipindi cha mafunzo ambayo wanafanya uzoefu,na kuwahimiza juu ya wajibu  wao wanaopaswa kuwa nao, na kwamba si tu wa kujua karama na tabia ya familia ya mashirika yao, lakini cha zaidi  ni kutambua kuishi kwa kina na kwa upendo karama hiyo.

Maisha yakijumuiya, mahalia ni mwafaka wa mafunzo kwani ni kuufunza kuka na kuishi kindugu

Akiendelea na ufafuzi juu ya mantiki kwa kina  hasa ili ya kipaumbele cha mafunzo ya hawali kwa vijana hao, amewataka wajipyaishe katika zawadi ya Mungu ambayo imo ndano mwao ( 2Tm 1,6) na kuwahimiza wajikite zaidi katika kukomaa kibinadamu na kiroho na ili waweze kuwa wanaume na wanawake wa Mungu na wenye ukuu wa kimaadili, tayari kuuishi ule useja wa kidiini kama hali ya kujitoa binafsi kwa Mungu na kwa ajili ya Kanisa. Kardinali Filoni pia amesisitiza juu ya maisha ya kijumuiya, mahalia ambapo ni mwafaka wa mafunzo na mahali ambapo kila mmoja anajifunza kuishi kindugu na wale ambao Mungu aliweka kuwa karibu na kwa kukubali tabia zao chanya lakini pamoja ule utofauti na vikwazo na udhaifu wa kila mtu.

Mafunzo lazima yapelekwe katika umisionari kwa mujibu wa Papa Francisko

Kardinali Filoni, akikimbusha hotuba mbalimbali za Papa Francisko, kuhusiana na ulazima wa matendo hai ya kimisionari, anasema katika maono ya Papa anasisitza zaidi juu ya Kanisa ambalo linapaswa kutoka njia kwenda kukutana na uhai wa dhana mbalimbali ua kijamii na kikanisa. Kutokana na hilo, ni lazima kuiga ule mtindo mpya wa roho ya kimisionari ili kuweza kushikishana furaha ya Injili. Mfuasi wa Kristo ni lazima awe mmisionari wa kweli ambaye anapenda mwalimu wake kwa upendo upeo na kwa kina katika mahusiano na watu wa Mungu ambao amepewa.

Akiwageukia walimu wa manovizi wa mashirika mbalimbali ya dini, Kardinali  pia amewaambia kuwa tendo mafunzo ni kazi ngumu,muhimu na nyeti ambayo inapaswa ijikite kwa dhati na uwajibikaji. Hiyo pia anasisitiza ni kutokana na matokoeo yake ya wakati endelevu wa Kanisa mahalia na ulimwengu. Kwa kutoa mifano amesema na hili ni jukumu kubwa kutokana na inavyoonesha matatizo ya sasa ambayo yanatoa majeraha ya Kanisa na kwa maana hiyo maisha ya makuhani na watawa, lazima yake na msingi wa dhati , unaojikita juu ya ukomavu kibinadamu na kiroho.

Hata hivyo ameendelea kuelezea kwa dhati juu ya kazi za walimu wa manovi alizobainisha kuwa, kwanza ni ile ya kuwasaidia vijana wafanye mang’amuzi mema na kujikita kwa dhati katika ushaguzi wa makandidate wa shirika au wakati wa kufunga nadhiri za dini. Kwa maana hiyo wahudumu katika kitengo nyeti cha mafunzo lazima wawe na ujuzi na na utaalamu wa kweli wa kibinadamu, kimaadili na kiroho na lazima wawe mfano hai kwa vijana.

Waseminari wajifunze vema kitaalimungu na kiutamaduni ili baadaye waweze kuwa wafuasi wa kimisionari

Na katika Seminari ya Jau, mchana tarehe 15 Novemba, amekutana na Waseminari wanaojifunza Taalimungu na Falasafa wa majimbo ya Angola ambao wanasoma huko  Lubango. Kardinali amewapatia salam na Baraka kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko na kuwashauri waseminari hao, juu ya  uwajibu kwa ukarimu na uaminifu wa wito wa Bwana na matarajio ya watu wa Mungu kwa kujiandaa vema katika utume ambao unatokana na msingi wa mafunzo, kwanza ya kibinadamu, kiroho, kitaalimungu na kiutamaduni ili badaye waweze kuwa wafuasi wa kimisionari ambao daima wanayo shauku ya Yesu na katika utume wake!

Katika hotuba yake, Kardinali ameendelea kujikita kwa dhati kwa kutazama kipindi mwafaka cha maandalizi ya kuwa padre yaani kuwa watu wa Yesu Kristo na kusema kuwa: Padre lazima awe wa dhati,  mfuasi na mmisionari ambaye siyo mtu wa malipo; ya kuishi vizuri katika utajiri na wala kuwa mfanyakazi wa mambo matakatifu au  kuwa na tabia za ukuhani ukuhani ,lakini zaidi, awe padre anayetoka nje , kwanza kusikiliza Kristo ili aweze kupeleka furaha ya Injili kwa maskini na wale wote atakaokutana nao. Amewashauri waseminari  wote kwa wosia huu: “muwe wafuasi wakimisionari na msiwe na hofu ya kujiandaa kuwa mapadre na mitume wamisionari”. Mwisho wa mkutano huo,ameadhimisha misa na waseminari pamoja na walimu wao.

Kukutana na kuongozi wa serikali huko Lubango na vyama vya kitume katoliki

Hata hivyo mara baada ya kumtembelea kiongozi wa serikalia katika  eneo Lubango, asubuhi, pia Kardinali Filoni amekutana na wajumbe wa vyama katoliki vya kitume na mashirika  mbalimbali ya walei katika Parokia ya Lage huko Lubango. Akijikita katuka moja ya wito wa hitimisho la Konagamo la Walei Katolini nchini Angola, Kardinali Filoni amewaomba walei wa Angola wawe wamisionari, kwa maana ni kwa njia ya ubatizo, kila mkristo anao wajibu wa kujibu wito wake kwa Yesu ambaye anawaelekeza wote wawe wamisionari. Hiyo ni kuwataka watu walei wakumbuke vema wito wao maalum na  ili kuweza kuutafuta  kwanza Ufalme wa Mungu pamoja na kujikita katika shughuli za mambo yao ya wakati, wakati huo huo wakijibu na kufanya mapenzi ya Mungu. Kardinali Filini anasisitiza kwamba: “ Ni kweli kwamba Askofu ndiyo mwajibikaji wa kwanza katika uinjilishaji, kushirikishana na mapadre na watawa, lakini pia hata mwili wa Kristo, wa Kanisa  na  wa kila mbatizwa, amepokea kutoka kwa Mungi wito  binafsi wa kushuhudia Injili kila wakati na kipindi muda wote!

Vile vile Kardinali, mara baada ya kukumbusha juu ya Mwezi wa Kimisionari Maalum wa mwezi Oktoba 2019, na lengo lake, amesisitizia juu ya hali halisi ya mahalia ya nchi  kwa maneno haya: “ inaonesha kwa dhati ushirikiano wa walei na wachungaji wake, unachangia kufanya Kanisa la Angola kuwa hai. Uhai huo unajionesha kwa njia ya ushiriki hai wa imani ya waamini katika maadhimisho ya liturujia mbalimbali na shughuli za kikanisa na kijamii. Kuna uhai mkubwa wa uchanuzi wa mashirika na vyama vingi vya kilei. Ninashangaa kwa namna ya pekee nafasi ya makatekista katika uinjilishi na katika utume wa kichungaji wa parokia. Zaidi Kanisa linajivunia kwa namna ya pekee juu ya mahusano mema katika nchi kwa maana ya Kanisa linaheshimwa na yote hayo shukrani kwa  matokeo ya jitahada zenu za kila siku!

Changamoto:kuondoa mizizi ya ukabilia, ushirikina na kuyumba kwa imani

Hata hivyo  pamojana sifa alizoziotoa za Kanisa la Angola, katika hotuba yake, kwa walei, Kardinali Filoni hakunasahu, kukumbusha juu ya baadhi ya changomto zilizo mbele ya kanisa la Angola kwa upande wa kambi ya kijamii na Kikanisa, ambazo zimeweza kuwekwa bayana katika hitimisho la Kongamono la Walei, wakiwa katika maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanza kwa Baraza la Maaskofu Katoliki mahalia.

Kutokana na hizo, Kardinali Filoni anasisitiza kwamba changamoto hizo zinahitahiji msaada mkubwa ambao utatokana na mchango wa wote na ili kuweza kupata ufumbuzi wake. Katika changamoto hizo kwanza ni uinjilishaji katika utamaduni, ili kuweza kuondoa kila aina ya mizizi inayotanda ya miganyiko ya ukabila na ambayo ni moja ya hatari ya maisha ya jumuiya. Kadhalika changamoto ya kuhamahama Kanisa moja na nyingine na mabyo amesema inaleta huzuni, kuona ukosefu au kuyuymba wa imani ya kina kwa baadhi ya wakristo. Kadhalika na changamoto nyingine nyingi zinazojitkeza katika maisha ya uinjilishaji, na amapo amebainisha kuwa yote hayo ni dharura ya kupambana na tabia hizo zilizo kinyume na Roho ya Injili. Na hatimaye amehimiza kwamba kuna ulazima wa dhati wa mafunzo kamili yanayofaa.

 

 

16 November 2018, 16:06