Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteua Askofu Philip Srnold Subira Anyolo kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Kisumu, Kenya. Papa Francisko amemteua Askofu Philip Srnold Subira Anyolo kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Kisumu, Kenya. 

Askofu Philip Anyolo ateuliwa kuwa Askofu mkuu, Jimbo Kuu la Kisumu, Kenya

Askofu mkuu mteule Philip Arnold Subira Anyolo alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Homa Bay na pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, msimamizi mkuu wa Sekretarieti, msemaji mkuu na mwakilishi mkuu wa Baraza ndani na nje ya Kenya.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Zacchaeus Okoth wa Jimbo kuu Katoliki la Kisumu, Kenya. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Philip Arnold Subira Anyolo kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Kisumu. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu mteule Philip Arnold Subira Anyolo alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Homa Bay na pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, msimamizi mkuu wa Sekretarieti, msemaji mkuu na mwakilishi mkuu wa Baraza ndani na nje ya Kenya.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Philip Arnold Subira Anyolo alizaliwa tarehe 18 Mei 1956 huko Tongareni. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, hapo tarehe 15 Oktoba 1983 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mtakatifu Yohane Paulo II, tarehe 6 Desemba 1995 akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kericho na kuwekwa wakfu tarehe 3 Februari 1996. Papa Yohane Paulo II kunako tarehe 22 Machi 2003 akamteuwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Homa Bay na kusimikwa rasmi tarehe 23 Mei 2003. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 15 Novemba 2018 akamteuwa kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo Katoliki la Kisumu, Kenya.

Kisumu, Kenya
15 November 2018, 11:31