Cerca

Vatican News
Waamini wa Kibudha katika utamaduni wa sala Waamini wa Kibudha katika utamaduni wa sala 

Taiwan:Tujenge madaraja ya kuunganisha tasaufi za kidini

Hivi karibuni umefanyika Mkutano wa kwanza kimataifa wa watawa wa kibudha na kikristo kwa ajili ya mazungumzo ya kidini. Mwisho wa mkutano huo wametoa hati yao ya pamoja kuthibitisha majukumu wanayopaswa kuendeleza katika tasaufi za dini licha ya utofauti wao

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

 “Watawa wa kibudha na wakristo katika mazungumzo: lugha yetu ni upendo”, ndiyo kauli mbiu ya hati yao ya pamoja ya mwisho mara baada ya Mkutano wao wa kwanza wa mazungumzo ya kidini kimataifa kati ya watawa wa kibudha na kikristo uliofanyika huko Kaohsiung nchini Taiwan. Waliohamasisha Mkutano huo ni Baraza la Kipapa la mazungumzo ya kidini ambao wametoa taarifa hiyo kwa ushirikiano wa Chama cha Wakuu wa Mashirika ya Kidini nchini Taiwan kwa kuongozwa na Mada ya  Matendo hai ya kusali na kutafakari: watawa wa kibudha na wakristo katika mazungumzo.

Mkutano wa hivi karibuni huko Taiwan umefanyika katika Monasteri ya kibudha ya Fao Guang Shan huko Kaohsiung, ikiwa ni Mkutano wa kwanza kimataifa wa watawa 70 kutoka nchi ya Taiwan Korea, Japan India, Sri Lanka, Myanmar, Thailand, Singapore, Hong Kong, Cambodia, Ufilippini, Brazil, Italia, Ujerumani, Norway na Marekani. Aidha kulikuwapo na washiriki wa Baraza la Makanisa Duniani na  Hsin Bao, ambaye ni abate wa Monasteri ya  wabudha ya Fo Guang Shan, aliwakaribisha washiriki wote wakati wa  hotuba ya ufunguzi, ambayo ilitolewa na Askofu Miguel Ángel Ayuso Guixot, Katibu wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini.

Kujenga madaraja ya kuunganisha michakato mbalimbali ya kitasaufi

Waakati wa kuhitimisha mkutano wao, umeona matunda ya kazi, kwa washiriki ambao wamependa kutoa hati ya kutambuliwa katika Mkutano huo wa kwanza wa mazungumoz kimataifa kwa ajili ya watawa wa kibudha na kikrito. Hati hiyo ina jikita hasa katika kuhamasisha uwelewa wa pamoja na urafiki kati ya watawa wote, ili kujenga madaraja yanayo unganisha michakato yao ya kitasaufi tofauti.

Hati hiyo inasema inathibitisha kuwa: “Watawa wa kike wanatambua kwamba kwa pamoja na uimara wao kulingana  na ukweli wa kina kwamba, inawezekana kujifunza kutoka kwa wengine, na kama kujitajirisha, kiutamaduni na kijamii ili kwa  unyenyekevu na kuaminiana kama ndugu na  kaka na dada.

Mazungumzo ya kidini ni mchakato wa kufanya kwa pamoja

 Aidha Hati yao inasema kuwa, wao wanaamini kwamba katika ushuhuda wa mtindo wa maisha, unaweza kuwa na maana na furaha katika  kuondokana na utumiaji hovyo  wa mali na ubinafsi, na wanaweza kuwaambukiza wengine ili kutembea pamoja katika njia ya wema. Na zaidi watawa wanasisitiza umuhimu wa kuonesha huruma na upendo, na kupeleka matumaini kwa kila yoyote mwenye kuhitaji. Wanathibitisha pia kuamini kuwa mazungumzo ya kidini ndiyo kweli  safari ya wanaume na wanawake wambao wanapaswa kutembea katika njia moja. Na kutokana na hilo, wanawatia moyo watawa daima ili waendelee kutoa mchango wao wa dhati kama wanawake katika kujenga mahusiano mema, mapya na  ubunifu wa mtindo wa mazungumzo kati ya dini na kujifungua wazi  katika jumuiya zao ili waweze kweli kufikia malengo ya dhati katika mchango wao.

Kutambua kwa pamoja, ni utajiri  na wema wa pamoja  katika dunia

Vilevile watawa wanahisi ulazima wa kusaidia wanafunzi, walimu, watoto ili waweze kuwa mabalozi wa amani na umoja, ili kuwaali binadamu wote kutembea katika njia ya kuheshimu mazingira na kutotumia vurugu. “Tunatambua kuwa upendo ndiyo lugha ya pamoja, ambayo inatutaka kwenda zaidi ya mawazo yetu na hisia zetu binafsi na kukumbatia mwingine, licha ya utofauti ambao upo kati yetu”. Kadhalika wanathibitisha: “Tunahisi kuwa karibu na wengine, tunapounganisha mioyo na akili wakati wa kutembea kwa pamoja kulingana na michakato ya kitasaufi na hivyo tunaona ulazima wa kuendelea na umoja huo kwa ajili ya kutajirishana pamoja, ili kuboresha dunia yetu!

Shukrani kubwa kwa matokeo mazuri ya mkutano

Mwisho washiriki wote hao, wanatoa shukrani kubwa kwa wandaaji, walioweza kutengeneza hali halisi nzuri ya kupendeza na ukarimu wa kweli na urafiki ambao umekuwa na tabia ile ya mazungumzo. Wanawashukuru hata viongozi wa raia. Monasteri ya Wabudha wa Fo Guang Shan, Kanisa Katoliki mahalia na Chuo Kikuu cha Orsoline, kwa ajili ya ukarimu wa msaada mkubwa uliowawezesha kufanikisha Mkutano wap wa kwanza wa kimataifa kati ya watawa wa Kibudha na wakristo pamoja!

 

 

 

 

25 October 2018, 13:03