Tafuta

Vatican News
Sinodi ya Maaskofo Vatican Sinodi ya Maaskofo Vatican 

Sinodi:Kanisa na familia kufanya agano ili kuwasindiza vijana!

Kazi inayoendela ya Sinodi juu ya vijana: Asubuhi ikiwa ni sehemu ya nne ya Mkutano. Hotuba 20 za Mababa wa Sinodi kuhusu sehemu ya kwanza ya kitenda Kazi Instrumentum Laboris. Nafasi ya wasikilizaji 8 kama wawakilishi maalum wameweza kuzungumza

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Nafasi ya wasikilizaji 8 maalum wa Sinodi wameweza kusikilizwa na kwa maana hiyo : Wengi leo hii wanazungumzia juu ya vijana, lakini siyo wengi wanazungumza na vijana. Aliyathibitisha hayo Paulo VI ambaye atatangazwa Mtakatifu na anarudia leo hii kuzungumza katika Sinodi.

Mada ya kusikiliza imerudi tena katika Sinodi ya Maaskofu inayoendelea ikijikita katika mitindo tofauti ambapo Ijumaa 5 Okotaba asubuhi ilikuwa ni usikivu wa mkao wa nne: kuna ulazima wa kusikiliza vijana katika ulimwengu wa dijitali mahali ambapo mitandao ya kijamii mara nyingi inakuwa ni ugonjwa wa ndoto, na hatari ya kuwafanya vijana wanenepe na habari nyingi. Lakini pia kuna haja ya kutazama uso chanya kwa vijana ambao ni wachukuzi wa rasilimali ya binadamu na tasaufi ambayo ni urafiki, mshikamano, kujitolea, ushuhuda wa dhati, maombi ya kweli yanayoelekezwa katika jamii ya raia na wito kwa Kanisa kuwa na furaha zaidi ya kiinjili.

Inahitajika makabiliano ya ujenzi wa watu wazima

Vijana watafute kusiliza watu wazima na ambao wanajitoa kwa muda wao, kupokea kwa ukarimu na kuheshimu, wasihukumiwe bali kusindikizwa katika mang’amuzi hata ya miito. Kuna ulazima tena na mkubwa leo hii unaotazamwa katika tabia ya baadhi ya wazima ambao ni vijana, tabia ile ya kutotoa mwelekezo wa vijana, na kuwakosesha kituo msingi cha kukimbilia.

Umuhimu wa liturujia na sakramenti

Mababa wa sinodi wamekumbuka pia umuhimu wa kuhamasisha kwa upya Misa na sala za kila siku, sakramenti ambazo ziwakilishe kwa namna ya kuwavutia vijana na kuwafanya wawe hai katika maisha ya Kanisa na kukuza kipaumbele kwao. Katika maadhimisho ya liturujia, umakini uwepo hasa katika matumizi ya vyombo vya muziki, na kama ilivyo hata kwa upande wa katekesi na mahubiri.  Haitoshi kuwa na kumbukumbu za sala na taratibu za kawaida, bali, sinodi inasema, inahitajika mahubiri ya furaha ambayo yana uhai, ili vijana waweze kutambua katika vichwa vyao na kuamini kwa moyo. Ni kwa namna hiyo, inawezekana kuwa kama mitume wa kwanza katika rika lao. Wadau wa mabadiliko, wajenzi wa amani, umoja katika dunia, vijana ambao wanafikiriwa mahali pa kitaamungu na ambalo Kanisa linawatamani.

05 October 2018, 15:53