Tafuta

Vatican News
Papa ameshiriki Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na wanahija mababa wa Sinodi na washiriki, katika kaburi la Mtakatifu Petro Papa ameshiriki Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na wanahija mababa wa Sinodi na washiriki, katika kaburi la Mtakatifu Petro  (Vatican Media)

Papa ameshiriki Misa ya wanahija wa Sinodi katika kaburi la mt. Petro

Petro alikuwa amevua samaki usiku kucha, lakini hakupata chochcote. Yesu akamkaribia na kumwambia atupe jarifa. Ni sehemu ya mahubiri ya Askofu mkuu Rino Fischella Rais wa Baraza la Kipapa la Ujilishaji mpya, wakati wa misa ya Hija ya mababa na washiriki wa Sinodi kwa ushiriki katika misa hiyo Papa Francisko

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 25 Oktoba 2018, imefanyika Hija ya vijana na Mababa wa Sinodi kuanzia saa 2.30 asubuhi kwa kutembea 6 km, katika njia ya Francigena, iliyo anzia katika uwanja wa Montemario kwenye kituo cha Padre Orione Roma, hadi kufika uwanja wa Mtakatifu Petro saa 5.30 asubuhi masaa ya Ulaya. Hija hiyo imehitimishwa na maadhimisho ya Ekaristi Takatifu katika kaburi la Mtakatifu Petro mjini Vatican saa 6.00 kamili masaa ya Ulaya ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Tukio hilo limeandaliwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji mpya.

Waliodhuria hija hiyo, karibia mababa 300 wa Sinodi, wasikilizaji na vijana wengine kutoka katika maparokia ya mji wa Roma. Njia ya hija hiyo imeandaliwa vituo vitatu ili kuwapa muda wa sala na tafakari na kituo cha mwisho kilikuwa katika kaburi la Mtakatifu Petro kwa kushiriki Misa Takatifu ambayo iliyoongozwa  na Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu  na  ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko. Mahubiri yametolewa na Askofu Mkuu  Rino Fischella Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji mpya.

Mahubiri ya Askofu Mkuu Rino Fischella yameanza kwa kusema, “Baba Mtakatifu, kaka na dada, tumemalizia hija yetu katika kaburi la Mtakatifu Petro, hata kwa mwanga wa Neno la Mungu tumesikia na tunashauku sasa ya kupokea maana ya kile ambacho tumetimiza”. Akiendelea amesema, wapo wanaadhimisha pamoja Sinodi ya vijana; na wamesadiki imani yao na sasa ni kutaka kupokea kwa ajili ya maisha yao maana ya Petro, maisha yake na wito wake.

Katika Kanisa la Mtakatifu Petro kila kitu kinazungumza Petro na kuonesha kwao jinsi gani ya kuishi maisha ya kikristo. Wamesikia Katika somo  la Injili ya kwamba, Petro ulipokuwa kijana alikuwa anakwenda mahali popote anapotaka na kujitosheleza,lakini anaongeza kusema Askofu Mkuu Fischella ya kuwa, ndiyo hicho hata kwa wote wanashauku, hasa nyakati hizi. Japokuwa ijili inasema: “kipindi kingine kitafika na utapelekwa mahali ambapo hutaki”. Ili kuweza kutambua maneno hayo ya Yesu kwa Petro, ni lazima kutambua ni kitu gani kilikuwa kumetokea katika miaka ya kwanza anathibitisha Askofu Mkuu Fischella na hivyo anasema, “Mtakatifu Luka anatafsiri katika sura ya tano ya Injili yake na kuelezea juu ya wito wake”. Petro alikuwa amevua samaki usiku kucha, lakini hakuwa amepata chochote. Yesu akamkaribia na kumwambia atupe jarifa. Petro hakuwa anamtambua Yesu lakini kwa hakika alimpenda mara katika kukutana kwa mara ya  kwanza na Yeye. 

Swali la kujiuliza Kardinali anasema, “Lakini ni jinsi gani huyo kijana amweleze yeye ambaye mvuvi wa samaki na utaalam wake atupe jarifa? Na isitoshe yeye “alikuwa amevua usiku wote, lakini hakupata chchote… Petro alikuwa amechoka na kukata tamaa”. Lakini hakumwambia Yesu: “Fikiria kufanya uselemala mimini mvuvi”. Hakujibu hivyo. Badalka yake Petro alisema: “Lakini kwa kuwa umesema nitatupa wavu”. Katika neno lako, ninajikabidhi kwako. Hiyo ni imani ambayo Petro anamwonesha Yesu hata kama alikuwa hajawahi kumwona kwanza, hata kumjua. Na hapo ndipo anaanza kupata mafundisho ya kwanza yale ambayo Mwinjili Yohane baadaye atatueleza katika sura ya 15 ya Injili yake na kusema: “Bila mimi hamwezi kufanya lolote”. Anayekaa nami, atazaa matunda mengi”. Petro kwa taratibu anatambua na  kumwamini kwa maana anahitaji neema ya Mungu.

Askofu Mkuu Fischella anathibitisha hiyi ina maana kuwa: “Bila Yeye hatuwezi kufanya lolote, na tunarudia maneno haya mara nyingi tunaposali sala ya Rho Mtakatifu, bila uwepo wake, bila mwanga wake, hakuna lolote ndani mwetu. Pamoja na hayo, baada ya Petro kuona kwamba kutegemea Yesu ni kuzaa matunda, uvuvi wake ulienda vizuri na baada ya kutambua zaidi na zaidi kuwa ni Yeye, alimwambia, “kaa mbali nami , kwa maana mimi mdhambi”. Kuwa mbali nami Yesu kwa maana sistahili kukaa karibu nawe. Lakini Yesu anao mpango mwingine juu yake, maana alimjibu: “Petro usiogope”. “Petro usiwe na hofu, maana nitakufanya uwe mvuvi wa watu”. Usiogope Petro endelea kunitumainia; endelea kuwa karibu nami, na usiniache.

Katika kugundua Petro ni nani, ni mkarimu

Askofu Mkuu Rino Fischella ameendelea kufafanua  zaidi sura ya Petro kwamba: “Tunagundua Petro kuwa mwenye tabia ya ukarimu kama ilivyo tabia ya vijana wetu”. Ukarimu huo unajionesha katika kukimbia kwa haraka; kuwa na mshikamano mahali penye mahitaji… Petro ni mtu mkarimu! Petro aliacha yote na kumfuata Yesu. Hashutuki,, hana wasiwasi kwa ajili Yake. Anaacha yote na kumfuata Mwalimu. Kadhalika , ukarimu wake huo unapatikana katika kipindi chote cha miaka mitatu ya utume wa Yesu Duniani. Alipanda mlima Tabor na Yesu, mahali aliposikika akitamka  maneno: “ ni vema kukaa hapa!  Katika kukiri kwa mara ya kwanza Imani yake akimwambia: “Wewe ni Kristo”. Yeye yupo na Yesu katika shamba la mizeituni, na anamkata sikio mtumwa wa kuhani mkuuu na alikuwa anaitwa Malko, wakati huo Yesu anamwambia Petro, rudisha upanga alani mwake; kwani haiwezekani kulipiza  kwa vurugu”. Petro hatua kwa hatua anapaswa kutambua kuwa yeye hawezi kujiokoabinafsi bali ni Yesu, ni Mungu anayeokoa.

Wito wa Petro ni kuwa mvuvi wa watu

Askofu Mkuu Fischella  akielezea juu ya wito wa kwanza wa Petro anasema ; ni ule ambao unasikika katika sura ya 21 ya Injili ya Mtakatifu Yohane iliyosomwa katika fursa hiyo Injili inaonesha jinsi gani uvuvi  haikufanikiwa kwa sababu siku ile hawakupata chochote. Hapa Yesu anafika na wito wake, “tupa jarifa”. Katika sehemu hiyo inaonesha wazi utii wa Petro, kwa maana katika kutupa nyavu zao, wanapata samaki wengi. Yohane ambaye alikuwa ni mpendwa na aliye mtambua haraka anasema, ni Bwana! Hapo ndipo kuna utofauti uliopo kati ya siku ile walipokimbia kwenda kaburini, upendo unafika daima wa kwanza. Lakini hapo ni kuonesha kuwa Petro alikuwa tayari amebeba majukumu, hivyo yeye anakwenda taratibu katika safari. Upendo unatambua, upendo unafika mara na kuifikia haraka kaburi. Yohane alisimama akisubiri Petro na kwa mara hiyo Petro alifika haraka!

Ni Bwana na Yeye alikwenda

“Ni Bwana na yeye akaenda”. Ni mazungumzo mazuri sana, anathibitisha Askofu Mkuu Fisichella. Hiyo ni kuona kuwa, Yesu hakusema Petro kwanini ulinisaliti? Lakini  kama angekuwa mimi ningefanya hivyo,“kwanini ulinisaliti? Kardinali amekiri,  badala yake Yesu anatufundisha kwamba,  ukiwa na Yeye unafikiri kwa namna nyingine! Na ndiyo maana hapo kuna mchezo wa maneno mawili ambayo ni muhimu, yasemayo: Petro je unani penda mimi? na Petro anajibu: ninakujali. Petro unanipenda? – (agapao) yaani unao uwezo wa kutoa maisha yako yote? Lakini yeye anajibu, “Yesu ninakutakia mema”. Na kwa mara ya Tatu, Yesu hasemi tena, “ unanipenda, kwa sababu anatambua kuwa Petro, bado hana uwezo, na hivyo bado anapaswa kuwa na uvumilivu na ndipo anashuka katika uwezo wake na kusema “Petro unanitakia mema?  Na hiyo inampa faraja Petro na kujibu kwa imani yake: “Bwana wewe wajua kuwa ninakutakia mema”. Yesu anamwambia: “Nifuate!  Wito huo  kwa mara ya pili, ni wito wa upendo, wa kujitoa kila kitu! Na si tu kuacha, bali kutoa kila ulicho nacho binafsi, japokuwa Petro hakuwa na uwezo huo bado.

Miaka 30 inapita na miaka 30 ya kupiga magoti mbele ya Mungu

Kwa kuhitimisha, mahubiri yake, Askofu Mkuu Fischela anathibitisha kuwa, itapitia miaka 30, kama ilivyo andikwa juu ya maelezo ya Sanamu ya Mtakatifu Petro kwamba: itapita miaka 30 na baada ya miaka 30, Petro wakati ule atapiga magoti mbele ya Mungu. Petro sasa anao uwezekano na uwepo wake wa kujitoa yeye binafsi. Hiyo ndiyo zawadi ya kofodini. “Hakuna anaye kuondolea maisha, bali  mimi ninayotoa mwenyewe kwa ajili yako” na ndipo tazama hapo Petro anatimiza wito wake anathibitisha Askofu Mkuu na kuongeza kusema: hata kama itatakiwa miaka 30 , usijali; Mungu ana uvumilivu nasi. Wakati wake siyo wakati wetu. Yeye anakuwa kukutana nasi, Yeye anapoamua kuja kukutana nasi. Anapaswa kukuta mioyo iliyo wazi. Na Petro hapo anasema na kama alivyokuwa amesema Paulo kwa wakristo wa kwanza wa Tesalonika kuwa, “Sisi tulikuwa tunataka kuwapa si Injili tu bali maisha yetu wenyewe”. Hapa Petro anatoa maisha yake: hapa ndiyo kukiri imani ambayo lazima igeuke kuwa ya kwetu, yenye uwezo wa kutoa maisha yetu kwa Bwana Yesu!

25 October 2018, 14:29