Tafuta

Briefing ya Sinodi ya maaskofu kuhusu vijana tarehe 8 Oktoba 2018 Briefing ya Sinodi ya maaskofu kuhusu vijana tarehe 8 Oktoba 2018 

Sinodi, Askofu Mkuu Scicluna:ipo kiu ya haki ya kutafuta ukweli!

Briefing mpya juu ya kazi ya Sinodi imetolewa na vyombo vya habari Vatican kwa waandishi wa habari. Kati ya walio shirika katika briefing, alikuwa Askofu Mkuu Charles J. Scicluna wa Malta ambaye amezungumza kiu ya ukweli na haki katika suala la manyanyaso, lakini pia kuonesha hata mapadre wengi watakatifu wanaosaidia vijana katika safari ya maisha

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kiu ya ukweli na haki katika suala la manyanyaso, lakini pia uwepo wa  mapadre wengi. Ndiyo masuala msingi ya  baba wa Sinodi aliyechaguliwa na Baraza la Maaskofu wa Malta, Askofu Mkuu Charles J. Scicluna wakati wa kutoa briefing, Jumatatu mchana tarehe 8 Oktoba 2018 katika ukumbi wa  habari Vatican kwa waandishi wa habari juu ya Sinodi ya XV ya Maaskofu inayohusu, “vijana, Imani na mang'amuzi ya miito”.  Kwa kuzingatia maswali aliyoulizwa hasa kuhusu manyanyaso, Askofu Mkuu wa Malta amewambia waandishi wa habari kuwa kashfa hiyo ambayo inaonekana katika kitendea Kazi, Instrumentum Laboris, kipengele cha 66 ni kisima cha aibu hasa kwa sababu, sehemu kubwa ya waathirika ni vijana, wakiwa na majeraha na ambayo yangeweza kuponeshwa na yule ambaye amesababisha, na ambayo yanahitaji kuwajibika.

Kiu ya haki na ukweli

Askofu Mkuu pia amesema, haki hiyo haipaswi lakini kuchukua muda kwa maana hata Papa mwenyewe anateseka kuona mchakato unakwenda taratibu licha ya kutambua kuwa kuna utaratibu wa muda wa kisheria kwa upande wa kiraia. Kadhalika Askofu amesisitiza kwamba, hata hivyo wote tunahitaji huruma ya, lakini pia huruma hiyo ni inaweza kuwa ya utupu iwapo aiheshimu ukweli na haki. Kwa kufikiria mkutano ulioitishwa tarehe 21-24 Februari 2019 kwa Marais wa mabaraza ya maaskofu ulimwenguni kote ili kujadili suala la ulinzi wa wadogo dhidi ya manyanyaso, ameongeza kusema kuwa, ni muhimu kwenda katika mzizi wa tatizo, akikumbuka kuwa, huduma lazima iwe huduma na siyo kutumia madaraka. Askofu Mkuu wa Malta mwisho amekumbusha kuwa hata wale mapadre watakatifu ambao wanafany a kazi na wana imani katika Bwana.Utakatifu ni kukutana kati ya udhaifu wa binadamu na huruma ya Mungu.

Vijana katika kutafuta furaha

Katika mchakato wa briefing, Baba wa Sinodi aliyechaguliwa na Baraza la Maakofu wa Ufaransa, Askofu Emmanuel Gobilliard wa Jimbo la Carpentras na msaidizi wa Lyon , amekumbusha hata mada nyingine ambazo hadi sasa zimegusiwa wakati wa kazi, kama vile mshikamano kati ya kizazi, mchango wa wanawake katika utume wa Kanisa, masuala ya uhamiaji na yale yanayohusu ngono, kama vile hata ya utakatifu. Askofu amesisitiza kuwa:“Kila kijana amaalikwa kuwa na furaha, utakatifu na kukutana na Kristo”. Akimbusha hata ushauri wa Baraza la Maaskofu wa Ufaransa, anathibitisha: “tendo la kuwa binadamu, linahitaji usikivu makini katika ugumu wake na sio kubaguliwa katika urahisi wa utambulisho, lazima kuweka kiini msingi na siyo kitu”.

Jibu hata kwa vijana waliozaliwa katika nyakati za kipindi kama maji maji

Katika ukumbi wa habari Vatican, alikuwapo hata Thomas, Leoncini, msikilizaji, mwandishi wa vitabu na mtaalam wa mitindo ya kisaikolojia na kijamii nchini Italia. Ni mwenye umri wa miaka 33 ambaye amaeelezea kupenda mkutano huo. Na ambao unaonesha mapenzi ya Kanisa kijikita katika usikivu na bila kujizuia kwa urahisi wa  dhamiri tu, bali katika kutafuta majibu yenye msingi.  Kwa maana hiyo ameongeza kusema, ni sinodi ambayo haitazami vijana katoliki, bali haya hata wasio amini, na ambao wako katika kutafuta maana ya masha na vijana wote ambao wanatafuta matumaini ya wakati endelevu katika jamii hii iliyo kama maji maji.

 

09 October 2018, 10:52