Tafuta

Vatican News
Sarafuza  shaba na dhahabuza za kumbukumbu 2018 zimetolewa Sarafuza shaba na dhahabuza za kumbukumbu 2018 zimetolewa 

Sarafu kwa ajili ya kumbukumbu ya Padre Pio na Paulo VI

Zimetengenezwa aina mbalimbali za sarafu ambazo zimetolewa kuanzia tarehe 3 Oktoba ambazo ni za shaba na dhahabu katika kufanya kumbukumbu ya miaka 50 tangu kifo cha Padre Pio na miaka 40 ya tangu kifo cha Papa Paulo VI

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Na ofisi ya Filatelico na Numismatico ya kutengeneza Sarafu mjini Vatican, katika fursa ya kukumbuka Padre Pio na Paulo VI wametoa sarafu mpya tarehe 4 Oktoba 2018. Hii ni kutaka kufanya kumbukumbu ya miaka kama mfano wa mika 50 tangu kifo cha Mtakatifu Padre Pio

Sarafu ya Mtakatifu Padre Pio

Zimetengenezwa aina mbalimbali za sarafu ambazo zimetolewa kuwanzia tarehe 4 Oktoba. Kwa maana hiyo kutaka kukumbuka miaka muhimu kama vile miaka 50 tangu kifo cha Padre Pio kilichotokea tarehe 23 Septemba 2068 huko San Giovanni Rotondo.

Sarafu ya Papa Paulo VI na Yohane Paulo I

Ni karibia sarafu 4,500 zilizotengenzwa katika kufanya kumbukumbu ya kutangazwa Mtakatifu Papa Paulo VI tarehe 14 Oktoba na kumbukumbu ya miaka 40 tangu kifo cha Papa Yohane Paulo I. Ofisi ya Filatelico inaadhimisha kutolewa kwa sarafu mbili, zote pamoja zikiwa ni shaba. Na ile inayohusu Papa Montini yaani Papa Paulo VI inathamani ya euro 5 na nyingine ya Papa Luciani yaani Papa Yohane Paulo I ina thamani ya euro 10, zilizotengenzwa na wasanii Patrizia, Daniele na Mariangela Crisciotti.

Sarafu iliyotolewa kukumbusha Kitabu cha Matendo ya Mitume

Ofisi ya Filatelico na Numismatic inaanza na mzunguko mpya wa kazi yake ya utenegenezaji wa sarafu za dhahabu kuanzi euro 20 hadi 50 ambazo zinahusu, kitabu cha  Matendo ua Mitume. Ni kitabu cha tano katika Agano la Jipya linalotoa habari zaidi ya kile ambacho kinatukia baada ya Ufufuko wa Kristo.

Euro 20 ya dhahabu, zimetengenezwa na msanii Orietta, ikionesha Kupaa kwa Yesu; na Euro 50 ya dhahabu imetengenezwa na Daniela Longo, inayowakilisha Pentekoste, sherehe kubwa ya dini inayokumbusha maandhimisho ya kushuka kwa Roho Mtakatifu kwa njia ya ndimi za moto juu ya Mitume na Bikira Maria wakiwa wameungana katika Karamu

 

 

04 October 2018, 16:18