Tafuta

Vatican News
Papa Francisko, tarehe 13 Oktoba 2018 amekutana na Rais wa Chile; amewavua pia hadhi ya ukasisiviongozi wawili wa Kanisa. Papa Francisko, tarehe 13 Oktoba 2018 amekutana na Rais wa Chile; amewavua pia hadhi ya ukasisiviongozi wawili wa Kanisa. 

Papa akutana na Rais wa Chile; awavua ukasisi viongozi wawili wa Kanisa kutoka Chile!

Viongozi hawa wamekazia umuhimu wa ushirikiano wa dhati kati ya wadau mbali mbali ili kuhakikisha kwamba, kashfa hii inatokomezwa katika jamii, kwa kuzuia na wahusika wote kufikishwa mbele ya sheria, ili haki iweze kutendeka! Baba Mtakatifu ni mgeni wake, wamegusia pia mada nyingine zenye mwelekeo wa kimataifa na kikanda hasa suala la wakimbizi na wahamiaji.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi, tarehe 13 Oktoba 2018 amekutana na kuzungumza na Rais Sebastian Pinèra Echenique wa Chile, ambaye baadaye amekutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallaghar, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wameridhishwa na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili. Wamekazia umuhimu wa jamii kusimama kidete kulinda na kutetea Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo na kashfa ya nyanyaso dhidi ya watoto wadogo.

Viongozi hawa wamekazia umuhimu wa ushirikiano wa dhati kati ya wadau mbali mbali ili kuhakikisha kwamba, kashfa hii inatokomezwa katika jamii, kwa kuzuia na wahusika wote kufikishwa mbele ya sheria, ili haki iweze kutendeka! Baba Mtakatifu ni mgeni wake, wamegusia pia mada nyingine zenye mwelekeo wa kimataifa na kikanda kwa kuangalia changamoto ya kuwapokea na kuwahifadhi wakimbizi na wahamiaji.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amewavua ukasisi: Padre Francisco Josè Cox Huneeus na Marco Antonio Ordenes Fernàndez, Askofu mstaafu wa Jimbo Katoliki la Iquique kutokana na kujihusisha na kashfa ya nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo. Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Kanisa kuhusu ulinzi wa watoto wadogo dhidi ya nyanyaso za kijinsia. Huu ni uamuzi wa mwisho kutoka kwa Baba Mtakatifu na wala hakuna nafasi ya kukata rufaa. Wahusika wote wamekwisha kufahamishwa uamuzi wa Kanisa kama sehemu ya mapambano dhidi ya kashfa ya nyanyaso za kijinsia ambazo kwa miaka ya hivi karibuni zimechafua maisha na utume wa Kanisa nchini Chile.

14 October 2018, 15:08