Cerca

Vatican News
Kardinali Giovanni Angelo Becciu Rais Mpya wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza wenye heri na watakatifu Kardinali Giovanni Angelo Becciu Rais Mpya wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza wenye heri na watakatifu 

Kard. Becciu Mwenyeheri Anna Kolesárová mfano wa kuigwa na vijana

Kardinali Becciu huko Slovakia kwenye fursa ya kumtangaza kijana mfiadini Anna Kolesárová, aliyekuwa na umri wa mika 16 aliyeuwawa mnamo mwaka 1944 kwa njia ya mikono ya wajeshi wa kisovietik wakati wa vita nchini humo.

Sr. Angela - Vatican

Katika mkesha wa kuanza rasmi kama Rais mpya wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza wenye heri na watakatifu, Kardinali Becciu huko Slovakia kwenye fursa ya kumtangaza kijana mfiadini Anna Kolesárová, aliyekuwa na umri wa mika 16 na kuwawa 1944 kwa njia ya mikono ya wajeshi wa kisovietik wakati wa vita nchini humo, amewaalika wakatoliki kuungana pamoja na Baba Mtakatifu Francisko katika kipindi hiki cha ulegevu wa imani kati ya waamini.

Ameyasema hayo wakati wa mahojiano na Vatican news akisimulia hisia zake za kuanza sehemu hii mpya ya maisha yake kwamba anahisi utulivu wa ndani, na kuwa na fursa ya kuanza siku ya kwanza na kazi ya kumtangaza kijana Anna Kolesárová. Kwa maana hiyo anaanza na matashi mema na furaha kubwa.

Ujumbe wa Kijana huyo ambaye anatangazwa kuwa mwenye heri, ni ujumbe unaokwenda kinyume na kijana wa miaka 16 ya leo. kwa maana ni kijana ambaye kwa wakati ule alikuwa tayari ana nguvu ya kuvumilia mateso katika mikono ya wanajeshi wa kisovietik ambao walitaka kumnyanyasa kijinsia. Yeye alikataa na akiwa na utambuzi wa kutaka kutunza usafi wake. Katika dunia ya leo, ambayo wengi wancheka na kukejeli thamani hiyo, ujume huu ni mwafaka kwao. Aidha ameshangazwa na kijana huyo ambaye aliugunduliwa na kikundi cha wanafunzi wenzake, waliojua kufuata dini na hivyo wengi walikwenda katika kaburi lake.  Kuanzia hapo ikatokea kugundua maisha ya kijana huyo ambaye hadi kufikia mapadre kuanza kuwa makini na kusambaza juu ya historia ya maisha ya Anna Kolesárová.

Huo ni ushuhuda wa imani ya nguvu na rahisi katika nyakati zile na hata za sasa. Kanisa kwa wakati ule, Kardili Becciu anafafanua kwamba, hakika hata leo hii, watu wamekuwa na mashaka juu ya imani yao, na kama wakatoliki basi ni muhimu kuwa na ukaribu wa Baba Mtakatifu na uwezekano wa kumtetea daima. Na ni matumaini ya Kardinali Becciu kuwa kile tulichokipokea tangu tukiwa watoto ya kwamaba Papa anapendwa na yeye anapenda hadi mwisho. Na kwa maana hiyo tunapokea maelekezo , mafundishi na maneno daima yake ya kutia moyo, hivyo tuungane na Papa, kwani kwa kuungana pamoja Kanisa litaokoka. Lakini iwapo tutagawanyika, Kanisa litaishia katika  matokeo mabaya. Kardinali Becciu anaomba ushirikiano maombi ya pamoja kwa ajili ya  Papa na Kanisa lote zima.

01 September 2018, 16:10