Tafuta

Saini ya Mkataba wa Muda kati ya Vatican na Serikali ya  Jamhuri ya Watu wa China Saini ya Mkataba wa Muda kati ya Vatican na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China 

Vatican na Jamhuri ya China kutia saini ya Mkataba wa muda!

Baaada ya hatua ndogo ndogo ya ukaribu, hatimaye umetiwa saini mkataba wa muda mjini Peking kati ya Vatican na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China juu ya uteuzi wa Maaskofu!

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mfumo wa mawasiliano kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China, ambao umeendelea kwa muda mrefu katika mchakato wa  kukabiliana na masuala ya pamoja ya kidini katika  maslahi ya kawaida ya kukuza mahusiano zaidi ya ufahamu, hatimaye tarehe 22 Septemba 2018, imewezekana  kutia saini ya Mkataba wa muda i, mjini Peking katika  mkutano kati ya Askofu Mkuu Antoine Camilleri, Katibu Msaidizi wa Mahusiano na ushirikiano wa kimataifa Vatican,  pamoja na Mhesh Wang Chao, Waziri msaidizi wa Biashara na Mambo ya nchi za nje wa Jamhuri ya watu wa China, wakiwepo pia wawakilishi viongozi wakuu wa Vatican na China.

Katika muktadha wa mkutano huo, Wawakilishi wawili walisaini Mkataba wa Mpango wa makubaliano ya muda juu ya uteuzi wa Maaskofu. Mkataba wa Muda mfupi ni matokeo ya matunda ya mchakato wa taratibu  taratibu na wa pamoja. Kwa hakika ni   baada ya mchakato mrefu wa mazungumzo yenye uzito na kutoa tathmini mara kwa mara juu ya utekelezaji wake. Mkataba huo unajihusisha  na uteuzi wa Maaskofu, ambalo ni suala muhimu  kwa maisha ya Kanisa na inajenga mazingira ya ushirikiano mkubwa katika ngazi ya nchi mbili.

Ni matarajio ya kwamba makubaliano hayo, yanaweza kuleta matunda ya muda mrefu ya mchakato wa mazungumzo ya katiba na kuchangia unyanya wa maisha ya Kanisa Katoliki nchini China, wema wa watu wa China na amani katika ulimwengu.

 

25 September 2018, 10:24