Tafuta

Vatican News
Kardinali Krajewski alitembelea wakimbizi katika kituo cha  Mondo Migliore Kardinali Krajewski alitembelea wakimbizi katika kituo cha Mondo Migliore 

Baraka na salam ndizo zawadi za Papa kwa wakimbizi

Watoto wakimbizi hawakukosa kumtumia Papa zawadi kwa maana watoto wawili wa Siria walimtumia picha yake waliyo ichora,pia mwanamke mmoja wa kiislal amemtumia Papa Picha ya Bikira Maria aliyofuma kwa mikono yake

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 5 Septemba  2018 Kardinali Konrad Krajewski, Krajewski Mhusika Mkuu wa Sadaka ya Papa, alitembelea Kituo cha Mondo Migliore huko Rocca di Papa kwa ajili ya kuwaona wahamiaji walio kwekwa hapao mara baada ya malumbano ya meli yua Dicioti wiki za hivi karibuni huko Cicilia. Kardinlai amekwenda kuwakilisha Papa , ambapo ametoa salam na baraka kwa niaba yake. Aliye msindikiza Karidnli Conrad alikuwa na Mkurugenzi wa Caritas ya Italiwa Moanisnyo Francesko Soddu. Wahamiaji waliko katika jengo hilo, bado wanendelea kuwaganywa katika maeneo mbalimbali ya majimbo katoliki chini Italia.

Chakula cha mchana na zawadi za Papa

Kardinali, Conrad, amepata mlo wa mchana na wahamiaji karibia 340 ambao bado wapo katika kituo hicho, wahudumu, na baadaye amekutana na watu 40 wa kujitolea ambao wanajikita katika wiki hizi mbili kusaidia kupanga namna ya kuwahamisha vijana hawa katika majimbo mengine nchini Italia. Naye Kardinali, ametoa zawadi ya picha ya Papa ambayo imepokelewa kwa shangwe kuu na furaha, Hata hivyo zawadi nyingine hazikukosa za kumtumia Papa kutoka kwa watoto wawili wa Siria ambao wamemtumia Papa picha waliyo ichora, pia mwanamke mmoja wa kiislam amemtumia Papa Picha ya Bikira Maria aliyofuma kwa mikono yake.

Ice-cream 20000 kwa maskini

Katika taarifa kutoka ofisi ya Sadaka ya Papa, wanajulisha kuwa tarehe 5 Septemba 2018 pia  zimetolewa   Ice-cream 20,000 katika nyumba za mapokezi na vituo vingi vya chakula cha maskini mjini Roma. Zawadi hii imetolewa na kiwanda kimoja ambacho kilitaka kushirikishana na wahitaji. Pamoja na hayo hata Icecream 1,300 zimeweza kufika katika Kituo cha Mondo Migliore cha Rocca di Papa kando kando ya mji wa Roma.

06 September 2018, 13:08