Cerca

Vatican News
Mwenyeheri Papa Paulo VI alifanya ziara yake ya kitume nchini Colombia 1968 Mwenyeheri Papa Paulo VI alifanya ziara yake ya kitume nchini Colombia 1968 

Ziara ya Papa Paulo wa VI nchini Colombia miaka 50 iliyopita!

Papa wa kwanza kutembelea Amerika ya kusini, alipowasili mji mkuu Bogotà nchini Colombia kuanzia tarehe 22-25 Agosto 1968, aliongea na maaskofu na mapadre wa Colombia katika Kanisa kuu; kuhusu Ekaristi ambayo ilikuwa na kauli mbiu ya kongamano, na kutoa daraja la upadre kwa mapadre 200 na mashemasi!

Frt Tito Kimario - Vatican

Miaka 50 iliyopita, Colombia ilibahatika kutembelewa na Baba Mtakatifu Paulo wa VI katika safari yake ya sita ya kitume  mjini Bogotà kuanzia tarehe 22-25 Agosto 1968. Ni katika kongamano la Ekaristi kimataifa na mkutano mkuu wa maaaskofu wa Amerika ya kusini, waliokutana Medellìn.  Papa wa kwanza kutembelea Amerika ya kusini, alipowasili mji mkuu, aliongea na maaskofu na mapadre wa Colombia katika Kanisa kuu; kuhusu Ekaristi ambayo ilikuwa kauli mbiu ya kongamano, ambapo pia alipta fursa ya kutoa daraja Takatifu la upadre kwa mapadre 200 na mashemasi wa Colombia.

Siku iliyofuata, katika misa kwa ajili ya “siku ya maendeleo” katika uwanja Mtakatifu Yosefu iliyohudhuriwa na watu mia tatu elfu, Papa alikemea juu ya ukosefu wa msimamono na ukosefu wa haki kijamii mambo ambayo yalikuwa tayari katika barua yake ya kichungaji “ Populorum Progressio” ya mwaka uliotangulia 1965, akifafanua zaidi  juu ya “upendo mkuu usi ona kikomo  wa Kanisa kwa masikini na akawataka kuepuka fujo na uvunjivu wa amani ili kuinua matarajio ya watu.

Papa pia alikutana na wawakilishi wa makanisa ya kikristo, Jumuiya ya Wayahudi na wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao Colombia. Siku iliyofuata katika Kanisa kuu, alizindua mkutano mkuu wa maaskofu  kutoka bara la America ya Kusini, akiwakabidhi maaskofu kazi ya “kuhimiza jitihada zote za uaminifu ili kukuza na kuimarisha maisha ya maskini” na kutoa onyo kwamba: Hatuwezi kuwa na  mshikamano wa mifumo na miundo ambayo hufunika na kuendekeza ukandamizaji mkubwa wa usawa wa madaraja kati ya wananchi wa nchi moja. Baada ya uzinduzi wa makao makuu mapya ya Baraza la Maaskofu wa Amerika ya kusini (CELAM) na mikutano ya viongozi wa serikali na watawa aliwaaga na kurejea Roma.

Ziara ya Papa nchini Colombia ilipotangazwa.

 Frateli Roger aliyemfahamu vizuri Papa Paulo wa sita hata alipokua bado “Askofu Montini” aliyechukua nafasi ya katibu wa Vatican na aliyeota kwenda Amerika ya kusini. Alipojua ya kwamba ndoto ile ingetimia tena na mmoja wa jumuiya yao, frateli Robert alialikwa kusafiri pamoja na Baba mtakatifu  Paulo VI ndani ya ndege moja “kama mgeni na rafiki wa Papa”, moyo wake ulienda kasi! Anatthibitisha kuwa: “Nina furaha kuu leo kupata bahati ya kuelezea sababu ya yote haya. Wakati ule sikuwa kwenye jumuiya ila nilisikia mara nyingi fateli Roger akizungumzia; na ilibaki kuwa kumbukumbu ya daima kati yetu, ile safari ya mwanzilishi wetu akiwa na Papa kwenda Bogotà. Wazo la kumsindikiza Baba Mtakatifu katika utume wake mpya, ambayo ni safari kubwa, anaeleza frateli Roger.

Baadaye wakati wa Papa Yohane Paulo II, Safari za Papa za kitume kwenda dunia nzima zilikuwa jambo la kawaida katika maisha ya Baba Mtakatifu ila kwa wakati wa  Papa Paulo VI, kutoka bara moja hadi jingine bado lilikuwa jambo la kipekee sana. Frateli Roger alikuwa na furaha ya kushiriki kwa maana baada ya mikutano na Papa Yohane wa XXIII iliyomgusa sana, aliendelea kuweka ukimya moyoni na kutafakari maana ya utume wa mchungaji mkuu wa dunia katika moyo wa Kanisa. Hadharani anaongea kidogo sana, anajua ni mada moto ya mahusiano kati ya wakristu waliotengana. Kuona kwa karibu Papa Paulo VI akitimiza utume wake duniani kunavutia na kufurahisha.

24 August 2018, 08:52