Cerca

Vatican News
Picha ni mwimbaji maarufu Andrea Bocelli anayetarajiwa kutuimbuiza katika tamasha la Familia Dublin Picha ni mwimbaji maarufu Andrea Bocelli anayetarajiwa kutuimbuiza katika tamasha la Familia Dublin 

Mwimbaji maarufu Andrea Bocelli katika Tamasha mjini Dublin

Mahojiano maalum, Vatican News na mwimbaji maarufu Andrea Bocelli ambaye tarehe 25 Agosti 2018 ataimba katima Tamasha la Familia huko Dublin kwa ajili ya Papa Francisko na Familia nzima ya Ulimwengu. Wanachi Dublin wanasubiri kwa hamu kubwa kusikiliza sauti yake nzuri mwimbaji huyo!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Itakuwa ni siku ya aina ya pekee katika Mkutano wa IX wa Dunia kwa ajili ya Familia  huko Dublin, kwani kunako tarehe 25 Agosti 2018 katika Uwanja wa Crocke mjini Dublin Mwimbaji mashuhuri wa nchi ya Italia, Bwana Andrea Bocelli ataimba kwa ajili ya Papa Francisko na kwa ajili ya familia duniani watakio wakilishwa na wanafamilia kutoka nchi 100!

Mwimbaji huoyo mashuhuri mwenye sauti ya kushangaza, ameahi kuomba hata katika mikutano mingine ya familia mwezi Septemba 2015 huko Filadelfia.Hata hivyo siku chache mara baada ya tukio la Dublin msanii huyo maarufu ataimba tena katika mji wa Verona Italia, tarehe 8 Septemba 2018 katika fursa ya tamasha la hisani. Katika usiku huo wa tamasha hili, fedha sitakazo patikana ni kwa ajili ya  mpango wa chanama chake “Andre Boccelli na Muhammad Ali Parinkson Centre.

Katika mahojianno na Vatican news Bwana andrea ameelezea umhimu wa imani katika maisha yake, mategemeo yake binafsi kwa  mkutano huko Dublin na kusistizia jinsi gani muziki unaweza kusaidia familia kuishi na kushuhudia furaha na upendo kama anavyoomba Baba Mtakatifu Francisko.

Katika mahojiano hayo Bwana Andrea akielezea juu ya shauku alizo nazo juu ya mkutano na kuweza kuimba kwa ajili ya papa na familia duniani, kwa urahisi anasema hawali ya yote kama msanii kupewa fursa ya aina hiyo ni tunu kubwa, hasa kuimba mbele ya Baba Mtakatifu, jambo ambalo analipenda, hasa kiumbe mdhaifu hivyo kuweza kukutana na mwenye karama kubwa kama Papa, ni kuhisi furaha ya ajabu!  Lakini pia anathibitisha kwamba, ni uwajibikaji, hasa katika  mantiki kama hizi muhimu, na ni kutoa ujumbe unaostahili kulingana na siku yenyewe. Kuna haja ya kutoa ujumbe unao kwenda na siku hiyo, hivyo anakiri kwamba atafanya kila liwezekanalo kuwa tayari, kujiandaa kikamilifu kama jinsi afanyavyo katika fursa mbalimbali za kimataifa na kitaifa na matarajio yake kwamba familia zinaweza kuondoka mwenda nyumbani kwao wakiwa na kumbukumbu ya muda huo wa nyimbo zake!

Akijibu juu ya swali ambalo wangi watakao udhuria mkutano huo, mara baada ya kusikia tangazo hili wanayo matarajio makubwa, na huko Dublin wengi wanamsubiri kwa hamu kubwa kumwona mna kumsikiliza, Yeye binafsi anasema amesha zoea kila mmara akipanda katika jukwaa kama msanii anapenda ajitoa na kuonesha  ubora yeye alivyo. Na kwa kawaida wasikilizaji na watazamaji, wanapokea kadiri msanii na matokeo ya shukrani ambazo yeye binafsi amejiandaa. Ni mategemeo yake kuwa hivyo na kupokelewa hivyo. Hata watu wa Ireland hata hivyo anawapenda na hivyo kuwa na utulivu wa ndani kabisa…

Papa Francisko anaomba familia zote ziwe na furaha kwa ajili ya ulimwangu , waweni waamni au wasio waamini. Wimbo na muziki wake utaweza kusaidia familia katika changamoto hiyo?

Bwana Bocelli katika kujibu swali hili anasema, kila chochote kifanyikacho na chenye lengo jema  uweza kusaidia na kwa hakika kinasaidia ! Kwa mna hiyo kazi yake ya kisanii kama ya kuimba, inajikita katika lengo hilo la  kutoa furaha, kutoa muda wa kulegea  na kulainisha roho ambayo kwa wakati mwingine uweza kupaa na kutaka kutafakari, kwa nama ya kutafuta maana ya maisha, juu ya mambo ambayo kwa dhati ni ya msingi…. Wimbo  kwa namna hiyo ni sehemu muhimu na ya uhakika katika sual hili la furaha. Na kwa kutilia mkazo zaidi wa nyimba kama sala anasema Mtakatifu Agostinio alikuwa anasema “ anayeimba anasali mara mbili ! Kwa upande wake Bwana Bocceli anathibitsha kuwa  anaamini kwasababu kama ni kweli katika maisha yake amesali sana kutokana na nyimbo.

Kama anamtaja Mtakatifu Agostino , kwa yule anaye amini , sauti ya Andrea ni zawadi ya Mungu. Je imani yake inapewa sehemu gani, na katika talanta yake ya kimuziki ambayo ni zawadi lakini pia ni zawadi ambayo ni lazima kuilisha?

Katika kuelezea hili, amependa kueleza tangu mwanzo , kwamba wimbo, sauti kama vile talanta nyinginezo duniani ni zawadi kutoka kwa Mungu , na kwa vitu hivyo hakuna wasiwasi wowote. Pia hakuna binadamu anayestahili kwasababu. Kila iana ya kitu kinachofanywa katika maisha ya binadamu kinafanywa kwa nia ya zawadi bna talanta tulizopokea bure bila masitahili, kwa  maana hiyo naongeza  hakuna haja ya kujivunia lolote kwa maana yote tumezwadaiwa na lazima kutoa shurani tu. Imani ni safari ambayo inatafuta namna ya kujua, kutambua maana ya maisha, Andrea naamini kwamba kila mmoja ameweza angali kukaa na kufikiria nini maana ya maisha. Na huwezi kufikiria umekuwa mtoto kwa bahati mbaya.

Asiye kuwa na imani ni sawa sawa na mfano huo wa anayefikiria picha ya Michelangelo ya huruma, Laki kwake yeye ni mchakato wa imani kubwa, ambayo yeye mwenywe alifikiria kwamba dunia haiwezekani kuwa tunda la utashi wa kiakili tu, zaidi ya akili zetu na katika kila tendo. Ni lazima kuamini utashi wa upendo ambao kweli unapendwa kwa dhati.

Aidha akihitimisha amethibitsha kwamba ipo mitindo ya  imani, kwa mfano ile ya wakristo ambao wanamweka  Mungu kuwa nafasi ya kwanza ya  matumaini na imani inayowezekana, wakati huo wapi wengine wa Iago na Otello wa shakespeare ambaye alikuwa anasema; ninaamini kwa Mungu mkatili ambaye alijiumba na kuifanana mwenyewe. Kwa maana hiyo inawezekana  wengine kuamini hivyo. Na mara nyingi inajitokezaoa kuliko kuamini anathibitisha Msanii maarufu Bwana Andre Bocelli.

 

 

16 August 2018, 16:34