Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
MISA KWA KILATINI: MUBASHARA
Ratiba Podcast
Jumatatu tarehe 9 Septemba 2024 Baba Mtakatifu ameanza hija yake ya kitume nchini Timor ya Mashariki. Jumatatu tarehe 9 Septemba 2024 Baba Mtakatifu ameanza hija yake ya kitume nchini Timor ya Mashariki.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Timor ya Mashariki: Utamadunisho

Jumatatu tarehe 9 Septemba 2024 Baba Mtakatifu ameanza hija yake ya kitume nchini Timor ya Mashariki. Hiki ni kituo cha tatu cha hija hii inayonogeshwa na kauli mbiu “Que a vossa fé seja a vossa cultura.” Ni himizo na kutia moyo kuishi imani mintarafu utamaduni na mila za watu wa Timor ya Mashariki. Akiwa njiani ametuma salam na matashi mema kwa Gavana mkuu wa Papua New Guinea pamoja na Gavana mkuu wa Jumuiya ya Madola ya Australia. Utamadunisho!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 2 hadi 13 Septemba 2024 anafanya Hija ya 45 ya Kitume Barani Asia na Oceania kwa kutembelea Indonesia, Papua New Guinea, Timor ya Mashariki na hatimaye, Singapore. Katika hija hii, Baba Mtakatifu Francisko ni shuhuda wa majadiliano ya kidini na kiekumene kama njia mahususi katika ujenzi wa mshikamano; mafungamano na udugu wa kibinadamu; haki, amani na maridhiano kati ya watu wa Mataifa. Kimsingi ni hujaji wa matumaini, faraja na ujirani mwema. Hii ni kati ya hija ndefu kuwahi kutekelezwa na Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Papa Francisko Hija ya Kitume Timor ya Mashariki 9-11 Septemba 2024
Papa Francisko Hija ya Kitume Timor ya Mashariki 9-11 Septemba 2024   (AFP or licensors)

Jumatatu tarehe 9 Septemba 2024 Baba Mtakatifu Francisko ameanza hija yake ya kitume nchini Timor ya Mashariki. Hiki ni kituo cha tatu cha hija hii inayonogeshwa na kauli mbiu “Que a vossa fé seja a vossa cultura.” Ni himizo na kutia moyo kuishi imani mintarafu utamaduni na mila za watu wa Timor ya Mashariki. Akiwa njiani, Baba Mtakatifu amemtumia telegramu Bob Dadae, Gavana mkuu wa Papua New Guinea, akimshukuru kwa niaba ya viongozi wote wa Papua New Guinea kwa ukarimu na mapokezi ya “kukata na shoka” waliyompatia wakati wa hija yake ya Kitume nchini humo. Amewahakikishia sala na sadaka yake kwa watu wa Mungu nchini Papua New Guinea na kwamba, anawaombea amani na utulivu.

Umati mkubwa wa watu wa Mungu Timor ya Mashariki umejitokeza kwa Papa
Umati mkubwa wa watu wa Mungu Timor ya Mashariki umejitokeza kwa Papa   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Baba Mtakatifu Francisko alipokuwa anaingia kwenye anga la Australia amemtumia ujumbe Sam Mostyn, Gavana mkuu wa Jumuiya ya Madola ya Australia, akiwatakia kheri na fanaka; na kwamba anapenda kuwahakikishia sala na baraka zake. Baba Mtakatifu amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dili na kulakiwa na viongozi wa Serikali na Kanisa. Hii ni hija kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 11 Septemba 2024.

Safari Timor ya Mashariki
09 Septemba 2024, 15:00
Prev
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930   
Next
May 2025
SuMoTuWeThFrSa
    123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031