Tafuta

2024.05.22  Picha ya Pamoja rsimi ya Mkutano Mkuu II wa Talitha Kum 18-24 Mei  2024. 2024.05.22 Picha ya Pamoja rsimi ya Mkutano Mkuu II wa Talitha Kum 18-24 Mei 2024.  ((foto: M. Simionati/Talitha Kum)

Papa:Tuendelee kama Talitha Kum:kuwa karibu na waathirika,tuwasikilize!

“Usafirishaji haramu wa binadamu ni shughuli isiyoheshimu na kupuuza mtu yeyote,ikihakikisha faida kubwa kwa watu wasio na maadili. Usafirishaji haramu wa binadamu unabadilika kila wakati na kila wakati hupata njia mpya za kukuza, kama ilivyotokea wakati wa janga la uviko."Ni katika Ujumbe wa Papa Francisko aliotuma katika Mkutano Mkuu II wa Mtandao wa Kimataifa wa Talitha Kum ulianza tarehe 18 na unahitimishwa 24 Mei 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Talitha Kum, tarehe 23 Mei 2024 katika ujumbe huo ananza kusema kuwa “Moyoni mwangu kuna shukrani nyingi kwa kile mnachofanya, kibinafsi na wote kwa pamoja, kushinda biashara ya binadamu, mojawapo ya mapigo ya kutisha zaidi ya wakati wetu. haramu wa binadamu ni uovu wa “kimfumo”, na kwa hivyo tunaweza na lazima tuuondoe kwa njia ya utaratibu katika viwango vingi. Usafirishaji haramu wa binadamu unaimarishwa na vita na migogoro, unafaidika na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, tofauti za kijamii na kiuchumi, inachukua fursa ya mazingira magumu ya watu wanaolazimishwa kuhama na hali ya kukosekana kwa usawa ambayo, juu ya yote, wanawake na wasichana wanajikuta.

Biashara haramu ya binadamu ni shughuli isiyoheshimu mtu

Baba Mtakatifu Francisko amekazia kusema kuwa “Biashara haramu wa binadamu ni shughuli isiyoheshimu na kupuuza mtu yeyote, ikihakikisha faida kubwa kwa watu wasio na maadili. Usafirishaji haramu wa binadamu unabadilika kila wakati na kila wakati hupata njia mpya za kukuza, kama ilivyotokea wakati wa janga la uviko . Hata hivyo, hatupaswi kuvunjika moyo. Kwa nguvu za Roho wa Yesu Kristo na kujitolea kwa wengi tunaweza kufanikiwa kuuondoa.”

Tunahitaji kufuata mfano wa Talitha Kum

Kwa njia hiyo Papa Francisko amesema kuwa “Tunahitaji kuendelea kufuatia kile ambacho kama Talitha Kum wamekuwa wakifanya kila mara: kuwa karibu na waathirika, kuwasikilize, kuwasaidie ili waweze kusimama wao wenyewe na  kwa pamoja, kwa kuchukua hatua dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu.” Na “ili kuwa na ufanisi wa kweli dhidi ya jambo hili la uhalifu la chuki, ni muhimu kuwa jumuiya. Haya yote yanaoneshwa vyema na mada ya mkutano wao: “Kutembea pamoja kukomesha usafirishaji haramu wa binadamu: huruma katika vitendo kwa ajili ya mabadiliko.”

Miito yao inajumuisha mwito mkali wa kuwajibisha serikali na taasisi za kitaifa na mahalia

Papa Francisko anakazia kusema kuwa “Siyo rahisi, lakini katika miaka hii kumi na tano umetuonyesha, katika kila latitudo, kwamba inawezekana kuifanya. Talitha Kum imekuwa mtandao ulioenea na wa kimataifa na, wakati huo huo, pia imejikita vyema katika Makanisa mahalia. Imekuwa rejea kwa waathrika, familia zao, watu walio katika hatari na jamii zilizo hatarini zaidi. Zaidi ya hayo, miito yao inajumuisha mwito mkali wa kuwajibika kwa serikali na taasisi za kitaifa na za sehemu mahalia.

Tutekeleze hatua za kuzuia,matibanu na kujenga uhusiano wa thamani

Papa amewahimiza kuendelea na njia hii, kutekeleza hatua za kuzuia na matibabu na kujenga mahusiano mengi ya thamani, ambayo ni muhimu kwa kupambana na kushinda biashara haramu. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amewaeleza kuwa anamshukuru “Bwana pamoja nanyi kwa kazi yote ambayo amewaruhusu kufanya katika miaka hii. Nitaisoma vizuri hati yenu na kuitangaza. Mama Yetu awasindikize kila wakati na kuwalinda. Ninawabariki kwa moyo wote ninyi na jumuiya zenu. Tafadhali endelea kuniombea.” Amehitimisha.

Ujumbe wa Papa kwa Taliyha Kum

 

23 May 2024, 17:18