Tafuta

Ujumbe wa Papa kwa Nuovi Orizzonti:karama,mwanzilishi na wanachama vilindwe!

Papa Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video aliomtumia Chiara Amirante na Jumuiya yake aliyoanzishwa katika fursa ya kushehereka miaka 30 tangu kunzishwa anamshukuru sana,kwamba wao wanawachukua walio wa mwisho bila kuwaondolea uhuru wao na wanafanya kwenda mbele nao na kulinda zawadi yao ya umoja na Kanisa.“Ukaribu kwa waliobaguliwa ndiyo uzuri wa karama yenu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya maadhimisho ya miaka 30 ya kuzaliwa Jumuiya ya Nuovi Orizonti, Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya Video  kwa Chiara Amirante  na jumuiya hiyo. Katika ujumbe huo, Papa anasema kuwa:“Napenda kutuma salamu kubwa kwa Nuovi Orizzonti pamoja na sherehe ya kumbukumbu ya miaka 30, na awali ya yote nimsalimu Chiara ambaye alikuwa mbunifu aliyechaguliwa na Mungu kuendeleza Harakati hiyo, pumzi hii ya Roho ambayo iliamsha dhamiri nyingi sana. “ Kwa njia hiyo katika siku ya kuzaliwa  iwe yenye furaha kwako kufikisha miaka  30 na mkafanye keki nzuri! Heri kuzaliwa!” Baba Mtakatifu amesema kuwa “Karama lazima ilindwe, kila wakati harakati inapokua kuna hatari kwamba karama inayeyuka kidogo na kupoteza nguvu ya mwanzo, karama lazima ilindwe na mwanzilishi, lazima alindwe na washiriki na wanapaswa kulindwa na Kanisa, kwa njia ya Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mashirika ya Kitwa na vyama vya Kitume husika ambalo lilifuatilia nyayo zao.

Sala na Ujasiri

Baba Mtakatifu Francisko aidha aliomba wasipoteze wazo hilo ambalo ni muhimu sana, kulinda maisha, kulinda kile ambacho Bwana amewapatia kupitia mwanzilishi. Karama yao lazima ilindwe na mambo mawili ya msingi: sala, huwezi kusonga mbele bila maombi, na ujasiri, usipoteze ari hiyo, ujasiri huo wa kuipeleka mbele. Karama inapotokea karibu kila mara katika historia ya karama katika Kanisa kumekuwa na nyakati za kutokuelewana, nyakati za giza, hata kwa upande wa Kanisa, nadhani kuhusu Jumuiya ya Yesu ambayo ilivunjwa na kisha kuishi tena,” Papa alisisitiza. “Wakati mwingine kuna nyakati ngumu, karama zote lazima zipitie msalaba wa Bwana, zinapita mapema au baadaye na ikiwa hatuchukui msalaba kwa nguvu ya Roho, tuna hatari ya kutafuta suluhisho ambazo sio za kiinjili. Ili kuendeleza karama na karama nyingi sana hupoteza nguvu zao baada ya muda na kutafuta mitindi ya kuishi ambayo kiukweli hujiweka mbali na karama hiyo. Uaminifu kwa karama ni moja ya mambo muhimu zaidi, kuilinda, na Kanisa linapoomba tuifanye ikue kwa amri fulani, tuwe waangalifu juu ya hilo, lakini daima uaminifu kwa Kanisa, utii kwa Kanisa na sio kwa wengine kutoka nje, au  shinikizo linalochukua fursa ya hali kuondoa uzuri wa  nguvu ya waanzilishi au mwanzilishi.

Kukabiliana na kutatua shida na matatizo

Papa Francisko vile vile alibainisha jinsi ambavyo alijua vema karama yao kutokana na habari, au kwa sauti, na alimjua mwanzilishi, lakini siku ambayo alielewa karama yao,  ndipo alikwenda kwao. “Kwangu mimi ilikuwa kama upako wa karama: kuona ninyi nyote mmeunganishwa na mwanzilishi na hamu ya kulipeleka Kanisa mbele. Wakati huo niliona kuwa mlikuwa na shida, lakini nilifurahi jinsi mlivyosuluhisha,  na mnajua jinsi ya kutatua mambo na shida. Lakini moja ya mambo mazuri sana kuhusu karama yenu ni ukaribu na masikini, waliokataliwa, na wale waliowekwa kando na jamii na mkawasemea  mkawachukoa  lakini bila kuwaondolea uhuru na mkawafanya watembee nanyi. Hili ni jambo zuri sana.” Baba Mtakatifu aidha amesema “Karama hukua, lakini kila mara hukua na karama ile ile iliyofanya maisha.” Papa ameongeza kusema: “Ni kwa jinsi gani ninavyopenda wakati mnakwenda mitaani, kuchukua vijana waliopotea katika udanganyifu wa maisha na kuwapa sababu ya kuishi, sababu ya kukua. Na aninapenda sana mnapokwenda kwa watoto.” Papa amesisitiza kuwa alipomwona  Chiara akiwa na watoto  alijua kuwa watoto ni ahadi. “Tumwombe Mungu ili  mwanzilishi aweze kusonga mbele kwa ujasiri na kupanda karama, na kisha kwa washiriki, ambao ni wema, hawa wanne kwa watano walio karibu naye. Amewasalimu sana na kuwapa baraka zake na ameomba wamwombee na sio  kinyume chake! Hatimaye aliwaptia Baraka za Mungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kwa heri Chiara, ninakutakia kila la kheri na uendelee mbele!” Papa alihitimisha ujumbe wake kwa njia ya video.

Ujumbe wa Papa kwa Nuovi Orizzonti
20 May 2024, 17:25