Tafuta

Makombora ya Urussi kushambulia Kharkiv Ukraine. Makombora ya Urussi kushambulia Kharkiv Ukraine. 

Papa Francisko:tunahitaji amani wakati huu wa vita vya dunia

Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito mara baada ya katekesi yake kuombea amani ulimwengu huu katika vita.Amehimiza kwa mara nyingine tena kutosahau Ukraine,Palestina,Israel,Myanmar na nchi zote zinazokumbwa na migogoro duniani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Sio tena vipande, lakini vita vya ulimwengu  halisi. Ni maneno ya uchungu yaliyotamkwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kuhitimisha katekesi yake, akiwa anatoa salamu mbali bali kwa maefu ya waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanaja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 22 Mei 2024. Papa alisema  “Tunaomba amani. Tunahitaji amani. Dunia iko vitani.”

Kufikiria juu ya Ukraine, Mashariki ya Kati, Myanmar

Papa aidha akijitenga na  hotuba iliyoandikwa na kuorodhesha nchi zinazoteseka kutokana na migogoro alisema: Ukraine, ambapo mvua ya ndege zisizo na rubani za Urussi zinaendelea; Mashariki ya Kati, ambapo idadi ya vifo kutokana na milipuko ya mabomu inaendelea; Myanmar, pamoja na mgogoro wa ndani na huko janga la Rohingya.  “Tusisahau Ukraine inayoteswa ambayo inateseka sana. Tusisahau Palestina, Israel: acha vita hivi vikome. Tusisahau Myanmar na tusisahau nchi nyingi kwenye vita. Kaka  na dada, tunahitaji kuombea amani wakati huu wa vita vya ulimwengu.” Alitoa wito Baba Mtakatifu Francisko.

Mwaliko kwa watoto

Amani ambayo kila mtu, kwa mchango wake, anaweza kuijenga. Hata watoto. Katika salamu zake kwa mahujaji wa Poland Papa Francisko, akiwahutubia vijana wote wanaosherehekea Komunyo yao ya Kwanza, alisema mkutano muhimu na Yesu, aliwahimiza katika wakati huu wa furaha kuweza pia kuona mahitaji ya wenzao ambao wanateseka, waathirika wa vita, njaa na umaskini. Maria atufundishe huduma ya unyenyekevu ambayo ni chemchemi ya amani duniani na Kanisani. Alisema papa

Uhaba wa miito nchini Italia

Katikati ya majanga ya dunia, Papa  Francisko pia alitoa tafakari fupi kuhusu matatizo katika Kanisa, kama vile mgogoro wa ukosefu wa miito. Katika kuwasalimia Waitaliano, aliwatazama watawa waliokuwepo katika uwanja wa Mtakatifu Petro , na kusema: "Ninawaona hawa wanovisi na ninajiuliza: Waitaliano ni wangapi? Huh? Wachache... Kuna uhaba wa miito katika maisha ya wakfu nchini Italia.

Papa atoa wito wa kusitisha vita duniani
22 May 2024, 16:49